DeepPond
JF-Expert Member
- Nov 18, 2017
- 40,552
- 99,395
Nimesikiliza hotuba ya Rais Museveni akihutubia viwanja vya Ikulu, jijini Dar.
Ameongea mambo mengi ya msingi sana. Kama humjui unaweza kusema anaongoza taifa tajiri zaidi duniani.
Anasema Afrika ina utajiri mkubwa wa rasilimali lakini ina umaskini mkubwa sana wa kipato. Ametolea mfano wa nchi ya Japan na kusema haina gesi, madini, mbuga, wala mafuta lakini ni moja ya nchi tajiri sana Ulimwenguni.
Akaongezea kua maendeleo ya Japan ni kwa sababu ya uongozi bora.
Ukimsikiliza kwa makini RAISI Mseveni Akiongea, utadhani kama ndio anagombea Urais kwa mara ya kwanza ili akafanye mabadiliko chanya kuliinua taifa lake.
Kumbe ni mtu mwenyewe amekaa madarakani kwa zaidi ya miaka 35.
Yaani Anaongea kama kiongozi shupavu mwenye mikakati ya kuikomboa nchi yake na Lindi la umaskini.
Yani ukimsikiliza kwa makini, huwezi amini kama yeye ndio aliekopa pesa Exim bank CHINA, akaweka rehani uwanja wa ndege wa Entebe, ambao umechukuliwa na wachina hivi karibuni baada kushindwa kurejesha deni.
Afrika sijui aliyetuloga ni nani?