Rais Magufuli, wananchi hawakuelewi

Rais Magufuli, wananchi hawakuelewi

Vuta nikuvute wengi wetu tunajua Magufuli hana sera za kutengeneza vyanzo vya mapato vitakavyoleta nafuu kwa wananchi na kufanya mzunguko wa pesa uwafike walengwa yule ni mchoyo wa asali jana kato mpya kasema watu wanaagiza very inferior sugar jamani ha ha
 
Ndugu tunaanzia kwanza Dar then kwingineko watafuata hapa Dar ndo kumtima kwa ufisadi na wakwepa kodi tumuunge mkono huyu jamaa pia na safu yake
 
Siku atakayokumbuka Wapinznai nao ni watanzania na wanatakiwa kuijenga nchi atakuwa ameshapotea sana.Wanaomuharibia ni watendaji wake mwenyewe.

Ma DC wako busy kutifuana na wabunge waupinzani wkaitafuta kick ya kutoka.Kazi ipo.

Mbunge wa upinzani, mchungaji na msafisha fisadi anatafuta "kick" ya kisiasa kwa kutaka kupambana na Mkuu wa Wilaya
 
Wananchi wa kawaida hawaamini kinachoendelea. Wanashuhudia tu fukuzafukuza ya watendaji Serikalini pamoja na mikwara iliyokwenda Shule. Wanamshuhudia Rais,Makamu, Waziri Mkuu,Mawaziri na watendaji wengine wakiendelea kutema mikwara kwa wa chini yao pamoja na kumwaga ahadi kana kwamba uchaguzi bado.

Wananchi wa kawaida wanamshuhudia Rais na serikali yake wakiizungumzia na kuiimarisha Dar es Salaam kana kwamba Tanzania ni Dar pekee. Wananchi wa kawaida wanamshuhudia Rais akitumbua majipu halafu hakuna impact ya moja kwa moja katika maisha yao.

Bei za vyakula zimepanda. Bei za vifaa vya ujenzi zinazidi kupaa. Bei ya hata maji safi inapaa kila uchao. Makazi yao duni. Matibabu yao duni. Lishe hafifu. Hawakuelewi. Hawaioni thamani ya kutumbua majipu. Wananchi wa kawaida,walio wengi mijini na vijijini wanahitaji maisha yao yabadikike hata kidogo. Kuwe na direct impact ya kutumbua majipu kwenye maisha ya watanzania!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Kibaraka uliyebaki CCM...Si umfuate mzee tu Chifu?

Acha unafiki
 
Kuna viumbe humu wanapenda sifa tu, hawataki kutumia akili wala macho yao. someni hoja kwanza kabla hujakurupuka kujibu. ikikuumiza bora unyamaze kuliko kujitoa akili.
 
Wananchi wa kawaida hawaamini kinachoendelea. Wanashuhudia tu fukuzafukuza ya watendaji Serikalini pamoja na mikwara iliyokwenda Shule. Wanamshuhudia Rais,Makamu, Waziri Mkuu,Mawaziri na watendaji wengine wakiendelea kutema mikwara kwa wa chini yao pamoja na kumwaga ahadi kana kwamba uchaguzi bado.

Wananchi wa kawaida wanamshuhudia Rais na serikali yake wakiizungumzia na kuiimarisha Dar es Salaam kana kwamba Tanzania ni Dar pekee. Wananchi wa kawaida wanamshuhudia Rais akitumbua majipu halafu hakuna impact ya moja kwa moja katika maisha yao.

Bei za vyakula zimepanda. Bei za vifaa vya ujenzi zinazidi kupaa. Bei ya hata maji safi inapaa kila uchao. Makazi yao duni. Matibabu yao duni. Lishe hafifu. Hawakuelewi. Hawaioni thamani ya kutumbua majipu. Wananchi wa kawaida,walio wengi mijini na vijijini wanahitaji maisha yao yabadikike hata kidogo. Kuwe na direct impact ya kutumbua majipu kwenye maisha ya watanzania!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Labda wewe na wenzio mliojifungia huko Lumumba ndio pekee msioona kinachoendelea.

Kwa taarifa yako wananchi huku mitaani na vijijini tunajua kinachoendelea ndani ya miezi hii mitatu kuliko ambavyo tulijua kilichokuwa kikiendelea katika serikali ya Kikwete kwa miaka yake 10.

Tulichokuwa tukikiona wakati wa utawala wa awamu ya nne ilikuwa ni maktaim ya maisha na kiuchumi kwa wanyonge na goose-step kwa wakubwa na walionacho.

Kuhusu majipu kutumbuliwa Dar tu, ni kweli lakini si unajua Dar ndiyo makao makuu ya kila kitu? Wakubwa wote wako huko, mafisadi wako huko, bandari ziko huko, TRA iko huko, hazina iko huko, benki kuu iko huko n.k na ndio maana hata wewe uko huko hukukaa Songea. Acheni Magufuli achape kazi.
 
Mafuta naweka kumbukumbu sawa, yameshuka kiasi kwamba hata hili punguzo la hapa Dar la Petrol 1842 bado haikustahili. Ilitakiwa iwe chini Tsh 1600, huko soko la dunia bei iko chini sana.
Hapa Canada petrol tunanunua $60cents ni kama 900/=.. Huko Bongo vipi?!
 
Ninyi ni vibaraka tu,,,,, ulitegemea Magu afanyaje kwa mfano ili useme anafanya vema?

Nilitegemea Magufuli wangalau achukulie hatua makampuni ya umeme ambayo hata maazimio yake yalishapitishwa na bunge. Gharama za kampuni za simu zimeshapigiwa kelele sana mpaka bungeni ila zilikosa utekelezaji wenye dhamira njema. Je hata hili atajifanya mgeni? Kumbuka yeye sio mgeni kwenye serekali, alikuwepo serekalini karibia miaka 20 tena akiwa waziri. Kwa hiyo sioni ni kwa jinsi gani ajigeuze mpya kabisa wakati nchi inaendeshwa kwa sera. Labda kama unataka kusema huko ccm hamfuati sera bali kila kiongozi akiingia madarakani anaanza upya. Kuna mambo mengi ambayo tayari yameshapangwa yalikosa utashi tu wa uongozi, nilitaraji angeshayatolea maamuzi, badala yake kwa kuwa anaongoza wajinga wengi hivyo anafanya kazi ya kufukuza zaidi ili kufurahisha kundi hilo la wajinga lakini tija halisi kwenye maisha yetu hatuoni.
 
Ficha ujinga wako wewe......So akimfukuza Mkurugenzi wa Hospitali basi Chakula kishuke bei,tumeeni akili mnataka direct impact gani nyinyi.....Faida ya haya majibu yanayo tumbuliwa utaiona baadae!

Hujawahi tumbuliwa jipu hospitalini maumivu huwa yanaisha mara baada ya kumaliza kutumbua? Eti direct impact au unaropoka tuu wakurugenzu wafukuzwe wewe unataka siku hio hio sukari ishuke bei? ni ujinga gani unaongea wewe usie na shukrani

Juhudi zote hizo hamzioni hata kama uchumi hujasoma lakini hata akili ya kufikilia tuu huna eti direct impact......

Hoja zako zinaongozwa na jazba, kwa kifupi ni hoja za nguvu. Huyu rais ni mgeni tu kwenye hicho cheo, lakini sio mgeni kabisa kwenye serekali, alikuwa waziri zaidi ya miaka 15, hivyo alipaswa kuingia moja kwa moja kwenye utekelezaji kwani tayari yeye ni kama msafiri anayerudi kwenye njia aliyopita hivyo anajua pabaya na pazuri. Huu umeme tunapigwa bao sana na yeye alikuwepo mpaka bungeni wakati bunge linapitisha azimio kwamba makampuni ya umeme wanatuuzia kwa bei mbaya. Je hili nalo anahitaji miaka 100 ili bei ishuke? Mbona anawafahamu hao wahuni wanaotulalia. Makampuni ya simu yanafahamika kwa kutucharge gharama za juu zisizo halisi na wala hawalipi kodi stahiki, mbona basi hata gharama hatuoni zikishuka?

Najua kinachokutesa wewe, uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana hivyo ukiona mtu anafukuzwa kazi kwako wewe inakuwa burudani bila kujua faida yake ni nini kwako. Hiki chama kilichoko madarakani sio kipya kama alivyo yeye hivyo nilitarajia afuate sera za chama ili tuone unafuu wa maisha, lakini kama anaanza upya kama vile ni mtu wa chama tofauti basi kuna walakini sana kwenye chama na rais aliyeko madarakani kuhusu suala la uchumi. Wewe baki ukisifia tu bila kupima mwelekeo wa nchi kwani sasa hivi kusifia kwenye ni fashion.
 
Wakati ufike siasa tuziweke pembeni tuweke uhalisia. unaposema bei zinazidi kupaa kila kukicha tuwekee na mifano. mie nina mfano wa bei ya Mafuta, alipoingia Magufuli madarakani nilikua nanunua petroli lita 1 kwa sh 2194 kwa sasa nanunua petroli lita moja kwa sh 1920


Uwe unajifunza kukumbuka, mafuta kunakipindi yalishuka hadi sumatra waliambiwa na washushe nauli ya kwenye mabasi yote, lakini sumatra walijitetea kuwa ni kweli bei ya mafuta imeshuka ktk soko la dunia lakini sasa hatujui bei hiyo itaendelea kuwa chini kwa kipindi gani! Tunaweza kushusha bei ya nauli leo baada ya muda mfupi itapanda tenda kwahiyo ni vema tukavuta subila. Na kweli baada ya muda kidogo ukaanza mgogoro wa SAUDI ALABIA NA YEMEN mafuta yalipanda tena, na kwasasa kule kumetulia na mafita yameshuka tena, sasa nakuaachia kazi ya nyumbani, je umashawahi kuhoji kuwa kwanini swala la kushusha nauli halizungumziwi tena wakati mafuta yameshuka kwa mala nyingine tena? TUMIA MTANDAO HUOHUO KUHOJI NA WAHUSIKA WATAKUSIKIA.
 
Ficha upumbavu wako, kwani huo utumbuaji umeleta impact gani kwenye maisha ya wananchi zaidi ya kuuza sura tu kwenye media!!! Badala ya kujibu hoja unamshambulia mtoa mada wakati anaongelea hali halisi ya maisha ya wananchi. Hayo maigizo hayawasaidii wananchi. Wajipange kimikakati, sio kufanya mambo kwa kutaka sifa ili waonekane wanachapa kazi lakini hakuna matokeo chanya.
Unawezaje kuwa na maisha bora bila kuwaondowa wapigaji...bure kabisa!
 
Mbunge wa upinzani, mchungaji na msafisha fisadi anatafuta "kick" ya kisiasa kwa kutaka kupambana na Mkuu wa Wilaya

Tatizo lenu hamtaki kukubali kama mmeshindwa kihalali hapo Iringa.Wakuu wa wilaya wanatakiwa kufanya kazi na wabunge na siyo kuwapiga majungu sababu tu siyo CCM hailipi
 
Back
Top Bottom