Rais mstaafu Mwinyi ana shamba la zaidi ya ekari 1,000 Mvomero, Morogoro

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Wakati Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye akiwa analalamikia kufutiwa hati ya mashamba yake mawili, serikali wilayani Mvomero imesema bado inahakiki mashamba ambayo hayajaendelezwa likiwemo la Rais wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.

Uongozi wa Mvomero umesema unahakiki ili kuona mashamba ambayo hayajaendelezwa na kuyafutia umiliki ili waweze kugawa upya kwa wananchi.
Shamba hilo, ambalo kwa mujibu wa serikali ya Kijiji cha Wami Luhindo lina ukubwa wa takriban ekari 1,000, linatumiwa kufugia ng’ombe na mbuzi.

Tamko hilo limetolewa na mkurugenzi wa halmashauri, Florent Kyombo alipohojiwa na gazeti hili kuhusu mashamba yasiyoendelezwa, huku kukiwa na wito kutoka wanasiasa wa upinzani wanaotaka Serikali ifute hati za mashamba yasiyoendelezwa ambayo yanamilikiwa na wanachama wa CCM.

Mkurugenzi huyo alisema tayari umiliki wa mashamba zaidi ya 10 yenye zaidi ya ekari 700 umeshabatilishwa na yamerejeshwa serikalini na wameshaanza kukaa vikao kwa ajili ya kuyapangia matumizi mengine. Alipoulizwa iwapo shamba linalomilikiwa na Rais Mwinyi lililopo Kijiji cha Wami Luhindo na jingine la mbunge wa Morogoro Mjini, Aziz Abood lililopo Milama ni miongoni mwa mashamba yaliyoombewa kufutiwa hati, alisema yanafanyiwa uhakiki.

“Mashamba yote makubwa, bila kujali linamilikiwa na nani tutayapitia na kuyahakiki uendelezaji wake, na iwapo tutabaini haujatosheleza kwa mujibu wa sheria tutayafuta,” alisema mkurugenzi huyo.

Mkurugenzi huyo hakuwa tayari kutaja ukubwa wa mashamba hayo kwa madai kuwa bado wapo katika hatua za awali za ufuatiliaji, akisema kutaja ukubwa ni sawa na kutoa hukumu kabla ya uhakiki.

Kyombo alisema halmashauri inachofanya ni kutekeleza agizo la Rais John Magufuli na kupeleka maombi ya kufuta mashamba pori yote, lakini wanachofanya ni kuhakikisha kuwa sheria zinafuatwa katika kubatilisha umiliki huo. Alipohojiwa kuhusu uendelezwaji wa shamba la Mwinyi lililopo Kijiji cha Wami-Luhindo, mwenyekiti wa kijiji hicho Apolinary Kahumba alisema shamba hilo lina mifugo.

“Katika shamba la Mzee Mwinyi kuna ng’ombe na mbuzi wengi. Kuhusu ukubwa wa eneo la shamba hilo, sina uhakika sana lakini halipungui ekari elfu moja,” alisema mwenyekiti huyo. Akizungumzia uhakiki huo, mwenyekiti wa halmashauri, Jonas Van Zeeland alisema Mvomero imedhamiria kuhakikisha mashambapori yote yanarejeshwa bila kujali yanamilikiwa na nani.

“Katika suala la ubatilishaji umiliki wa mashamba, nadhani hakuna haja ya kulaumiana kwa kuwa ni zoezi linaloendeshwa kisheria na hakuna uonevu unaofanywa wala utakaofanywa kwa mtu yeyote. Kama hujaendeleza shamba utanyang’anywa tu,” alisema Van Zeeland.

Sumaye, ambaye alikuwa waziri mkuu kati ya mwaka 1995-2005, amekuwa akilalamika kuwa Serikali inamuandama kwa kuwa alichukua uamuzi wa kuhama CCM na kujiunga na upinzani.

Awali, Rais alifuta hati ya umiliki wa shamba lake la Mabwepande lililopo jijini Dar es Salaam na kuwagawia watu waliovamia. Naye Abood, alisema limeendelezwa kama alivyoomba.

“Shamba langu lililopo kule ni la mifugo na kuna ng’ombe. Kila siku maziwa yanakuja mjini. Kwangu hakuna shambapori, naomba mnielewe,” alisema mbunge huyo ambaye pia anamiliki kiwanda ambacho Rais ametishia kumpokonya.
 
Subutu!!!!
 
Waacheni Wazee Wapumzike Kumbukeni Hao Hawawezi Kulima
Acha Tuone Ikiwa Kauli Iliyotolewa Tanga Mwijage Alipoambiwa Nyang'anya Yoyote Na Hawana Cha Kukufanya
 
Hili suala la kunyang'anya mashamba aliyekuwa anatafutwa ni Sumaye,wakishamaliza mashamba ya Sumaye zoezi litaishia hapohapo! Japo kuna wengine watakuwa wameathirika lakini hao ni chambo tu ili kumnasa Sumaye! Ni sawa na ile vita uchwara ya dawa za kulevya iliyoanzishwa na Bashite,aliyekuwa anatafutwa ni Mbowe lakini kamanda alipowaonesha kwamba hakamatwi kiboya zoezi likaishia hapohapo!
 
Kumbukumbu zinanikubusha mwishoni mwa miaka 98 mpaka elfu 2 aliyekuwa bosi wake Sumaye aliwahi kusema
Ukitaka mambo yakunyookee baki CCM
Sijui mzee wetu alielewa maana ya maneno yale
 
Hili suala la kunyang'anya mashamba aliyekuwa anatafutwa ni Sumaye,wakishamaliza mashamba ya Sumaye zoezi litaishia hapohapo! Japo kuna wengine watakuwa wameathirika lakini hao ni chambo tu ili kumnasa Sumaye! Ni sawa na ile vita uchwara ya dawa za kulevya iliyoanzishwa na Bashite,aliyekuwa anatafutwa ni Mbowe lakini kamanda alipowaonesha kwamba hakamatwi kiboya zoezi likaishia hapohapo!
mi uwa najiuliza kila siku kwann mbowe akukamatwa walivyo sema. kweli siasa hapa tz usanii 90%

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom