Rais Magufuli, wananchi hawakuelewi

Rais Magufuli, wananchi hawakuelewi

Akili za vijana wa ufipa ni janga

Rais Magufuli wananchi tunamuelewa sana ambao hamumuelewi ni nyie nyumbu

Nashauri rudini Serengeti maana huku uraini hamupawez
 
Mimi ni mmojawapo simuelwi na simkubali kabisa, ukijumlishan na teuzi kama za watu kama Muhongo ,Znzibar case nk
 
Namshangaa kukataza sukari za nje wakati ya ndan inapanda bei kila siku. Wakati za nje zikiingia ya ndani ilikuwa chini baada ya kukataza naona imepanda zaidi ya elf kumi sasa tunazidi kuumia
MKUU HII ni impact ya kuzuia kitu flani bila mipango yakinifu....
sijaskia mipango thabiti dhidi ya sukari iliyowekwa.......
sukari ya ndani eti bei kubwa kuliko ya nje...haya maajabu
 
Inaudhi jamaa hataki kumsifia Magufuli wakati sasa hivi ni fashion kumsifia. Ukiachia jazba uliyoionyesha na kutumia utetezi dhaifu wa ubaguzi wa kikanda ulipaswa kuonyesha kama kweli, bei za vyakula, vifaa vya ujenzi na gharama nyingine za maisha zimeshuka kulingana na huo utumbuaji majipu? Hii tabia ya kusifia kuadhibu bila kuona impact kwenye maisha halisi ya mwananchi ni utoto uliopita kipimo. Tunachokiona ni vitisho kwa watumishi wa umma na ahadi kibao kama tulivyozoea.
mkuu usitegee points kutoka kwa vijana wa CCM zaidi ya mihemko na kashfa na vitisho....
jamaa katoa hoja mtu anapanic....wanataka wote tusifie etii
 
mimi kinachonipa stress...
hamna mtu asiyefahamu ubovu wa mikataba ya nchi,madini,gas,bandari(tics)
na rasilimali zinginezo....
na rais anayajua hayo yote na sisi wananchi tunamuamini JPM ila hadi leo yupo kimya hajagusia
hata kugusia tu2 ubadilishwaji wa mikataba.....
ili ilete tija kwa taifa na kutowafaidisha wachache...ifaidishe taifa zima kwa ujumla.....
hiki kitu kinanipa mawazo sanaa.....
please RAIS WETU...JPM cheki hili kwa jicho la pili....nchi ni rasilimali sio kodo pekeeee
hapo ndo tutaendelea...lasivyo kwa kutegemea kodi pekee nchi haitopiga atua
fukuza fukuza itaendelea na nchi itabaki pale na mifumo ya hovyo hovyo.................
 
Mimi ni mmojawapo simuelwi na simkubali kabisa, ukijumlishan na teuzi kama za watu kama Muhongo ,Znzibar case nk
mkuu inakatisha tamaa sanaaa
hamna jipya zaid ya wafanyakaz wa umma kuaminishwa mashetani
na akina chawene wakihusishwa na skendo mpyampya za ufisadi
na muhongo kutetea waharifu..bila kuchukuliwa hatuaa
 
Wananchi wa kawaida hawaamini kinachoendelea. Wanashuhudia tu fukuzafukuza ya watendaji Serikalini pamoja na mikwara iliyokwenda Shule. Wanamshuhudia Rais,Makamu, Waziri Mkuu,Mawaziri na watendaji wengine wakiendelea kutema mikwara kwa wa chini yao pamoja na kumwaga ahadi kana kwamba uchaguzi bado.

Wananchi wa kawaida wanamshuhudia Rais na serikali yake wakiizungumzia na kuiimarisha Dar es Salaam kana kwamba Tanzania ni Dar pekee. Wananchi wa kawaida wanamshuhudia Rais akitumbua majipu halafu hakuna impact ya moja kwa moja katika maisha yao.

Bei za vyakula zimepanda. Bei za vifaa vya ujenzi zinazidi kupaa. Bei ya hata maji safi inapaa kila uchao. Makazi yao duni. Matibabu yao duni. Lishe hafifu. Hawakuelewi. Hawaioni thamani ya kutumbua majipu. Wananchi wa kawaida,walio wengi mijini na vijijini wanahitaji maisha yao yabadikike hata kidogo. Kuwe na direct impact ya kutumbua majipu kwenye maisha ya watanzania!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Siku atakayokumbuka Wapinznai nao ni watanzania na wanatakiwa kuijenga nchi atakuwa ameshapotea sana.Wanaomuharibia ni watendaji wake mwenyewe.

Ma DC wako busy kutifuana na wabunge waupinzani wkaitafuta kick ya kutoka.Kazi ipo.
 
Kwa uandishi huu,fikra hizi,mbinu hizi za siasa za fisi kuvizia mkono uanguke ni dalili za kukosa dira,ila hili bomu la fikra potofu litaitafuna chadema kama siasa za mtandao zilivyoitesa ccm...hakika mkigundua project ya EL ndani ya chadema ninavyowajuwa bavicha mtakula nyama DJ...nakusikitikia nawewe umekuwa msukule!...naweka akiba ya maneno.

Mkuu ntoa mada ni CCM yuko Lumumba unamhusisha vipi na CHADEMA au Bavicha?
 
Wananchi wanataka matokeo ya haraka? namshauri Magu afanye jambo moja tu rahisi kabisa ili kupunguza foleni ya magari katika jiji la Dar (hii italeta matokeo ya haraka na yatakayoonekana wazi): ONDOA vituo vyote vya Daladala pembezoni mwa barabara; ili mabasi ya daladala yanapotaka kupakia au kushusha abiria yatoke kabisa katika barabara kuu. Sambamba na hili, aondoe pia biashara zote pembezoni mwa barabara kuu.
 
Wakati ufike siasa tuziweke pembeni tuweke uhalisia. unaposema bei zinazidi kupaa kila kukicha tuwekee na mifano. mie nina mfano wa bei ya Mafuta, alipoingia Magufuli madarakani nilikua nanunua petroli lita 1 kwa sh 2194 kwa sasa nanunua petroli lita moja kwa sh 1920
manufaa binafsi yakisiasa yanaitikisa nchi yetu, ni haki kwa watanzania kuhoji hatima yao ila kwa mwendo wa raisi unaleta matumain makubwa sio kidogo so maon yangu tuache siasa mda huu ila tuongee au mda mnaotumia kupiga kelele hizo tutumie kupiga kelele nn kifanyike ila kujinasua kwenye umasikin au sio ndugu yangu
 
Inaudhi jamaa hataki kumsifia Magufuli wakati sasa hivi ni fashion kumsifia. Ukiachia jazba uliyoionyesha na kutumia utetezi dhaifu wa ubaguzi wa kikanda ulipaswa kuonyesha kama kweli, bei za vyakula, vifaa vya ujenzi na gharama nyingine za maisha zimeshuka kulingana na huo utumbuaji majipu? Hii tabia ya kusifia kuadhibu bila kuona impact kwenye maisha halisi ya mwananchi ni utoto uliopita kipimo. Tunachokiona ni vitisho kwa watumishi wa umma na ahadi kibao kama tulivyozoea.
Ninyi ni vibaraka tu,,,,, ulitegemea Magu afanyaje kwa mfano ili useme anafanya vema?
 
Ficha upumbavu wako, kwani huo utumbuaji umeleta impact gani kwenye maisha ya wananchi zaidi ya kuuza sura tu kwenye media!!! Badala ya kujibu hoja unamshambulia mtoa mada wakati anaongelea hali halisi ya maisha ya wananchi. Hayo maigizo hayawasaidii wananchi. Wajipange kimikakati, sio kufanya mambo kwa kutaka sifa ili waonekane wanachapa kazi lakini hakuna matokeo chanya.
Wew ndie mpumbavu namba moja kwamba mpaka sasa hivi bado unazumgusha....mabadiliko ni hayo anayofanua magufuli mzee acha kuwa mtumwa wa kisiasa
 
Wakati ufike siasa tuziweke pembeni tuweke uhalisia. unaposema bei zinazidi kupaa kila kukicha tuwekee na mifano. mie nina mfano wa bei ya Mafuta, alipoingia Magufuli madarakani nilikua nanunua petroli lita 1 kwa sh 2194 kwa sasa nanunua petroli lita moja kwa sh 1920

We kweli haupo sawa, maskini wa kawaida wengi hawana magari. Watajuaje kuhusu mafuta kuwa yamepungua tsh. Hamsini ,kwaiyo kwa MTU wa rufiji huko ambae ananunua sukar elfu mbili na Mia tatu,kiberiti Mia na hamsini ,nauli kutoka makumbusho had I Bunju watu wa daladala wamejipandishia kiholela bila kutangazwa na Sumatra,basi bora kuwa mafuta yangekuwa yamepanda bei, NAULI kutoka Mia sita ya kikwete hadi sasa Mia nane NAULI, acha bidhaa zingine ndo hazishikiki kabisa, ,,
 
Ficha upumbavu wako, kwani huo utumbuaji umeleta impact gani kwenye maisha ya wananchi zaidi ya kuuza sura tu kwenye media!!! Badala ya kujibu hoja unamshambulia mtoa mada wakati anaongelea hali halisi ya maisha ya wananchi. Hayo maigizo hayawasaidii wananchi. Wajipange kimikakati, sio kufanya mambo kwa kutaka sifa ili waonekane wanachapa kazi lakini hakuna matokeo chanya.
ujinga ni kuamini kuwa ndani ya siku 100 baada ya uchaguzi kila kitu kitakuwa poa...ujinga ni kuamini kuwa ndani ya muda huo impact ya kusimamia mapato na matumizi itapunguza mfumuko wa bei na ujinga mbaya zaidi ni kuamini kuwa porojo zenu hizi zinaweza kumzuia jamaa aache kuwatumbua!!!!!tunajua kuwa nyie ni mamluki wa wahujumu uchumi ambao wanahaha kila kona na kwa mbinu mbalimbali kuionyesha/kuiaminisha jamii kuwa anachofanya JPM si sahihi.hii sio short term project....tuonane 2020.
 
Anachofanya raisi ni kuwavutia wananchi wengi zaidi Dar kitu ambacho kitazidisha idadi ya watu ktk mji wenye msongamano tayari. Mimi naona alipaswa kuboresha maisha katika miji midogo inayochipukia ili kupunguza rural-urban migration. .....sasa kama kila kitu kizuri kipo Dar, kwanini nibaki Magu.? "Tanzania ni Dar es Salaam"....well after all nasubiri labda bajeti yake itatupa unafuu sisi walalahoi
 
Wananchi wa kawaida hawaamini kinachoendelea. Wanashuhudia tu fukuzafukuza ya watendaji Serikalini pamoja na mikwara iliyokwenda Shule. Wanamshuhudia Rais,Makamu, Waziri Mkuu,Mawaziri na watendaji wengine wakiendelea kutema mikwara kwa wa chini yao pamoja na kumwaga ahadi kana kwamba uchaguzi bado.

Wananchi wa kawaida wanamshuhudia Rais na serikali yake wakiizungumzia na kuiimarisha Dar es Salaam kana kwamba Tanzania ni Dar pekee. Wananchi wa kawaida wanamshuhudia Rais akitumbua majipu halafu hakuna impact ya moja kwa moja katika maisha yao.

Bei za vyakula zimepanda. Bei za vifaa vya ujenzi zinazidi kupaa. Bei ya hata maji safi inapaa kila uchao. Makazi yao duni. Matibabu yao duni. Lishe hafifu. Hawakuelewi. Hawaioni thamani ya kutumbua majipu. Wananchi wa kawaida,walio wengi mijini na vijijini wanahitaji maisha yao yabadikike hata kidogo. Kuwe na direct impact ya kutumbua majipu kwenye maisha ya watanzania!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Mkuu uko wapi na una shughuli gani waje wakutumbue ili ukome kuuliza maswali?
 
Mkuu unajua tena Mgema akisifiwa tembo ulitia maji.
 
Inaudhi jamaa hataki kumsifia Magufuli wakati sasa hivi ni fashion kumsifia. Ukiachia jazba uliyoionyesha na kutumia utetezi dhaifu wa ubaguzi wa kikanda ulipaswa kuonyesha kama kweli, bei za vyakula, vifaa vya ujenzi na gharama nyingine za maisha zimeshuka kulingana na huo utumbuaji majipu? Hii tabia ya kusifia kuadhibu bila kuona impact kwenye maisha halisi ya mwananchi ni utoto uliopita kipimo. Tunachokiona ni vitisho kwa watumishi wa umma na ahadi kibao kama tulivyozoea.
Ficha ujinga wako wewe......So akimfukuza Mkurugenzi wa Hospitali basi Chakula kishuke bei,tumeeni akili mnataka direct impact gani nyinyi.....Faida ya haya majibu yanayo tumbuliwa utaiona baadae!

Hujawahi tumbuliwa jipu hospitalini maumivu huwa yanaisha mara baada ya kumaliza kutumbua? Eti direct impact au unaropoka tuu wakurugenzu wafukuzwe wewe unataka siku hio hio sukari ishuke bei? ni ujinga gani unaongea wewe usie na shukrani

Juhudi zote hizo hamzioni hata kama uchumi hujasoma lakini hata akili ya kufikilia tuu huna eti direct impact......
 
Sijui nani ampelekee salam, amwambie sisi hatumwelewi kabisaa, maisha magumu kodi kubwaa, yaani shida tupu, hayo majipu huku kwetu matombo hayana msaada kwetu, atoe hizo ela benk watu tufanye biashara
Mkuu tatizo wanaona kila analofanya liko sawa hawataki akoselewe,huo ni udhaifu mkubwa sana.
 
Back
Top Bottom