Mlianza kwa kuzinanga serikali zilizopita hasa ya awamu ya nne. Mnapoulizwa kitu gani "so special" mlichofanya ambacho huko nyuma hakikufanywa, mnatoa povu. Tuwakumbushe tu, tangia mwanzoni mwa 1900, nchi hii ilianza kuwa na reli, mlipokuja mjini mlipita katika mabarabara ya lami toka huko mlikokuwa.
Kila kijiji mlikuta kina shule ya msingi, kila kata mlikuta kuna shule ya sekondari. Madaraja yote makubwa yalishajengwa. Yote hayo yalifanyika kwa combination ya resources za ndani na nje kwa njia ya ushirikiano. Self-seclusion itatufikisha wapi katika Dunia ya leo jamani.
Now mnageukia "mabeberu". Jamani "mabeberu" si washindani wetu kwenye maendeleo wala si size yetu. Tunawaita mabeberu ila wao wakituita manyani tunapayuka Dunia nzima. Maana maneno huuma nayo. Let's promote harmony, peace and unity.