Rais Mteule, Magufuli aanza kutema ''cheche'' ndani ya CCM.

Rais Mteule, Magufuli aanza kutema ''cheche'' ndani ya CCM.

Chama kinaendeshwa kwa siasa sio amri na ubabe ndo maana mwalimu alisema ccm ni kama kokoro
 
Watanzania ni wepesi mno wa kuingizwa mkenge na lip service.

Jiulize, miaka yote hiyo akiwa mwanachama wa CCM na waziri, mbona alikuwa hayasemi hadharani haya?

Halafu, watu kama sisi...we've seen this movie before.

Mwinyi alikuja na blah blah za fagio la chuma. Mkapa akaja na porojo za uwazi na ukweli. Mkweere akaja na tiralila za ari mpya, kasi mpya, na sijui nguvu mpya na mambo ya maisha bora kwa kila Mtanzania.

Wote hao hamna kitu cha maana walichokifanya.

I am not falling for this kind of BS.

Ni kama ninyi mlivyoingizwa Mkenge na akina Sumaye Mtu aliyekaa kwenye uwaziri mkuu muda mrefu kuliko yeyote yule,halafu anawaambia CCM haijafanya lolote tokea uhuru,na pia eti wao ndio wataleta mabadiliko.Kwanini msingewauliza walishindwaje kuyaleta ndani ya CCM?wanaishia kuwadanganya mfumo ndio tatizo,bila kufafanua huo mfumo ni upi,ulianza lini?na mwasisi wake ni nani?na pia je,huo mfumo kuna ugumu gani wa kuuvunja?Mwisho wa yote unagundua ni propaganda za kisiasa
 
Chama kinaendeshwa kwa siasa sio amri na ubabe ndo maana mwalimu alisema ccm ni kama kokoro

Chama kinaendeshwa na katiba ya chama sio siasa.Na yeyote anayeivunja katiba ya chama yafaa akemewe hadharani
 
Ni kama ninyi mlivyoingizwa Mkenge na akina Sumaye Mtu aliyekaa kwenye uwaziri mkuu muda mrefu kuliko yeyote yule,halafu anawaambia CCM haijafanya lolote tokea uhuru,na pia eti wao ndio wataleta mabadiliko.

Nani aliingizwa mkenge na akina Sumaye?

Kwanini msingewauliza walishindwaje kuyaleta ndani ya CCM?

Usitumie wingi. Mimi sina chama ila niko anti-CCM. Na sikuwa na haja ya kumwuliza mtu aliyetoka CCM. Nikitaka kuuliza ntawauliza CCM kwa nini wameshindwa kuboresha maisha ya Watanzania licha ya kukaa madarakani zaidi ya nusu karne.

wanaishia kuwadanganya mfumo ndio tatizo,

Mfumo gani ndo tatizo?

bila kufafanua huo mfumo ni upi,

Unazungumzia mfumo wa CCM?

ulianza lini?

Kama unazungumzia mfumo wa CCM basi huo ulianza na CCM ikiwa madarakani.

na mwasisi wake ni nani?

Kama unazungumzia mfumo wa CCM ni wazi muasisi wake ni hilo hilo dubwasha liitwalo CCM.

na pia je,huo mfumo kuna ugumu gani wa kuuvunja?

Kama unazungumzia mfumo wa CCM basi ugumu wa kuuvunja ni hofu yao ya kupoteza fursa za maslahi ya mnufaiko.

Mwisho wa yote unagundua ni propaganda za kisiasa

Kuna propaganda za kisiasa kuzidi hizi: Fagio la chuma - Mwinyi, Uwazi na ukweli - Mkapa, Maisha bora kwa kila Mtanzania - Kikwete, na Hapa kazi tu - Magufuli.
 
Nani aliingizwa mkenge na akina Sumaye?



Usitumie wingi. Mimi sina chama ila niko anti-CCM. Na sikuwa na haja ya kumwuliza mtu aliyetoka CCM. Nikitaka kuuliza ntawauliza CCM kwa nini wameshindwa kuboresha maisha ya Watanzania licha ya kukaa madarakani zaidi ya nusu karne.



Mfumo gani ndo tatizo?



Unazungumzia mfumo wa CCM?



Kama unazungumzia mfumo wa CCM basi huo ulianza na CCM ikiwa madarakani.



Kama unazungumzia mfumo wa CCM ni wazi muasisi wake ni hilo hilo dubwasha liitwalo CCM.



Kama unazungumzia mfumo wa CCM basi ugumu wa kuuvunja ni hofu yao ya kupoteza fursa za maslahi ya mnufaiko.



Kuna propaganda za kisiasa kuzidi hizi: Fagio la chuma - Mwinyi, Uwazi na ukweli - Mkapa, Maisha bora kwa kila Mtanzania - Kikwete, na Hapa kazi tu - Magufuli.

Naona hapo umekwepa kumtaja Nyerere kwenye hizo propaganda ukizoziorodhesha hapo chini
 

mimi tangu nianze kumsikiliza Magufuli sio mwanasiasa wa kawaida, na ndio naona ni vizuri tukimpata mtu ambaye sio breed ya kawaida ya wanasiasa tuliozoea itakuwa vizuri sana.
Kuna baadhi ya watu wanataka kiongozi mkuu wa CCM afanane na viongozi wakuu wa zamani!

WanaCCM wanataka mabadiliko ya kiuongozi. Hawataki kiongozi ajaye afanane na waliopita.

WanaCCM wengi wamemchagua Magufuli. Wapiga kura wengi wamemchagua Magufuli.

Haya mengine ni story tu ambazo zinachagizwa na mitazamo tofauti na ile ya Watanzania waliomchagua Magufuli.
 
Japokuwa sipendi CCM ,hila Magufuli nilimkubali kitambo sana ,nilipenda Wapinzani wachukue nchi lakini aikuwezekana.Lakini naamini Magufuli akipewa ushirikiano mzuri na Sisi Watanzania wote huyu jamaa anaweza kufanya mambo makubwa sanaa.


Watanzania hawakumchagua so hawezi kupewa ushirikiano!
 
Haya...kuna propaganda kuzidi ule ujinga wa 'zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa CCM'?

Fikra zake zilikuwa sahihi kwa mujibu wa nini?

Nilidhani utaitaja ile ya siasa ya ujamaa na kujitegemea,ambayo yeye Nyerere alikuwa anainadi hadi umauti,nadhani na wewe unajua kutokana na msimamo aliokuwa nao kwa kiasi kikubwa alifanikiwa kuifanya nchi kuwa ya kijamaa na kujitegemea.Ndio maana rais Mteule Dr.Magufuli anaposema hapa kazi tu,Watanzania tuliomchagua tunamuelewa hasa kwa kurejea rekodi yake ya kusimamia mambo mbalimbali katika wizara alizosimamia.
 
Anapozungumza hayo watu wameufyata au wanampigia makofi ?

kama wanampigia makofi basi ujuwe wanamcheka na kumuona Magufuli katika hali yake ,Magufuli haielewi CCM kiundani na tupo hapa hapa nawapa miezi mitatu tu ,lazima apige push up ikulu.
 
Chama kinaendeshwa kwa siasa sio amri na ubabe ndo maana mwalimu alisema ccm ni kama kokoro
Nani amekwambia chama hakiendeshwi na katiba?

Kwa hiyo unataka kusema unafiki unakubalika ndani ya katiba?
 
Hizi ni fikra zako na una haki ya kufikiria hivyo lakini nadhani fikra zako ni kama kupiga ramri!

Kwa kuwa Pombe ni mropokaji anawasaidia mahacmu wake ndani ya chama kujipanga mapema na ninaamini watamtengenezea mazinira magumu sana ya kikazi. Anaujua MTANDAO???
 
Akimfukuza Pinda kwa kutoshiriki kampeni nitamsifu sana pia tutampa orodha ya kila mkoa
 
Alivyokuwa waziri Ni mchapa kazi sawa ila ngoja tuone atakavyokuwa raisi wa jamhuri ya muungano na pia mwenyekiti wa chama
 
Siasa za 'kutema cheche'
na 'kutingisha' zimeshapitwa na wakati.....
Angejifunza 'boardroom' politics...
Ameanza kampeni za kuwa Mwenyekiti wa chama, he can't wait for Kikwete to die of old age any less than Mkapa waited anxiously for Mwalimu to abscond so you can assume plenary powers within the party and country, kwa sababu huwezi kuwa Rais kamili ilhali aliyekuweka Ikulu kwa hisani yake bado anakupumulia pumulia kisogoni kila unapokwenda.

But that was a false start, he was very unpresidential and very unstatesmanlike. Badala ya kujenga madaraja ndani na nje ya chama anaendeleza kampeni against Lowassa na siasa za vita ndani ya chama ilhali nchi na chama viko politically charged and wounded right now. He is very unprepared for office of president. I mean, he couldn't be more ridiculous. Very dictatorial.
 
Mwambieni aandae na yeye ndg zake! Ccm bila kuendeleza uko si jambo njema!
 
Kuna viongozi wengi sana ndani ya chama kwa sasa wana wasiwasi na hatima yao.

Magufuli ''hakopeshi''.

The guy calls a spade a spade.

And they will sabotage Him from the Start to the End! Ameanza na gear mbaya, those guys are not just mere members but also powerful members in the party, and they are many! Naanza kumuhurumia, hii ni gear aliyopaswa kuitumia katikati ya safari baada ya kuwatambua wote na namna bora ya kuondokana nao!
 
Nasita kuamini unachosema.Ninawasiwasi hii nchi itakuwa kama Russia kipindi Puttin alipopumzika. Behind the curtains Puttin alikuwa bado raisi. Hiki ndicho kitakachotokea kwa Magufuli. The man will only be a ceremonial leader, JK will be running the show behind close doors. Mark my words #

Mkapa, not Kikwete! Mark my Words
 
CCM wana utaratibu baada ya Rais kuapishwa, Mwenyekiti wa CCM-Taifa hujiudhuru wadhifa wake na kumwachia Rais aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM-Taifa.

Baada ya Magufuli kuapishwa, CCM wataitisha Mkutano Mkuu ili Rais Kikwete akabidhi Uenyekiti wa Taifa kwa Magufuli.

Hadi mwaka 2017 mwenyekiti aliyepo atakapokuwa anamaliza miaka yake mitano ya uenyekiti.
 
Back
Top Bottom