Matumizi stahiki ni kama haya kuwatambua mijiziMitandao ni swala geni hapa kwetu na nchi nyingine, laiti kama kungekuwa na elimu kama ilivyo elimu ya hesabu na sayansi mashuleni, watu wangejuwa matimizi stahiki ya mitandao.
Yaani una post maneno ya Zitto kama umeandika wewe. Sio fair. Weka source vinginevyo ni uhuni wa kiuandishi.Kwenye ripoti yake, CAG hajasema popote kuwa TZS 1.5trn zimeibiwa. Alichosema leo Ikulu ndio msimamo wake uliopo kwenye Taarifa yake ukurasa wa 34. Fedha hizo HAZIONEKANI kwenye matumizi ya Serikali ya mwaka 2016/17.
Ndio maana tunahoji zipo wapi. Tunataka Ukaguzi Maalumu ili kuhakiki majibu ya Serikali na kujua hela zetu zipo wapi. Hilo tu, hakuna lingine.
Vitisho vya hatua za kisheria ni tambo tu za watawala, hazina maana yeyote. Kumsimamisha CAG Ikulu na kumhoji mbele ya Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ni kumtisha CAG, ni kinyume na misingi ya Katiba yetu. Ripoti ya CAG ikishakuwa mbele ya Bunge sio Ripoti ya Executive tena. Ni mali ya Bunge. Kama Rais ana majibu aende akayaseme Bungeni mbele ya PAC.
Rais sio wa kumchekea chekea anapovunja misingi ya nchi yetu. Ni lazima ADHIBITIWE na Taasisi za Kikatiba ikiwemo Bunge. Rais leo amekosea. CAG naye amekosea kwenda Ikulu.
Watanzania sikilizeni, mimi nimekuwa Mwenyekiti wa PAC/POAC miaka 8, ninajua kusoma, kuchambua na kutafsiri Taarifa ya CAG. TZS 1.5trn hazina maelezo, hazipo Benki Kuu na Maelezo ya Naibu Waziri Fedha leo ni kujikosha tu.
Nikiwa Mwenyekiti wa PAC, Mwaka 2013 Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli alikutwa na Hoja ya ukaguzi ya TZS 252 bilioni ya ujenzi wa barabara hewa ambayo mpaka sasa haijajibiwa na utaikuta kwenye Hoja za CAG za mwaka 2016/17. Hivyo ni Kawaida yake kutoheshimu sheria za Fedha na kutojibu Hoja za Ukaguzi.
Kama Serikali ina uhakika kabisa hii hoja ya TZS 1.5trn haipo inipeleke mahakamani hata leo. Nitawashinda hata Jaji akiwa mmoja wa majaji wapya walioapishwa leo.
Mimi siogopi. Nitasema UKWELI daima fitina kwangu mwiko.
Zipo wapi TZS 1.5trn?
Yaani una post maneno ya Zitto kama umeandika wewe. Sio fair. Weka source vinginevyo ni uhuni wa kiuandishi.
Rais Magufuli leo akiwaapisha Majaji 10 aliowateua pamoja na Mawakili amesema kuwa Watanzania tunaamini kila kinachoandikwa kwenye mitandao ya kijamii. Hii inatokana na kutoku-control mitandao hiyo wamiliki wako huko wao interest yao ni kutengeneza biashara wala hawajali consequences zitakazotokea
> Rais Magufuli ameongeza kuwa hadhani kama ukienda kwenye nchi kama China utakuta wana 'Google' na 'WhatsApp' kama hizi za kwetu huku
> Rais Magufuli: Kila Mtu anapojifikiria anapost chochote kwenye mitandao ya kijamii
Rais ameelezea tabia ya kuamini mijadala ya mitandaoni kama ugonjwa ambao hafahamu umetoka wapi. Ameeleza kuwa siku moja alikua akisoma mtandaoni kuhusu serikali kuiba Trilioni 1.5 ikabidi ampigie CAG kuuliza kuhusu wizi huo
======
Ikumbukwe kuwa mnamo Septemba 28 mwaka 2016 Rais Magufulia alinukuliwa akisema kuwa ''Anatamani Malaika washuke wazime mitandao ya kijamii, irudi baada ya mwaka 1 ikute hatua kubwa za kimaendeleo tulizopiga''
Huyu ni mwizi kuliko wezi wote waliopo magereza ooops mafisadi wote waliopo ccmHakuna uongo kuhusu udikteta wake, ukwapuzi wa nyumba za Serikali, ukwapuzi wa bilioni 16 za wahanga wa tetemeko, ununuzi wa kivuko uozo, kuchota trillions hazina bila idhini ya Bunge, ubaguzi wake wa kutisha etc.
Matumizi stahiki ni kama haya kuwatambua mijizi
Kwani wanaposema social media wewe unaelewa nini?
Trump ana tweet kila siku yahusuyo serikali yake sasa cha ajabu nini Waafrica kufanya haya
Trillion zinawatoa ufahamu kutetea majizi
Mitandao si swala geni linakwenda sambasamba ulimwenguni kote acheni kuwabeza WaTz
Mitandao ni swala geni hapa kwetu na nchi nyingine, laiti kama kungekuwa na elimu kama ilivyo elimu ya hesabu na sayansi mashuleni, watu wangejuwa matimizi stahiki ya mitandao.
Kwa nini umetolea mfano wa marehemu na sio mfano wa hili lililopo mbele yetuMimi sikatai umuhinu wa mitandao ya kijamii, lakini je ni wangapi wanajuwa kupanga na kupanguwa kilicho kwenye hiyo mitandao? hata huyo Trump mwenyewe, mara ngapi anadika vya uwongo na baadhi ya watu wanaamini. Kuna kijana mmarekani alianika mwili wa mjapani aliye jingonga bila kujali madhara ya hizo picha kwa wanadugu wa marehemu, Je kwako wewe huo ndio matumizi stahiki ya mitandao. Hata kama watu wanataka kuibuwa wizi Je aliye andika kama kadanganya na nchi ikavurugika kwenu hili ni jambo jema?
Huyu ni mwizi kuliko wezi wote waliopo magereza ooops mafisadi wote waliopo ccm