Rais Mwingine Aenda Kutibiwa Nje

Rais Mwingine Aenda Kutibiwa Nje

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,154
Reaction score
13,267



Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amepelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu.



Malinzia amepelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu, ingawa haikuelezwa anasumbuliwa na kitu gani.


Lakini alipozungumza na gazeti hili, Malinzi amesema kweli yuko nchini India kwa ajili ya matibabu lakini ni ya kawaida kila mwaka.


“Nimekuwa nikipenda kufanya uchunguzi wa afya kila mwaka. Hivyo niko India kwa ajili ya uchunguzi wa kiafya.


“Baada ya kukamilisha kila kitu, ninatarajia kurejea nyumbani baada ya wiki siku chache kuendelea na majukumu,” alisema Malinzi.

Hivi karibuni, Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Jakaya Kikwete alifanyiwa upasuaji wa tezi dume nchini Marekani.

chanzo: saleh jembe blogspot
 
hapana watu8 najigharamia mwenyewe,nimekuja kwa ajili ya kufanya annual medical check up,huu ni mwaka wa tano mfulululizo ninafanya hivyo.Ni vyema kukagua afya zetu mara kwa mara na India gharama ni nafuu sana.
Ok Kiongozi, uwe na Wakati mzuri, mungu akutie nguvu.
 
Kwa nguvu za Mungu ma dr wasikukute na lolote baya!
 
Safi sana Mzee kwa kujali afya...routine check up ni muhimu sana ingawa wengi wetu tunapuuzia!<br><br>Kila la heri na InshaAllah, urudi salama!
 
hapana watu8 najigharamia mwenyewe,nimekuja kwa ajili ya kufanya annual medical check up,huu ni mwaka wa tano mfulululizo ninafanya hivyo.Ni vyema kukagua afya zetu mara kwa mara na India gharama ni nafuu sana.

Asante mkuu kwa kuondoa huu utata...

Ni vyema haswa watu kufanya uchunguzi wa afya kwa ujumla kama ulivyoshauri...

Nchi kama ya China nao wana gharama nafuu kidogo za utabibu na ni moja kati ya nchi ninazozikubali kwenye tasnia ya utabibu...

Kila la kheri urejee salama mkuu...
 
Last edited by a moderator:
Huenda wengine tukadhani ni status na position but I can imagine watu hapa hapa wana opt soda badala ya machungwa sembuse check up..!!!!!!!!
 
hapana watu8 najigharamia mwenyewe,nimekuja kwa ajili ya kufanya annual medical check up,huu ni mwaka wa tano mfulululizo ninafanya hivyo.Ni vyema kukagua afya zetu mara kwa mara na India gharama ni nafuu sana.

Huaminiki kwa mambo ya fedha na ndio maana umemuweka jamaa yako kama treasurer wa TFF; hii safari lazima umechukua fungu toka TFF kwa kupitia malango wa nyuma!! Nafsi yako inajua hilo na itakusuta!!
 
Back
Top Bottom