Rais Mteule, Magufuli aanza kutema ''cheche'' ndani ya CCM.

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,055
Wakati akiongea na umati wa wanaCCM na wananchi wengine katika ofisi za CCM, Lumumba waliojitokeza kumlaki baada ya kupokea cheti cha kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania, Magufuli amesema Mwenyekiti wa CCM-Taifa, Rais Kikwete alikuwa ameruhusu wanafiki ndani ya chama.

Magufuli amesema ni mara kumi uwe na mpinzani kutoka nje kuliko kuwa na mpinzani ndani ya CCM kwa sababu mipango yetu tunaifanya mchana halafu wao wanaenda kuitoa mipango yetu usiku. wapinzani ndani ya CCM ni wabaya zaidi ya mchawi kwa sababu mchawi atakuroga ufe kuliko kukaa na mnafiki ndani ya chama.

Magufuli alisema, ''Mweshimiwa Mwenyekiti wangu wa Taifa naomba unisamehe lakini ukweli utabakia kuwa ukweli. Wewe ni Mwenyekiti wangu wa Taifa lakini ulikaa na wanafiki ndani ya chama ambao kwa kiasi kikubwa wametufanya tufike hapa tulipo''.

Magufuli aliendelea kusema, ''Kwa hiyo ninakuomba Mwenyekiti wangu mpendwa ukitengeneze chama chetu vizuri. Usiwaonee huruma wanafiki. Ukishamgundua mnafiki leo, usikae naye, fukuza kesho''.

Magufuli alisema, ''Ni mara kumi tubaki na wanachama wachache kuliko kukaa na wanachama wanafiki wanatuhujumu na kusabisha kushindwa kufika kwenye malengo yetu ya chama''.

''Naomba Mwenyekiti wangu unisamehe kwa kulisema hili kwa sababu kama nisingelisema lingekaa kama kiungulia ndani ya moyo wangu wakati nimekumbana nalo sana wakati nafanya kampeni sehemu mbali mbali nchini'', Alisema.

Magufuli alimalizia kwa kusema, ''Mheshimiwa Mwenyekiti wangu, naungana na wewe kwa kumpongeza Katibu Mkuu, Kinana kwa kukilinda chama chetu kwa vile amekuwa mkweli na muwazi. Mwenyezi Mungu amemsaidia''.

Video ya alichokisema, Magufuli.
 
Last edited by a moderator:
kabisa, inabidi kwanza hawahakikishie wananchi kwamba yeye ndiye ataongoza nchi, na watu wajiandae :lock1:
 
Hata baba riz alianza na kiki za kujidai anatembelea hosptal ...baada 2mths akaanza safari za kufanya massage marekani na ulaya
 
Acheni ututusa huo!:Huyo Magufuli ni NANI ndani ya chama? Hata aweze kukisafisha chama.

Je! Yeye ni mwenyekiti wa chama? Je! Labda yeye ni katibu mkuu, makamu mnykti?

Ni NANI chamani!

Yalimshinda Kinana.

CCM ni ile ile.CCM INA wenyewe babu!
 
Last edited by a moderator:
kabsa, inabidi kwanza hahakikishe kwamba yeye ndiye ataongoza nchi, na watu wajiandae :lock1:
Baadhi ya viongozi wa CCM na wafanyakazi waandamizi wa serikali kwa sasa watakuwa wana wasi wasi mkubwa wa maisha yao ndani ya chama na serikali.
 
Hata baba riz alianza na kiki za kujidai anatembelea hosptal ...baada 2mths akaanza safari za kufanya massage marekani na ulaya
Baba riz ndiye nani?

Kwa nini unaandika kwa kutumia format ya text message?
 
Alichosema ni sahihi kabisa, watu wanafiki ni kuwafukuza kwenye chama tuu. hata wenye tuhuma za ufisadi wengine bado wapo ndani ya ccm ni kuwatimulia mbali. ili kurejesha misingi ya awali.
 
Hii ni nguvu ya Soda, ndani ya miaka miwili atakuwa amebadilika kabisa. Huwezi kuwa CCM na ukawa na uwezo wa kusimamia maslahi ya Taifa kwa asilimia mia moja. Kwani walioko chini yake watamwacha apete namna hiyo?
 
Siasa za 'kutema cheche'
na 'kutingisha' zimeshapitwa na wakati.....
Angejifunza 'boardroom' politics...
 
No......kwa muono wangu hataweza hata kidogo.Hapo CCM ni Majungu Ltd na asipoangalia atashindwa kabisa.Mtihani wa kwanza ni ZEC na uchaguzi wa huko...zigo hilo atatupiwa.
 
Acheni ututusa huo!:Huyo Magufuli ni NANI ndani ya chama? Hata aweze kukisafisha chama.

Je! Yeye ni mwenyekiti wa chama? Je! Labda yeye ni katibu mkuu, makamu mnykti?

Ni NANI chamani!

Yalimshinda Kinana,
CCM wana utaratibu baada ya Rais kuapishwa, Mwenyekiti wa CCM-Taifa hujiudhuru wadhifa wake na kumwachia Rais aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM-Taifa.

Baada ya Magufuli kuapishwa, CCM wataitisha Mkutano Mkuu ili Rais Kikwete akabidhi Uenyekiti wa Taifa kwa Magufuli.
 
Alichosema ni sahihi kabisa, watu wanafiki ni kuwafukuza kwenye chama tuu. hata wenye tuhuma za ufisadi wengine bado wapo ndani ya ccm ni kuwatimulia mbali. ili kurejesha misingi ya awali.

Wengine wameshakuwa wabunge tayari sasa mtaufuta ubunge wake au ilikuaje akapitishwa kugombea ubunge
 
Siasa za 'kutema cheche'
na 'kutingisha' zimeshapitwa na wakati.....
Angejifunza 'boardroom' politics...

Watanzania ni wepesi mno wa kuingizwa mkenge na lip service.

Jiulize, miaka yote hiyo akiwa mwanachama wa CCM na waziri, mbona alikuwa hayasemi hadharani haya?

Halafu, watu kama sisi...we've seen this movie before.

Mwinyi alikuja na blah blah za fagio la chuma. Mkapa akaja na porojo za uwazi na ukweli. Mkweere akaja na tiralila za ari mpya, kasi mpya, na sijui nguvu mpya na mambo ya maisha bora kwa kila Mtanzania.

Wote hao hamna kitu cha maana walichokifanya.

I am not falling for this kind of BS.
 
Kwa haya anakazi kushinda awamu ya pili.
Angeweza kufanya huo ubabe enzi za chama chama kimoja. Lakini sasa hivi hao "wanafiki" wanapa kukimbilia.
Wata frustrate ata hiyo miaka mitano atamaliza kwa shida.
 
CCM wana utaratibu baada ya Rais kuapishwa, Mwenyekiti wa CCM-Taifa hujiudhuru wadhifa wake na kumwachia Rais aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM-Taifa.

Baada ya Magufuli kuapishwa, CCM wataitisha Mkutano Mkuu ili Rais Kikwete akabidhi Uenyekiti wa Taifa kwa Magufuli.
Utaratibu ni anakabidhi baada ya miaka miwili, yaani akiachia urais anaendelea kuwa mwenyekiti kwa miaka miwili ili kumpa crash course mwenyekiti ajaye.
 
Back
Top Bottom