VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Wananchi wa kawaida hawaamini kinachoendelea. Wanashuhudia tu fukuzafukuza ya watendaji Serikalini pamoja na mikwara iliyokwenda Shule. Wanamshuhudia Rais,Makamu, Waziri Mkuu,Mawaziri na watendaji wengine wakiendelea kutema mikwara kwa wa chini yao pamoja na kumwaga ahadi kana kwamba uchaguzi bado.
Wananchi wa kawaida wanamshuhudia Rais na serikali yake wakiizungumzia na kuiimarisha Dar es Salaam kana kwamba Tanzania ni Dar pekee. Wananchi wa kawaida wanamshuhudia Rais akitumbua majipu halafu hakuna impact ya moja kwa moja katika maisha yao.
Bei za vyakula zimepanda. Bei za vifaa vya ujenzi zinazidi kupaa. Bei ya hata maji safi inapaa kila uchao. Makazi yao duni. Matibabu yao duni. Lishe hafifu. Hawakuelewi. Hawaioni thamani ya kutumbua majipu. Wananchi wa kawaida,walio wengi mijini na vijijini wanahitaji maisha yao yabadikike hata kidogo. Kuwe na direct impact ya kutumbua majipu kwenye maisha ya watanzania!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam