Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 5,897
- 10,358
Vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vitaanza kurushwa live. Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma, Katibu wa Bunge. Ndg. Nenelwa Mwihambi.
Nenelwa amesema baada ya maboresho ya Studio ya Bunge na Kamati ya Uongozi ya Bunge kuridhia vikao vya Bunge vitaanza kurushwa live kuanzia kesho tarehe 05 Aprili 2022 wakati Mkutano wa Saba wa Bunge mahsusi kwa ajili ya kupitisha Bajeti ya Serikali utakapoanza Bungeni Jijini Dodoma.
Januari mwaka 2016, waziri wa habari wa wakati huo, Nape Nnauye alitoa tangazo bungeni la kusitisha matangazo ya Bunge ya moja kwa moja akitoa sababu ya kupanda kwa gharama kwenye shirika la utangazi la Taifa(TBC) zilizofikia bilioni 4.2 kwa mwaka.
Nape alisema TBC ilikuwa ikigharamia matangazo ya Bunge kwa kutumia vyanzo vyake vya mapato kama matangazo madogo ya kibiashara. TBC katika kupunguza gharama na kubana matumizi ikaona busara kurusha baadhi ya matangazo live na mengine kurekodiwa kisha kurushwa kwenye kipindi maalum usiku ambayo ingewapa pia fursa watanzania walio wengi kwani mchana huwa wana kazi za kiofisi au ujenzi wa Taifa.
PIA, Soma=>TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)