Rais Mama Samia sema chochote kuhusu Bunge kuoneshwa LIVE

Rais Mama Samia sema chochote kuhusu Bunge kuoneshwa LIVE

Twilumba

Platinum Member
Joined
Dec 5, 2010
Posts
13,468
Reaction score
16,168
Mama najua unapitapita kwenye mitandao ya kijamii direct au indirect.

Kwa siku hizi 18 ulizokaa kwenye hicho kiti kwa kweli umeleta nuru kwenye sura za watanzania walio wengi ukiacha wale Kenge walio kwenye msafara wa Mamba.

Pamoja na kauli nzuri za matumaini mpya nadhani Mama hujatamka chochote kuhusu Bunge letu kuoneshwa LIVE kama hapo awali ikiwa ni kwa lengo la wananchi kufuatilia mijadala mbalimbali inayoendeshwa na muhimili huo muhimu.

Nikuombe Mama hebu tamka waziwazi kuwa sasa Bunge lioneshwe LIVE katika session zake kama ilivyokuwa awali. Jambo hilo litakuwa kimekata kiu kavu na sugu waliyonayo watanzania walio wengi.

Najua wapo baadhi ya uliowaamini hasa wale uliowarithi kutoka utawala uliopita ambao kwa hakika bado wanashindwa kwenda na tune zako na hivyo kuonesha kukumwamisha kwa makusudi, mfano ni Dr. Abbas ambaye amenukuliwa na vyombo vya habari kuwa eti umesema vyombo ulivyoamuru vifunguliwe ni online TV peke yake.

Hii ni dharau kwa Mamlaka na kutaka kukugombanisha na wananchi wako, Mama mkanye aache mara moja. Afanye vile umemweleza bila kuanza kuleta ujuaji mwingine na urasimu usio na msingi.

Kila mtu amesikia LIVE umesema vyombo vya habari vifunguliwe lkn vifuate sheria, kanuni na taratibu, Dkt. Abbas anaanza ku-itemize kwamba ni Online TV pekee ndo ume?ungumzia, jamani ametoa wapi ujasiri wa kuiamulia mamlaka yako?

Mkanye mapema huyu Abbas ili utakaporuhusu kuonesha Bunge LIVE asitokee mwingine aseme Bunge lioneshwe specifically session fulani.

Kazi iendelee!!!
 
Japo litakosa ladha kwa kukosa wawakilishi wenye weledi mkubwa wa mambo ila watuletee tu tutafuatilia hivyo hivyo
 
Kwa sasa hata halina maana labda awarudishe wapinzani kule
 
Suala la Bunge kuonyeshwa live siyo mapenzi,hisani,kudra wala takwa la Rais.Suala la Bunge kuonyeshwa live ni haki yetu kikatiba.Haki huwa haiombwi kama unavyofanya bwana mleta uzi bali haki huchukuliwa kwa nguvu.Hatuna haja wala wajibu wa kumuomba Rais kuwa bunge liwe live bali tuna wajibu wa kuchukua haki hiyo kwa nguvu.Rais atake asitake suala la bunge kuwa live ni haki yetu wala siyo mapenzi yake.Umeelewa mleta mada?
 
Suala la Bunge kuonyeshwa live siyo mapenzi,hisani,kudra wala takwa la Rais.Suala la Bunge kuonyeshwa live ni haki yetu kikatiba.Haki huwa haiombwi kama unavyofanya bwana mleta uzi bali haki huchukuliwa kwa nguvu.Hatuna haja wala wajibu wa kumuomba Rais kuwa bunge liwe live bali tuna wajibu wa kuchukua haki hiyo kwa nguvu.Rais atake asitake suala la bunge kuwa live ni haki yetu wala siyo mapenzi yake.Umeelewa mleta mada?
Nimeelewa ndugu mchangiaji!!
 
Japo litakosa ladha kwa kukosa wawakilishi wenye weledi mkubwa wa mambo ila watuletee tu tutafuatilia hivyo hivyo
Ni kweli bunge halina ladha wala mvuto hata chembe. Labda kwa wanaopenda kusikia vishindo kwenye madawati na ndiooooo!!!
 
Kwa kitendo cha Mama, namfananisha na marikia wa Sheba cha kuruhusu vyombo vya habari vilivyofungiwa kufunguliwa kwani Marikia wa Sheba na yeye katika enzi zake kulitokea shida ya wanaume kuoa wake wangapi na sifa zipi lakini marikia alipoingia madarakani akapeta na kusema tuolewe tu bila mashariti hili taifa langu tuwe wengi. Mi nadhani hili kwa Mama liende sambamba na kufungulia bunge mubashara na lilushwe na TV zote za Tanzania kwa kadri inavyohitajika.

Hili bunge kwa sasa litakuwa zuri kwani wabunge wote ndani ya bunge ni CCM yaani asilimia 90 na kenda ni CCM hivyo ni wakati mzuri kwao kujinasbu kwani inasemekana wengine walikuwa hawachaguliki isipokuwa walibebwa na mfumo kwani watanzania walimkubali Magufuli na Mama Samia walipokuwa wanawaomba wananchi wa wape hao. Hivyo kuliachilia bunge live tutaweza kuwasikia kama walibebwa au walikuwa na uwezo. Pia kwa wabunge wenyewe watakuwa na sehemu ya kujinasbu kwa wapiga kura wao.

Hata hivyo zile sababu ambazo zilitolewa na Nape na wenzake wakati ule ikiwemo matumizi ya lugha za matusi na kudhalilishana na mambo mengine kama hayo, wale watu sasa hawapo ndani ya mjengo na waliopo ni viti maalumu hawatambuliki hata na ndugu zao hivyo si tishio tena kwani inasemekana huko nyuma walikuwa wanapelekwa chuo au kozi za kujifunza kutukana mitusi kabla ya kuja bungeni na walikuwa awadedi na chama wakitumia mitusi zaidi kuliko hoja.
 
Kwa kitendo cha Mama, namfananisha na marikia wa Sheba cha kuruhusu vyombo vya habari vilivyofungiwa kufunguliwa kwani Marikia wa Sheba na yeye katika enzi zake kulitokea shida ya wanaume kuoa wake wangapi na sifa zipi lakini marikia alipoingia madarakani akapeta na kusema tuolewe tu bila mashariti hili taifa langu tuwe wengi. Mi nadhani hili kwa Mama liende sambamba na kufungulia bunge mubashara na lilushwe na TV zote za Tanzania kwa kadri inavyohitajika...
Wawakilishi au Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM?
 
Back
Top Bottom