Rais Magufuli, wananchi hawakuelewi

Rais Magufuli, wananchi hawakuelewi

Wananchi wa kawaida hawaamini kinachoendelea. Wanashuhudia tu fukuzafukuza ya watendaji Serikalini pamoja na mikwara iliyokwenda Shule. Wanamshuhudia Rais,Makamu, Waziri Mkuu,Mawaziri na watendaji wengine wakiendelea kutema mikwara kwa wa chini yao pamoja na kumwaga ahadi kana kwamba uchaguzi bado.

Wananchi wa kawaida wanamshuhudia Rais na serikali yake wakiizungumzia na kuiimarisha Dar es Salaam kana kwamba Tanzania ni Dar pekee. Wananchi wa kawaida wanamshuhudia Rais akitumbua majipu halafu hakuna impact ya moja kwa moja katika maisha yao.

Bei za vyakula zimepanda. Bei za vifaa vya ujenzi zinazidi kupaa. Bei ya hata maji safi inapaa kila uchao. Makazi yao duni. Matibabu yao duni. Lishe hafifu. Hawakuelewi. Hawaioni thamani ya kutumbua majipu. Wananchi wa kawaida,walio wengi mijini na vijijini wanahitaji maisha yao yabadikike hata kidogo. Kuwe na direct impact ya kutumbua majipu kwenye maisha ya watanzania!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Jipe muda; usitake JPM afanye miujiza hata hii nchi ilichukua miongo kadhaa kuoza mpaka hapa ilivyo sasa; mambo mazuri hayataki haraka; vuta subira!
 
Kuna wilya inaitwa LOLIONDO haina barabara ya lami hata Petrol station hakuna
Kuna kipindi nilifika huko,ilinichukua dakika 30 kukipata Kibanda(siyo duka) ili nitoe fedha kwa M-Pesa,na hapo nilikua mjini Loliondo..
 
Kama anapenda sifa, mtamzoea tu hivyo hivyo na maisha yanasogea na maendeleo yatapatikana tu hamna shida!
 
Sishiriki malumbano yasiyo na tija. Kurekebisha uchumi sio suala la siku miamoja. Pia kutumbua majipu sio kushusha bei za vyakula, ni kuweka mfumo bora wa uwajibilkaji ambao utaleta matunda mema hapo baadaye. Kusema wananchi hawakuelewi wakati tunamwombea usiku na mchana ni uongo wenye nia ovu. Narudia kwa dhati, kuna ukanda ambao hawaungi mkono chochote kinachofanywa na serikali kwa sababu walitarajia "chama chao" kingeshinda uchaguzi mkuu. Hao hawawezi kamwe kumwelewa rais
Sio chama chao kushika hatamu, wanasema eti kwenye teuzi za JPM kanda hiyo hawamo, sasa kilichobaki ni kuponda chochote JPM anachofanya. Wakumbe majipu yaliyokwisha tumbuliwa mengi yametoka ukanda huo, sasa nani kichaa arudishe fisi kwenye butcher
 
Mkuu tindo,moja ya vtu vinavyowalewesha viongozi wetu ni unafiki wa wafuasi wao kuwasifia kwa kila kitu wanachokifanya hata kama hakina positive impact katika maisha ya watanzania,na hilo linawafanya waone kuwa wanafanya sawa.
Kwa mtu mwenye akil ya kawaida tu ya kuzaliwa nayo,angetegemea kuona siku 100 za uongozi wa JPM na utumbuaji majipu angalau unaleta nafuu ya maisha kwa mwananchi wa kawaida.
Kama siku 100 bado ni mapema kwa serkali ya awamu ya 5 kubadilisha maisha ya watanzania walau kwa unafuu fulani,basi bado ni mapema mno pia kumpa sifa hizo anazopata ambazo zinaweza mpelekea yeye na serikali yake kulewa na kuendelea hivyo hivyo .
Nina mashaka na uelewa wako, kweli siku 100 zianze kuleta unafuu wa maisha kwa watanzania milioni 50??? Kwanza huenda naongea na motto, ngoja niache
 
We kweli haupo sawa, maskini wa kawaida wengi hawana magari. Watajuaje kuhusu mafuta kuwa yamepungua tsh. Hamsini ,kwaiyo kwa MTU wa rufiji huko ambae ananunua sukar elfu mbili na Mia tatu,kiberiti Mia na hamsini ,nauli kutoka makumbusho had I Bunju watu wa daladala wamejipandishia kiholela bila kutangazwa na Sumatra,basi bora kuwa mafuta yangekuwa yamepanda bei, NAULI kutoka Mia sita ya kikwete hadi sasa Mia nane NAULI, acha bidhaa zingine ndo hazishikiki kabisa, ,,

umeshindwa kunielewa kwa sababu una akili za kinyumbu.
 
Haya ndio matunda ya kufurahia ngoma na buku tano wakati wa kampeni.
 
ki ukweli maisha ni magumu sana kwa wananchi wa kawaida kwa makazi hasa wa mabondeni nao hawana amani hawajui kesho yao wanavunjiwa au la wafanyakazi nao hawajui kesho zao mana kila siku viongozi wa ngazi zote za serikali wanadhindana kufukuza na kusimamisha kazi wenzao wenye maisha mazuri ni waandishi tu wa habari mana wao kila kukicha wanaitwa kurekodi na wafanyakazi wa serikali
 
Hata mzee wa vijesenti watu hawakumuelewa mwanzoni lkn baadae walikuja kumuelewa.
 
Akili za vijana wa ufipa ni janga

Rais Magufuli wananchi tunamuelewa sana ambao hamumuelewi ni nyie nyumbu

Nashauri rudini Serengeti maana huku uraini hamupawez
bora Nyumbu kuliko fisi anayesubirimkono wa binadamu ukatike ile aule wakati binadamu yupo hai
 
Wananchi wa kawaida hawaamini kinachoendelea. Wanashuhudia tu fukuzafukuza ya watendaji Serikalini pamoja na mikwara iliyokwenda Shule. Wanamshuhudia Rais,Makamu, Waziri Mkuu,Mawaziri na watendaji wengine wakiendelea kutema mikwara kwa wa chini yao pamoja na kumwaga ahadi kana kwamba uchaguzi bado.

Wananchi wa kawaida wanamshuhudia Rais na serikali yake wakiizungumzia na kuiimarisha Dar es Salaam kana kwamba Tanzania ni Dar pekee. Wananchi wa kawaida wanamshuhudia Rais akitumbua majipu halafu hakuna impact ya moja kwa moja katika maisha yao.

Bei za vyakula zimepanda. Bei za vifaa vya ujenzi zinazidi kupaa. Bei ya hata maji safi inapaa kila uchao. Makazi yao duni. Matibabu yao duni. Lishe hafifu. Hawakuelewi. Hawaioni thamani ya kutumbua majipu. Wananchi wa kawaida,walio wengi mijini na vijijini wanahitaji maisha yao yabadikike hata kidogo. Kuwe na direct impact ya kutumbua majipu kwenye maisha ya watanzania!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Umefanya utafiti gani ndani mda huu mfupi na kugundua hakuna ipmact yeyote? Je uozo wa miaka 30 unaweza ukaisha ndani ya siku 100?
 
Bidhaa zitashukaje bei wakati serikali aishushi gharama za kodi kodi Iko juu bidhaa nayo lazima iwe juu

uwezi ukamkemea mfanya biashara eti apunguze bei wakati kodi unampandishia Kila Siku.
mheshimiwa hili nalo jipu litumbue
wananchi tunaumia mchele bei juu mafuta ya kura bei juu mafuta ya taa bei juu kiberiti bei juu nauli za magari bei juu vifaa vya ujenzi ndo hatari tupu nguo za madukani ndo sigusi kabisa lakini wenzetu munakula na munaishi tu vizuri haya bana Bora salama.
 
Mbona sisi wengine tunamwelewa vizuri sana na tunataka akanyagie hapo hapo. Madudu serikalini yapo mengi na lazima yashughulikiwe. Na ndio yanayofanya Serikali ishindwe kushughulikia mahitaji ya wananchi. Watanzania bana, kama taifa la kenge, juani tunalalamika joto, kivulini tunalia baridi.
 
Pale watu wanapodhani uchumi unakuwa fixed in days, poor tanzania...nchi tajiri iliyo na umaskini mkubwa wa fikra.
Obama aliingia madarakani 2008 USA ikiwa hoi kiuchumi, imemchukua miaka yote kufix alichoharibu Bush...
Kama mnadhani bei madukani zitashuka kwa siku-mwezi, mnajidanganya. Itachukua mda, sacrifices, ikiwa ni pamoja na kuweka misingi imara kuimarisha uchumi.

Lakini kwa fikra za kina mzee tupa tupa wanaotafuta attention mitandaoni, usitegemee nchi kukua kiuchumi. I'm just saying..
 
Unampigia mbuzi gitaa. Mpaka amalize hasira ndipo atakumbuka kuna wananchi wanasubiri utekelezaji wa ilani ya CCM.
 
Nimewahi kuweka uzi kama huu ,na juzi pia nimeweka ila watu wananishambulia sana,kiiwelu fukuzafujuza haina majibu kwa matatizo yetu
 
Back
Top Bottom