Rais Museven ni Alama ya Viongozi wa hovyo kabisa barani Afrika

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,452
99,074
Nimesikiliza hotuba ya Rais Museveni akihutubia viwanja vya Ikulu, jijini Dar.

Ameongea mambo mengi ya msingi sana. Kama humjui unaweza kusema anaongoza taifa tajiri zaidi duniani.

Anasema Afrika ina utajiri mkubwa wa rasilimali lakini ina umaskini mkubwa sana wa kipato. Ametolea mfano wa nchi ya Japan na kusema haina gesi, madini, mbuga, wala mafuta lakini ni moja ya nchi tajiri sana Ulimwenguni.

Akaongezea kua maendeleo ya Japan ni kwa sababu ya uongozi bora.

Ukimsikiliza kwa makini RAISI Mseveni Akiongea, utadhani kama ndio anagombea Urais kwa mara ya kwanza ili akafanye mabadiliko chanya kuliinua taifa lake.

Kumbe ni mtu mwenyewe amekaa madarakani kwa zaidi ya miaka 35.

Yaani Anaongea kama kiongozi shupavu mwenye mikakati ya kuikomboa nchi yake na Lindi la umaskini.

Yani ukimsikiliza kwa makini, huwezi amini kama yeye ndio aliekopa pesa Exim bank CHINA, akaweka rehani uwanja wa ndege wa Entebe, ambao umechukuliwa na wachina hivi karibuni baada kushindwa kurejesha deni.

Afrika sijui aliyetuloga ni nani?

IMG-20211128-WA0007.jpg
 
Uganda ni nchi ndogo Ila inatufukuzia vizuri, Sisi Tanzania tunabadili kwa kupokezana Uongozi Ila tatizo letu ni Lile Alilolisema Abrianna
 
We, uwanja wa ndege umejaa matangazo katika madirisha na kuta zake, what a joke!
 
'Some people think that being in the government for a long time is a bad thing. But the more you stay, the more you learn. I am now an expert in governance'
Yoweri K. Museveni
 
Bara la Afrika ni mhanga wa biashara ya utumwa, ukoloni wa kale uliotokea mara baada mkutano wa Berlin na ukoloni mamboleo. Matukio haya yameathiri sana ustaarabu wa asili bara hili.

Tamaduni mseto iliyozaliwa baada uhanga huo ndiyo sababu kuu iliyopelekea kupoteza thamani ya ustaarabu wa awali uliokuwepo hapo kabla. Hiki ni kitu ambacho kimezalisha uduni katika masuala ya utawala na uongozi kwa viongozi tuliokuwa nao hivi sasa.

Tofauti na viongozi wa Asia, ijapokuwa nao walitawaliwa na kuwa watumwa, lakini waliendelea kudumisha tamaduni zao za asili. Pamoja na kurithi baadhi ya mazuri yaliyopo katika tamaduni za kigeni, lakini bado walidumisha misingi ya tamaduni zao za asili.

Afrika inapaswa ku "trace back" wapi ambapo iliingizwa chaka. Ni jambo rahisi sana kufanyika. Ni wakati sasa wa kutafuta katiba mpya, katiba ambayo itaweka mazingira bora ya kuibua fikra pevu na kuchochea mijadala yenye tija katika kutafuta majibu ya changamoto kubwa zinazokabili maendeleo ya bara letu.
 
Maendeleo ya Africa ni kurudi kinyumenyume na si kusonga mbele,viongozi wakisha jineemesha na wapendwa wao basi wanakaa na kutulia na kuanza kulinda maslahi yao
 
Mbona hawaigi Sera za uchumi za Japan za miaka 1930s na baada ya WWII?
 
Nimesikiliza hotuba ya Rais Museveni akihutubia viwanja vya Ikulu, jijini Dar.

Ameongea mambo mengi ya msingi sana. Kama humjui unaweza kusema anaongoza taifa tajiri zaidi duniani...
Over 60 years old hifai kuwa kwenye nafasi yyt ya maamuzi, must stay home kuwasimulia ja being grand child kuwasimulia watoto hadithi za ujana wako.
 
Mwingine ni dikteta Paul Kagame naye anapenda kutoa lectures za maendeleo sana.
 
Tatizo kubwa la viongozi Africa ni ujinga kupendwa kutukuzwa. Tunajenga watu badala ya mifumo na taasis imara.

" Mimi ninajua mengi...." Inazuia ubunifu, ujasiri mpaka kila Jambo mkuu alielewe atoe baraka zake, inategemea kamka vipi!
 
Back
Top Bottom