Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,175
- 143,964
- Thread starter
-
- #701
Ngosha na mimi ngoja nikupe shukrani kwa uzi maridadi kabisa! Umeona kwa usahihi kabisa, ngosha mwenzio nchi imemshinda!
Hii sentensi hapa nchi nimeielewa sana:Wewe sidhani hata umeelewa nilichokiandika.
Pole.
Lakini Mkuu Nyani, bado unasimamia huu uzi uliotoa? naona siku hizi kama kuna kacheo unakanyemelea vile... au nimekusoma vibaya?Shukran jazilan.
Lakini Mkuu Nyani, bado unasimamia huu uzi uliotoa? naona siku hizi kama kuna kacheo unakanyemelea vile... au nimekusoma vibaya?
OOOH BEN UKO WAPI JAMANI?Nilishaonya tangu Mwaka jana.Misingi ya Urais sio kusakata rhumba au push ups majukwaani
Ahsante kwa maelezo yako. Nimekuelewa vizuri.Ndiyo.
Bado naamini kabisa kuwa rais Magufuli yashamshinda.
Naamini kwamba rais Magufuli hana sifa za uongozi wa ki-urais.
Lakini, licha ya mapungufu yake ya kiuongozi bado kuna baadhi ya mambo ambayo nakubaliana naye.
Kwa hiyo msimamo wangu bado uko palepale.
Atakapokosea mahali, basi nitamkosoa kama ambavyo nimeshafanya mara nyingi tu humu [na ushahidi upo].
Nitakapoona kuna mahali kapatia, nitamuunga mkono na kumpa pongezi.
Vivyo hivyo kwa CHADEMA na vyama vingine vya upinzani.
Vikichemsha, nitavichana bila huruma.
Vikipatia, sitokuwa mchoyo wa pongezi.
Jana tu nimetoka kumpongeza Mh. Freeman Mbowe kwa maneno yake ya hekima na busara kwenye taarifa aliyoitoa kuhusu maendeleo ya Tundu Lisu.
Sasa kilicho kigumu hapo kueleweka ni nini?
Uchaguzi unafanyika October 2020. Kuanzia April 2020 mpk July 2020 wabunge watakuwa na jukumu la kuipitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021. Naamini hiyo ndio bajeti ya uchaguzi 2020/2021. Correct me if I'm wrong- Budget ijayo ni budget ya uchaguzi ( 2018/2019 ) hakuna cha maana kinachofanyika
Basi amebakiza budget moja tu kwa kuwa mpaka sasa hakuna lolote alilofanya la kuboresha maisha ya watuUchaguzi unafanyika October 2020. Kuanzia April 2020 mpk July 2020 wabunge watakuwa na jukumu la kuipitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021. Naamini hiyo ndio bajeti ya uchaguzi 2020/2021. Correct me if I'm wrong
For those running away from the truth aka LIARS "You belong to your father, the devil, and you want to carry out your father's desire. He was a murderer from the beginning, not holding to the truth, for there is no truth in him. When he lies, he speaks his native language, for he is a liar and the father of lies."Hivi ni mimi tu au na wengine mpo mnaoona kama vile mambo yashamshinda huyu Magufuli?
Kuna hali fulani hivi naiona ambapo jamaa ni kama anaamka tu kila asubuhi na kutoa maamuzi ya kukurupuka kurupuka.
Yaani yeye ni amri tu....fanya hivi....fukuza huyu....twende kule...nk.
Yapo baadhi ambayo ni mazuri ambapo mtu unaona kabisa hapa nia ni nzuri lakini kuna mengine yenye ukakasi sana hadi kunifanya nianze kuhoji hekima na busara za huyo bwana!
---
Mimi ni mmoja wa watu wanaoamini kuwa rais wetu huyu, mheshimiwa mtukufu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli si kiongozi mzuri hata kidogo, hususan katika ngazi ya urais.
Hilo nimekuwa nikilisema kwa muda mrefu sasa. Nakumbuka hata ile siku alipoteuliwa kuipeperusha bendera ya CCM nilisema hivyo humu humu JF.
Kwa kiasi fulani namkubali kwenye usimamizi lakini si kwenye uongozi. Hana kabisa haiba ya kiuongozi. Pia hana sifa za kuweza kuwa kiongozi mzuri.
Ni mtu mwenye jazba. Ana jeuri. Mwenye kuongea bila kufikiria athari za maneno yake[nyakati zingine]. Wengine wanasema eti kuwa hashauriki. Kwa ufupi ni mengi sana yanasemwa juu yake kiasi kwamba mengine ni vigumu kwa watu wa mbali kama sisi kujua kama ni ya kweli au la. Hivyo kwa sisi wa mbali tunaenda na yale tuyaonayo na tuyasikiayo toka kwake yeye mwenyewe.
Sasa kwa jinsi vile mambo yanavyoenda sasa hivi kuna kila dalili huenda nchi imeshamshinda kuiongoza. Hivyo ndivyo niuonavyo mwelekeo.
Hata ndani ya chama chake ukiangalia vizuri utaona nyuso nyingi tu za manung'uniko toka kwa wakereketwa. Wengi wao siku hizi wanashindwa hata kumtetea. Wapo kimyaaaa utadhani wagonjwa. CCM hawana furaha kabisa.
Naamini asipojiangalia na kujifanyia tathmini basi hiyo kazi itamshinda kabla hata hajafikia nusu ya muhula wa hii miaka mitano.
Niliwahi kuandika kuhusu 'a police state'. Jikumbushe....
A Police State
hakusema asalam aleikum bana alisema asaraam areikuumNimecha leo baada ya kumaliza hutuba anasema asalameku wakati iyo nisaram ya kuanzia
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo mmepanga kumuua?kwasabababu Mungu atamchukua nakumpangia majukumu mengine atakayomudu huko kuzimu kabla ya bajet 2018/2019
Ukiitoa Bajeti ya 17/18 - Current BudgetBasi amebakiza budget moja tu kwa kuwa mpaka sasa hakuna lolote alilofanya la kuboresha maisha ya watu