Rais Magufuli: Wanaoikosoa serikali kwa staha hatuwachukii

kwenye katiba yapo tatizo hata katiba hamijui

Katiba inatamka wazi kuwa kila mtu anastahili heshima na kutovunjiwa utu wake sasa ukiongea na mtu maneno yasiyo na heshima unakuwa umevunja katiba na kumvunjia hshima utu wake

ina maana hata ukichora katuni ya kumdhalilisha umevunja katiba ya nchi
Sidhani kama kuna utawala ambao umeongoza kuvunja katiba kama utawala wa awaku ya tano.

Siku utawala wa awamu ya 5, utakapotamka na kuwa tayari kuongoza nchi hii kwa mujibu wa katiba, hata hii ya sasa, ambayo ina kasoro nyingi, malalamiko mengi dhidi ya Serikali, na chuki dhidi dhidi ya serikali na viongozi, vitapungua.
 
Hayo maneno kwenye KATIBA hakuna!! Kama hawezi arudi chato mbona hatujamuomba kuwa Rais

Hapa yenyewe tunamsaidia kupata utajiri.
That is foolish! Unataka katiba ya nchi ikufundishe kutumia mdomo wako. Ikufundishe kuacha matusi? Hiyo siyo Katiba, labda diary yako.
 
Rais wa JMT ameyasema hayo wakati akizungza na watanzania kupitia hadhara iliyokusanyika jana viwanja vya mnazimmoja.

Rais Magufuli amesisitiza kuwa kwa sasa hapa Tanzania kuna vyombo vingi vya habari ambavyo vimepewa leseni za kufanyia kazi na hii ni ishara kuwa kuna uhuru mkubwa wa habari hapa Tanzania.

Lakini jambo la kusikitisha ni kuona kuna upotoshaji mkubwa unaofaywa na baadhi ya vyombo vya habari. Mfano ni kuandika habari za uzushi juu ya vifo vya viongozi na kupotosha kuwa sasa kuna maambukizi makubwa ya Corona tofauti na hali halisi.

Hivyo ni wazi kuwa kama serikali inakubali kukosolewa ni jambo jema kutumia lugha nzuri kufikikisha ujumbe kwa viongozi wa serikali ili wajirekebishe.
Hali halisi kwa takwimu zipi? Zile zile za mapapai?
 
kwenye katiba yapo tatizo hata katiba hamijui

Katiba inatamka wazi kuwa kila mtu anastahili heshima na kutovunjiwa utu wake sasa ukiongea na mtu maneno yasiyo na heshima unakuwa umevunja katiba na kumvunjia hshima utu wake

ina maana hata ukichora katuni ya kumdhalilisha umevunja katiba ya nchi

Kasome tena katiba hakuna kukosoa kwa Staha!!

Tunakosoa kutoka na tukio husika!!! Hakuna sehemu watu wanatukana ndio maana Gazeti Uhuru wanaandika uongo lakni hakuna anaesema lakini wengine wakiandika ukweli wanafungiwa .
 
Lakini jambo la kusikitisha ni kuona kuna upotoshaji mkubwa unaofaywa na baadhi ya vyombo vya habari. Mfano ni kuandika habari za uzushi juu ya vifo vya viongozi na kupotosha kuwa sasa kuna maambukizi makubwa ya Corona tofauti na hali halisi.

Hali halisi ikoje; Maambukizi na makubwa, madogo, ya wastani, machache au hayapo ?

Kama hatuambiwi maambukizi yakoje na Taasisi husika unategemea itakuwaje, tatizo ni kwamba either kwa makusudi au bahati mbaya sources za habari ambazo ndio zingetegemea haziaminiki...., Kazi yao imekuwa ni kubisha na kufanya propaganda
 
Akishasemaga hivyo kinachofuata hapo lazima mtu apopolewe.Rejea kauli yake ya nyuma baada ya hapo TL yakamkuta ya kumkuta!
 
Kwa hiyo nikisema " Ndugu Rais kutokana na changamoto zilizojitokeza wakati wa uchaguzi mkuu huu wa October 2021, (hamna haja ya kuzitaja zinajulikana kwa kila mtanzania mpiga kura) tunaomba kuanza mara moja kwa mchakato wa kuundwa kwa TUME HURU YA UCHAGUZI pamoja na mabadiliko yake ya KATIBA ambayo yataruhusu matokeo ya kura za URAIS yaweze kuhojiwa mahakamani kama kutakuwa na umuhimu huo kama zilivyo katiba za nchi karibia zote za Africa Mashariki (Majirani zetu)

Kama nikimwambia hivi nafikiri nitakuwa nimemshauri kwa staha.
Hapo ni sawa na kwenda kumuomba kiustarabu, mwizi aliyekuibia mali zako kwa kutumia silaha, akurudishie .Je,atarudisha??!!
 
Hapo ni sawa na kwenda kumuomba kiustarabu mwizi aliyekuibia mali zako kutumia silaha akurudishie .Je,atarudisha??!!
Nimeuliza hivi, kama ni sawa Je nitumie njia gani kuufikisha ujumbe huu wa Katiba na Tume Huru kwa watanzania walio wengi ili hoja yangu ibakie kuwa ya staha ?
 
Nimeuliza hivi, kama ni sawa Je nitumie njia gani kuufikisha ujumbe huu wa Katiba na Tume Huru kwa watanzania walio wengi ili hoja yangu ibakie kuwa ya staha ?
Kudai katiba na tume huru ya uchaguzi ni kutangaza vita.Kwa hiyo kwa vyovyote utakavyodai itaonekana huna lugha ya staha!
 
Je, Katiba yetu tuliyonayo inaruhusu kutokuheshimu mamlaka iliyoko madarakani au kutokuwaheshimu wengine? Kukosoa Serikali bila staha kwa maana nyingine ni kudharau mamlaka iliyoko madarakani. Katiba yetu inaruhusu hilo?

Tatizo lenu mnadhani kukosoa ni ombi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom