Rais Magufuli, Unawaza nini?

Rais Magufuli, Unawaza nini?

Bandikolako inaonesha mna uchu wa kuingia Ikulu..sio lazima! Mnaweza msiingia milele (kama CCM ikiendelea kufanya vizuri) na bado nchi ikawa ya kidemokrasia....in short, demokrasia sio kubadili vyama. Vichwa ngumu sana nyie aisee
 
Mada yako ina mawazo fikirishi lakini imeharibiwa na hisia zako za chuki dhidi ya Serikali iliyoko madarakani na kuamini kuwa matatizo ya Tanzania yatatuliwa na mataifa ya nje. Ebu jikumbushe kilichotokea Iraq na Libya.

Narejea hoja yako kuthibitisha hilo, kwamba unadai ati:
Vyama mamluki vya upinzani vilivyopandikizwa na System vijifanye eti ni vyama vya upinzani na vinashiriki Uchaguzi, mataifa makubwa yanajua ukweli wote juu ya hiyo ghiliba

Alichokisema ni ukweli, hahitaji kutoa mawazo yake kwa kuficha ukweli eti kisa ww utaona ana chuki na serikali. Iraq na Libya ziliharibiwa na viongozi wao kuendelea kung'ang'ania madaraka kama wafanyavyo ccm hapa nyumbani, hata baada kukosa uungwaji mkono wa wananchi walio wengi. Iwapo viongozi hao wangetii demokrasia na kukubali kukaa pembeni kwa amani, wala haya yanayoendelea yasingetokea.
 
TZ wapinzani kuongoza nchi labda mwaka 5020 watakapokuja wapinzani wenye akili siyo hawa wa sasa wanyama wa serengeti.
Wao wanadhani kubadili vyama kila baada ya miaka 10 ndo demokrasia..wanasiasa mna kazi kubwa ya kuelimisha wanajamii wanaotembelea zile barabara zinazoekekea Ufipa.
 
Ukisoma habari za mitandaoni, unaweza ukadhani 90% ya wabongo ni wapinzani...sasa ngoja muda wa kudemonstrate upinzani wao kwa vitendo...

Acha CCM watawale tu
Ndio ushangae kwa nini Jiwe anakuwa ! Anatumia vyombo vya dola kuwakandamiza wapinzani ambao ni 'wachache na dhaifu'! Anaharibu mpaka uchaguzi dhidi ya upinzani ambao ni ' dhaifu'! Ccm bila polisi ni wepesi kama unyoya
 
Bandikolako inaonesha mna uchu wa kuingia Ikulu..sio lazima! Mnaweza msiingia milele (kama CCM ikiendelea kufanya vizuri) na bado nchi ikawa ya kidemokrasia....in short, demokrasia sio kubadili vyama. Vichwa ngumu sana nyie aisee

Hakuna anayesema demokrasia ni lazima kubadili vyama, hatuna tatizo hata ccm ikitawala milele, bali watawale kwa kutii box la kura. Lakini kitendo cha kubaka box la kura kimacho macho hilo halikubaliki. Tunataka kuona ushindani kama wa Simba na Yanga, mshindi anapatikana kwa uhalali ndio maana hatuoni mikwaruzano isiyo ya lazima, japo wakati fulani fulani kuna mapungufu ya hapa na pale ambayo yanavumilika.
 
Na yeyeto asiyependa shaurika ni lzm aanguke
Kwani kuna mtu amelazimisha ushauri hapa? Na siyo rais tu hata wewe na mimi hatulazimiki kufuata ushauri wa Mtu yeyote! Hakuna sheria inayolazimisha kupokea ushauri, na kama ipo hiyo inakuwa amri siyo ushauri tena.
n
 
Najaribu kupata picha ya ametoka madarakani na hao anao waonyesha chuki kubwa kabisa bila kujificha wakawa madarakani atakuwa na wakati gani?
Kuwapata watu kama Mandela sio jambo rahisi ndani ya karne moja hivyo kutegemea visasi ni jambo lisilo kwepeka. Anajua hilo?
Mwinyi, Mkapa na hata JK hawakuwa wanaendesha nchi kwa chuki binafsi hivyo hata kama warithi wao wangekuwa chama tofauti bado heshima yao ingekuwepo.
Najaribu kumfananisha na kiongozi afrika mashariki na kati aliyetoka madarakani aliyekuwa na tabia hizi simpati zaidi ya Amin pekee.

Yeyeto aliyeelimika uitazazama kesho yake
 
Eti " mataifa makubwa yanajua hili...." Watu wanajua kujiwaza...
 
Watu waliowahi kuwekewa sumu au kujiwekea sumu vibaya wakakosa kufa huwa na mawazo,maamuzi na maneno ya hovyohovyo sn....chunguzeni!!!
 
O
Tatizo mkila mkashiba mnaona Kama CCM ndo mungu wa Tanzania, subiri, kuna mambo yatatokea hadi mtasambaana, muda kidogo mno umebakia
CCM itapata pigo kuuuuubwa sana pigo moja tu pigo takatifu pigo lililonyooka kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
 
Hilary Clinton alimzidi Donald Trump kwa idadi ya kura, lakini Donald Trumo akawa rais.

Sasa hiyo ni demokrasia?

Ndiyo. Ni demokrasia.

Demokrasia zipo za aina tofauti.

Aina ya demokrasia ya Marekani kwenye ngazi ya serikali ya shirikisho ni demokrasia ya uwakilishi [representative democracy].

Hakuna demokrasia ya moja kwa moja [direct democracy] kwenye uchaguzi wa Rais wa Marekani.

Lakini pia, kwenye nchi nyingi tu za kidemokrasia, kwenye chaguzi zao hususan za viongozi wakuu wa serikali, huwa hakuna demokrasia ya moja kwa moja.

Mfano, Uingereza huwa hawapigi kura kumchagua waziri mkuu wao. India vivyo hivyo. Israel pia.

Hata Afrika Kusini huwa hawampigii kura rais wao moja kwa moja.

Wamarekani, licha ya kwamba wanampigia kura rais wao moja kwa moja, ushindi wake huamuliwa ki majimbo na idadi ya wawakilishi ataopata kutoka majimboni ambao baadaye wawakilishi hao ndo watapiga kura zao za kuuthibitisha ushindi wake.

Hiyo nayo ni demokrasia.
 
Ndiyo. Ni demokrasia.

Demokrasia zipo za aina tofauti.

Aina ya demokrasia ya Marekani kwenye kiwango cha serikali ya shirikisho ni demokrasia ya uwakilishi [representative democracy].

Hakuna demokrasia ya moja kwa moja [direct democracy] kwenye uchaguzi wa Rais wa Marekani.

Lakini pia, kwenye nchi nyingi tu za kidemokrasia, kwenye chaguzi zao hususan za viongozi wakuu wa serikali, huwa hakuna demokrasia ya moja kwa moja.

Mfano, Uingereza huwa hawapigi kura kumchagua waziri mkuu wao. India vivyo hivyo. Israel pia.

Hata Afrika Kusini huwa hawampigii kura rais wao moja kwa moja.

Wamarekani, licha ya kwamba wanampigia kura rais wao moja kwa moja, ushindi wake huamuliwa ki majimbo na idadi ya wawakilishi ataopata kutoka majimboni ambao baadaye wawakilishi hao ndo watapiga kura zao za kuuthibitisha ushindi wake.

Hiyo nayo ni demokrasia.
Demokrasia ni nini?
 
Back
Top Bottom