Rais Magufuli, Waziri Ndalichako na wengine, acheni kuchezea elimu yetu

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
Uchumi wetu upo katika kipindi kigumu kuliko muda wowote .

Bado hata najiuliza ni kwanini Tanzania ipo katika kipindi kigumu wakati nchi zote duniani hali ya maisha ni raha msitarehe?....

Kwanini ni Tanzania tu makosa ni ya nani?.....

Umejaribu kila namna umeshindwa sasa umeamua kuwatoa kafara wanafunzi na wafanyakazi wa serikali ili kukwepa aibu ya anguko la kishindo la uchumi..

Umeamua kuja na mpango Wa kuondoa wafanyakazi kwa kisingizio cha vigezo vyao vya kujiunga chuo kikuu huko nyuma.

Umeamua kuwabana wanafunzi wasio na cheti cha form 6 wasiipate degree sijui unatumia sheria ya wapi ?ya nchi gani? Iliyopitishwa na bunge gani?

Kama sio mwendokasi na kukurupuka kutaka kuwaumiza watoto wa masikini waliosoma shule za kata kwa kutumia koloboi ambao hawajawai hata kuuona umeme Wa Tanesco ni nini?..

Sasa hivi wamiliki wa vyuo vidogo vya certificate & diploma itabidi wafunge vyuo na kufukuza wafanyakazi Wa vyuo hivyo.

Kiukweli umeingia chaka na ni kichekesho kwa msomi Mwenye PhD ya sayansi ya kemia kuwanyima fulsa ya vijana wetu kusoma .

Umebana mikopo umeweza sasa hata wanaofanya juhudi kusoma unawazuia?

Kwanini usianze kuhakiki hao mawaziri wako wenye vyeti vya kuunga unga wengine wapo kwenye wizara nyeti za ulinzi....

Hakika laana utakayoipata kwa kuwaonea wanafunzi na wafanyakazi na kuchezea elimu ya nchi kwa ujumla itakuandama mpaka mwisho.

Wana Jamvi,
Tukiwa bado tunaangaika na ajira na uhakiki ukishika kasi, huyu Prof tayari dunia inaonekana kumwacha kwa kasi kwa kuleta fikra za zamani zinazokinzana na sheria. Kila kukicha hakosi sababu naona anashindana na Paulo wa Dar kuteka media.

Ukiangalia kwa undani maresitter walikuwa wanaonewa sana, hufelishwa makusudi ili waendelee kula fedha zao, haiwezekani mtu alifeli alafu akirudia unampa mitiani mawili, kumbuka ana majonzi ya kufeli na anatumia gharama zake alafu unampa mtiani mgumu. Huyu anaposhinda hatumii fedha za serikali lakini bado unamkomesha.

Serikali ilianzisha shule za kata voda fasta bila walimu wala maabara hawa wanapomaliza shule na hawajafaulu wanatupwa dunia nyingine. Wewe Prof Joy ebu nenda shule ya sekondari mbweni uone madudu mliofanya alafu uje hapa utueleze vijana waliomaliza pale waende wapi?

Kumbuka walifaulu la saba leo hii mumewamyima walimu, maabara na madarasa hili muwaite Vilaza. Mmeanzisha VETA je wakifanya vizuri Waishie hapo? Jaribu kutafakari hata mkulu aliunga hata yule Wazir wa hela wa zamani mwanamke aliunga. Wapo wengi waliounga na wanafanya vizuri.

Wana JF sina personal vendetta/Chuki against Waziri wa Elimu profesa ndalichako.
Ila Kutokana na utata wa maagizo yake (directives) katika mambo ya elimu. INANIPA WASIWASI kuhusu UWEZO wake ambao unamwelekeo wa KUIUA sekta ya Elimu nchini kabisa na kuirudisha nyuma miaka ya1960 wakati sasa tuko katika karne ya 21 ya teknolojia kielimu.Kiasi kwamba mambo mengi yamebadilika na KURAHISISHWA!

Pia atuwekee tusome link ya Publications zake na Research zake zilizoko online ama google ili TUHAKIKI na TUTOE maoni yetu baada ya KUZISOMA!

Swali linalonisumbua.
Je huyu Waziri ni Profesa kweli ama ? Tungemwomba pia tuwekee hapa katika JF, Baadhi ya Kazi/Publications ni (NGAPI?)

Research work/ papers zake akianzia kutupatia THESIS zake za MASTERS na
PhD na ilikuwa JUU ya nini/FIELD hadi u PROFESA na atupe Publications zake hapa mtandaoni. Ili NASI TUHAKIKI KIMATAIFA maana ulimwengu ni Global village
Hii ITATUSAIDIA kama haku PLAGIARIZE/ KUKOPI RESEARCH work na PUBLICATIONS za watu wengine?Maana mtu MSOMI huwa na tabia ya usomi. Ya huyu nanipa mashaka!
 
Na alaaniwe daima, huyu MTU amebadilidha hata marks za kujiunga chuo kikuu?
Wakati nchi za wenzetu wanaanza kuhamasisha watu kuchukua masters, sisi bado tunakimbizana na degree
Hii nchi hatakuja kuendelea hata kidogo kwa viongozi wenye mawazo ya kimaskini kama haya
 
Wazalendo Wa nchi hii wote ni wakati wetu Wa kupaza sauti kukataa upuuzi unafanyika na hii siri-kali katili!!
 
Uchumi wetu upo katika kipindi kigumu kuliko muda wowote .

Bado hata najiuliza ni kwanini Tanzania ipo katika kipindi kigumu wakati nchi zote duniani hali ya maisha ni raha msitarehe?....

Kwanini ni Tanzania tu makosa ni ya nani?.....

Umejaribu kila namna umeshindwa sasa umeamua kuwatoa kafara wanafunzi na wafanyakazi wa serikali ili kukwepa aibu ya anguko la kishindo la uchumi..

Umeamua kuja na mpango Wa kuondoa wafanyakazi kwa kisingizio cha vigezo vyao vya kujiunga chuo kikuu huko nyuma.

Umeamua kuwabana wanafunzi wasio na cheti cha form 6 wasiipate degree sijui unatumia sheria ya wapi ?ya nchi gani? Iliyopitishwa na bunge gani?

Kama sio mwendokasi na kukurupuka kutaka kuwaumiza watoto wa masikini waliosoma shule za kata kwa kutumia koloboi ambao hawajawai hata kuuona umeme Wa Tanesco ni nini?..

Sasa hivi wamiliki wa vyuo vidogo vya certificate & diploma itabidi wafunge vyuo na kufukuza wafanyakazi Wa vyuo hivyo.

Kiukweli umeingia chaka na ni kichekesho kwa msomi Mwenye PhD ya sayansi ya kemia kuwanyima fulsa ya vijana wetu kusoma .

Umebana mikopo umeweza sasa hata wanaofanya juhudi kusoma unawazimuia?

Kwanini usianze kuhakiki hao mawaziri wako wenye vyeti vya kuunga unga wengine wapo kwenye wizara nyeti za ulinzi....

Hakika laana utakayoipata kwa kuwaonea wanafunzi na wafanyakazi na kuchezea elimu ya nchi kwa ujumla itakuandama mpaka mwisho.
mnajitekenya na kucheka wenyewe. mbona hili la equivalent qualification kuingia chuo kikuu lipo kila mahali duniani. wala hata hizo clip za ndalichako hakuna mahali kasema diploma hawaingii chuo kikuu. kitu kiko clear kilichopigwa marufuku ni ile kitu foundation course kutumika kama criteria ya admission. inaelekea vijana wa ukawa wako bussy na misinformation.
 
Sasa jamaa alisema afukui makaburi kwanini anataka kuwafukuza Kazi watu waliopata degree mwaka 1980?
 
wa2 wana uwezo mdogo sn wa kuelewa! mbona hyo video hajazungumzia equivalent? tupen nyingine bas km ipo! km nyie mnaopotosha hv na mnataka mkasome degree kazi ipo!
 
Hatujui mpaka sasa nini tunataka kama taifa...baadala yake tunalipa ramli tu...
 
Mifumo nayo sasa twaona wanazdisha mbwembwe mpk wanafunz wanashindwa kusoma wakisubr kubadlika kwa mfumo kila siku
 
Hasira nyingi mpaka naweza pga mtu.... Hii falme naidediketia matusi yote ya wapiga debe na makonda
 
Back
Top Bottom