jsenyinah
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 249
- 339
RAIS AWASILI BUKOBA: Rais John Magufuli amewasili mjini Bukoba kuwatembelea wananchi waliopata maafa ya tetemeko la ardhi mwaka jana.
-------
Hatimaye Rais John Magufuli amewasili mjini Bukoba na kushiriki misa ya kufungua mwaka mpya 2017 katika Kanisa la Kuu Katoliki mjini Bukoba.
Katika misa hiyo iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo la Bukoba, Mhashamu Desderius Rwoma, Dk Magufuli amewataka viongozi wa dini wamvumilie kwa kuwa fedha zitaendelea kupotea hata kanisani.
Amesema zamani zilikuwepo fedha za hovyo hovyo na sasa anachotaka ni kila mtu aendelee kula anachostahili.
Amesema uchumi wa nchi unaendelea kuimarika na Serikali imedhibiti mfumuko wa bei.
Akiwa Kagera, Rais Magufuli atapata fursa ya kuwasalimia wananchi waliopata maafa ya tetemeko la ardhi Septemba mwaka jana.