Rais Magufuli, Unawaza nini?

My Son drink water

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
4,932
13,283
Uliwaita watendaji wa Kata Ikulu na kuwapa maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa, kwamba wakikishe Chama tawala kinapata favor zote za ushindi.

Hivi umeshawaza kuwa maisha hubadilika? Leo wewe ni Rais, kuna siku hutakuwa Rais na hawahawa wapinzani unaowachukia ndio watakuwa wanaongoza nchi huku ukishuhudia kwa macho yako.

Kwa nafasi yako ya ukuu wa nchi watendaji wa Kata hawakuwa na hadhi ya kuonana nawe Ikulu.
Uliamua kuvunja itifaki ili tu CCM ipate ushindi feki.

Vyama mamluki vya upinzani vilivyopandikizwa na System vijifanye eti ni vyama vya upinzani na vinashiriki Uchaguzi, mataifa makubwa yanajua ukweli wote juu ya hiyo ghiliba.

Kila siku unataka tukuombee kwa Mungu ila Mungu hana chuki na wapinzani Kama uliyonayo wewe.
Mungu anawapenda wana CCM wote na wapinzani wote,na ndo huyu huyu Mungu atakuja kuwawezesha waingie Ikulu na kuongoza Tanzania huku wote mkiona.

Kwa akili za kibinadamu haiwezekani, ila kwa Mungu inawezekana.
Hata makaburu wa South Africa hawakuwahi kufikiria kuwa ANC ya weusi itakuja kuchukua Dola huku wakishuhudia.
Tabia ya Mungu huwa ni kukaa na wanyonge na kuwainua juu kutoka mavumbuni.

Badilika mapema uiandae kesho yako siku ukistaafu uwe kimbilio la wote kwa ushauri wa hekima, na siyo watu wakusambae kwa kuacha alama mbaya.
 
Marekani wabunge Republicans kipindi cha impeachment ya Bill Clinton waliweka taratibu za kumu impeach rais ziwe rahisi zaidi. Kwa lengo la kumuondoa Clinton.

Wakawa wanasema maneno mengi sana. Wamerekodiwa.

Leo hii wapinzani wao Democrats wanataka kutumia taratibu zilezile zilizowekwa na Republicans wakati wa impeachment ya Clinton, kumu impeach Trump, Republicans wanalalamika.

Mkuki mtamu kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu.
 
?????
IMG-20191116-WA0003.jpeg
 
kumbe hata amerika kuna mambo ya ajabu

sasa mbona jafo aliposema chicharito ni sehemi ya uchaguzi watu wakapanick!!!
 
wakati tukiwa shule tuliwahi kufundishwa concept ya deformation kwenye somo la strength of materials. elastic material ukiivuta sana mpaka ukavuka elastic limit ina undergo deformation na ni katika level hii ya deformation hata ufanye je ile material haiwezi kurudi tena kwenye hali yake ya kawaida. mzee yupo kwenye deformation state, kumshauri ni time wasting.
 
mie natamani sana ningekuwa daktari wake
 
Uliwaita watendaji wa Kata Ikulu na kuwapa maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa, kwamba wakikishe Chama tawala kinapata favor zote za ushindi.

Hivi umeshawaza kuwa maisha hubadilika? Leo wewe ni Rais, kuna siku hutakuwa Rais na hawahawa wapinzani unaowachukia ndio watakuwa wanaongoza nchi huku ukishuhudia kwa macho yako.

Kwa nafasi yako ya ukuu wa nchi watendaji wa Kata hawakuwa na hadhi ya kuonana nawe Ikulu.
Uliamua kuvunja itifaki ili tu CCM ipate ushindi feki.

Vyama mamluki vya upinzani vilivyopandikizwa na System vijifanye eti ni vyama vya upinzani na vinashiriki Uchaguzi, mataifa makubwa yanajua ukweli wote juu ya hiyo ghiliba.

Kila siku unataka tukuombee kwa Mungu ila Mungu hana chuki na wapinzani Kama uliyonayo wewe.
Mungu anawapenda wana CCM wote na wapinzani wote,na ndo huyu huyu Mungu atakuja kuwawezesha waingie Ikulu na kuongoza Tanzania huku wote mkiona.

Kwa akili za kibinadamu haiwezekani, ila kwa Mungu inawezekana.
Hata makaburu wa South Africa hawakuwahi kufikiria kuwa ANC ya weusi itakuja kuchukua Dola huku wakishuhudia.
Tabia ya Mungu huwa ni kukaa na wanyonge na kuwainua juu kutoka mavumbuni.

Badilika mapema uiandae kesho yako siku ukistaafu uwe kimbilio la wote kwa ushauri wa hekima, na siyo watu wakusambae kwa kuacha alama mbaya.
If you dominate the person with violence they'll eventually fight back because they got nothing to lose
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom