Rais Mteule, Magufuli aanza kutema ''cheche'' ndani ya CCM.

Rais Mteule, Magufuli aanza kutema ''cheche'' ndani ya CCM.

Safi sana taasisi imara inajengwa na watu wenye agenda moja, message tosha kwa wananchi na wanachama wazandiki things are about to change.

Goooo Magufuli the good thing hana mtu wa kumlipa fadhila zaidi ya chama kilichompa nafasi na wanachama wanaokiamini kutendewa haki god bless Magufuli.
 
Wengine wameshakuwa wabunge tayari sasa mtaufuta ubunge wake au ilikuaje akapitishwa kugombea ubunge
Mbunge ni mtumishi wa wananchi wote.

Wenye uamuzi wa mwisho wa kumchagua mbunge ni wapiga kura ambao wengi wao siyo wanachama wa vyama vya siasa.
 
Kwa haya anakazi kushinda awamu ya pili.
Angeweza kufanya huo ubabe enzi za chama chama kimoja. Lakini sasa hivi hao "wanafiki" wanapa kukimbilia.
Wata frustrate ata hiyo miaka mitano atamaliza kwa shida.
Amesema ni afadhari kuwa na wanachama wachache ambao siyo wanafiki.
 
Utaratibu ni anakabidhi baada ya miaka miwili, yaani akiachia urais anaendelea kuwa mwenyekiti kwa miaka miwili ili kumpa crash course mwenyekiti ajaye.
CCM huwa hawasubiri mpaka kipindi cha uongozi wa Mwenyekiti wa Taifa kimalizike baada ya Uchaguzi Mkuu. Historia inaonyesha hivyo ukiondoa kipindi cha uongozi wa Mwl. Nyerere.
 
Wakati akiongea na umati wa wanaCCM na wananchi wengine katika ofisi za CCM, Lumumba waliojitokeza kumlaki baada ya kupokea cheti cha kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania, Magufuli amesema Mwenyekiti wa CCM-Taifa, Rais Kikwete alikuwa ameruhusu wanafiki ndani ya chama.

Magufuli amesema ni mara kumi uwe na mpinzani kutoka nje kuliko kuwa na mpinzani ndani ya CCM kwa sababu mipango yetu tunaifanya mchana halafu wao wanaenda kuitoa mipango yetu usiku. wapinzani ndani ya CCM ni wabaya zaidi ya mchawi kwa sababu mchawi atakuroga ufe kuliko kukaa na mnafiki ndani ya chama.

Magufuli alisema, ''Mweshimiwa Mwenyekiti wangu wa Taifa naomba unisamehe lakini ukweli utabakia kuwa ukweli. Wewe ni Mwenyekiti wangu wa Taifa lakini ulikaa na wanafiki ndani ya chama ambao kwa kiasi kikubwa wametufanya tufike hapa tulipo''.

Magufuli aliendelea kusema, ''Kwa hiyo ninakuomba Mwenyekiti wangu mpendwa ukitengeneze chama chetu vizuri. Usiwaonee huruma wanafiki. Ukishamgundua mnafiki leo, usikae naye, fukuza kesho''.

Magufuli alisema, ''Ni mara kumi tubaki na wanachama wachache kuliko kukaa na wanachama wanafiki wanatuhujumu na kusabisha kushindwa kufika kwenye malengo yetu ya chama''.

''Naomba Mwenyekiti wangu unisamehe kwa kulisema hili kwa sababu kama nisingelisema lingekaa kama kiungulia ndani ya moyo wangu wakati nimekumbana nalo sana wakati nafanya kampeni sehemu mbali mbali nchini'', Alisema.

Magufuli alimalizia kwa kusema, ''Mheshimiwa Mwenyekiti wangu, naungana na wewe kwa kumpongeza Katibu Mkuu, Kinana kwa kukilinda chama chetu kwa vile amekuwa mkweli na muwazi. Mwenyezi Mungu amemsaidia''.

Video ya alichokisema, Magufuli.


Hata yeye naye ni mnafiki?Kwa nini hakumwambia bosi wake kuwa kuna watu kadhaa ni wanafiki
 
Last edited by a moderator:
Haya mawazo yako yakichagizwa na fikra zako!

Umenatumia kigezo gani kufikia hitimisho lako?

Mbona hata Kikwete aliaanza na mkwara huo huo..na baadae mpaka sasa wewe mwenyewe unajua maisha yetu yalivyokuwa ovyo?kasi ya maadui wakubwa ujinga,umaskini nk vimeongezeka kwa kasi ya ajabu?Mkapa naye ilikuwa hivyo hivyo sasa tutumie vigezo gani tena kama mabosi waliomweka walikuja kwa stairi hiyo hiyo!!
 
Japokuwa sipendi CCM ,hila Magufuli nilimkubali kitambo sana ,nilipenda Wapinzani wachukue nchi lakini aikuwezekana.Lakini naamini Magufuli akipewa ushirikiano mzuri na Sisi Watanzania wote huyu jamaa anaweza kufanya mambo makubwa sanaa.
 
Hajaongelea nani anaua TEMBO..? Nani katoa ruhusa TWIGA kupanda ndege..? Au hadi aapishwe atasema HAYA.. na mengine...? IPTL, Mikataba ya Gas, UDA, Katiba Mpya ya Wananchi... au anangojea KUAPISHWA..? Ila si anajua nani anamaliza TEMBO..? Naona anasifia mbuyu aliokalia ataukata kweli...? Fiction..? Or...
Historia inaonyesha utendaji wake lakini kikubwa tusubiri anapokuwa Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM-Taifa.
 
Magufuli namwaminia sana
Mungu amjalie apambane na mafisadi na wala rushwa
 
Alichosema ni sahihi kabisa, watu wanafiki ni kuwafukuza kwenye chama tuu. hata wenye tuhuma za ufisadi wengine bado wapo ndani ya ccm ni kuwatimulia mbali. ili kurejesha misingi ya awali.

Mwenyekiti atafukuzaje wanafiki na yeye ni mnafiki namba wani? Jamani a leader sets the tone na wengine wanafuata. A leader aliendekeza tabia fulani walioko chini nao wana adapt. Attitude is contagious. Acheni kuogopa kumwambia ukweli.
 
Japokuwa sipendi CCM ,hila Magufuli nilimkubali kitambo sana ,nilipenda Wapinzani wachukue nchi lakini aikuwezekana.Lakini naamini Magufuli akipewa ushirikiano mzuri na Sisi Watanzania wote huyu jamaa anaweza kufanya mambo makubwa sanaa.
Nasita kuamini unachosema.Ninawasiwasi hii nchi itakuwa kama Russia kipindi Puttin alipopumzika. Behind the curtains Puttin alikuwa bado raisi. Hiki ndicho kitakachotokea kwa Magufuli. The man will only be a ceremonial leader, JK will be running the show behind close doors. Mark my words #
 
..angeanza na mafisadi na wazembe ndani ya ccm.

..hii habari ya wanafiki ndani ya ccm nimeisikia ktk kampeni hizi.

..halafu huyu mzee aache kuzungumzia habari za wachawi na kurogana.

..this was supposed to be his victory speech, sasa mambo aliyoyazungumza hovyo kabisa.

cc MsemajiUkweli, The Boss, Nyani Ngabu, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
Alichosema ni sahihi kabisa, watu wanafiki ni kuwafukuza kwenye chama tuu. hata wenye tuhuma za ufisadi wengine bado wapo ndani ya ccm ni kuwatimulia mbali. ili kurejesha misingi ya awali.

Aanze na wale waliopandikiza chuki ya ukabila,udini,ukanda na kutufanya wengine kuichukia ccm kuliko ukoma!
 
Nyie mmekariri mno magufuli ni kesi nyingine,uzuri akiamuaga lake huwa atetereshwi
 
Hii ni nguvu ya Soda, ndani ya miaka miwili atakuwa amebadilika kabisa. Huwezi kuwa CCM na ukawa na uwezo wa kusimamia maslahi ya Taifa kwa asilimia mia moja. Kwani walioko chini yake watamwacha apete namna hiyo?
Tumeisha sahau ya Mwinyi na fagio la chuma? Kikwete na Ziara za kila wizara pamoja na semina kali ya Ngurdoto? Mkapa na Ukweli na uwazi? Haya si maajabu ila ni kawaida mwanzoni. Ila bahati mbaya sasa ni technolojia ya habari imbadirika sana.
 
Mwenyekiti atafukuzaje wanafiki na yeye ni mnafiki namba wani? Jamani a leader sets the tone na wengine wanafuata. A leader aliendekeza tabia fulani walioko chini nao wana adapt. Attitude is contagious. Acheni kuogopa kumwambia ukweli.
You're right on the money!

Ninaamini uongozi na utawala wa Magufuli utaondoa unafiki ndani ya chama.

Tone ya Magufuli ilikuwa inatuma ujumbe kwa Rais Kikwete!
 
..angeanza na mafisadi na wazembe ndani ya ccm.

..hii habari ya wanafiki ndani ya ccm nimeisikia ktk kampeni hizi.

..halafu huyu mzee aache kuzungumzia habari za wachawi na kurogana.

..this was supposed to be his victory speech, sasa mambo aliyoyazungumza hovyo kabisa.

cc MsemajiUkweli, The Boss, Nyani Ngabu, Nguruvi3
Kama umeisikia hotuba yake amezungumza mengi, hiki kilikuwa ni sehemu ya yale aliyoyazungumza.

Kwako unaweza kuyaona mambo aliyoyazungumza niya hovyo lakini kwake ni mambo ya muhimu kuondolewa ndani ya chama ambacho yuko mbioni kuwa Mwenyekiti wake kitaifa.

By the way, hujawahi kuliona jema hata zuri la utendaji wa Magufuli. You're just boiling internally with anger and disappointment caused by Lowassa misadventure coupled with political sinking ship.
 
Back
Top Bottom