Rais Magufuli, unateua kwa lengo la kupambana na wapinzani au kuleta maendeleo?

Umepotea, labda tafuta mfano mwingine. Huo, hapana. Tenga muda, tafari na utagundua Tanzania ni nchi inayokua kwa kasi ikiongozwa na dhamira na dhamiri za maendeleo. Kama umekalia majungu! Ndg yatakushinda utabaki unalialia tu bila sababu, maana hujitambui.
Uchumi unaporomoka kwa kasi no Sera yoyote unafikiri utakua kwa miujiza. Uwe unatumia common sense uzalendo ni maneno ya kimipasho ya wanasiasa uchwara hata kwenye kanga yapo. Uzalendo alikua nao Nyerere tu wengine wote uchwara tu wamekosa dira.
 
Nilikuwa na matumaini makubwa na jamaa ila nimeona ni Hopeless!!
Sijui kalewa na sifaaa?
Yaani kila siku kuteua na kutengua!!! Hivi utajiskiaje mwanao wa std 2 kasahihishiwa na mwl wa hesabu kapata 8/10, then ana chana karatasi zile na kunakili maswali yaleyale na kujisahihishia upya yy mwenyewe na kuweka vema 10/10!!!!! Huu utakuwa ni uchizi kwa huyu mtoto.
 
Mhe. Rais,una sera nzuri za kimaendeleo. Ilani yetu ya CCM,ahadi zako za papo kwa papo,kauli zako na matendo yako huakisi maendeleo ya Tanzania yetu. Kuwa Tanzania ya Viwanda. Lakini,teuzi zako hazibebi lengo lako hilo. Zinabeba dhima tofauti ya kupambana na kuwabana wapinzani hasa CHADEMA.

Natoa mifano mitatu. Wa kwanza ni uhusuo uteuzi/kupandishwa cheo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda. Makonda alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni. Tangu akiwa UVCCM,Makonda hujichora kama mpambanaji wa wapinzani na kwake hawafurukuti. Kinondoni UKAWA 'wakamtandika' kwa kutwaa majimbo yote. Rais ukasema mahali kuwa Makonda ana wapinzani wengi wanamchukia. Ukaahidi kumpandisha cheo. Ikawa kweli. Ameshaapa kuubomoa UKUTA wa CHADEMA wa hapo Septemba mosi!

Mfano wa pili ni uteuzi wa maDED na maDAS. Humo wamesheheni walewale wenye hulka na michoro ya kupambana na wapinzani. Watoa matamko ya kuponda bila kupenda wapinzani ndiyo wameula kwenye teuzi hizo. Matamko yao humu JF,WatsApp,Facebook na Instagram kuwakandiakandia wapinzani yakawalipa.

Mfano wa tatu ni wa uteuzi wa leo wa Mrisho Gambo. Umetengua uteuzi wa kaka Ntibenda na kumpandisha cheo kwa kumteua Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha. Mrisho Gambo alijaribu kugombea Ubunge Kinondoni. Akabwagwa na Idd Azzan ndani ya CCM yetu. Ni juzi tu amejigamba kuwa yeye ndiye kiboko ya Operesheni UKUTA ya CHADEMA kule Arusha. Gambo amejipambanua kuwa yuko Arusha kupambana na wapinzani wakiongozwa na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless J Lema.

Nia ya teuzi hizi ni ipi hasa? Maendeleo au 'kuwafunika' wapinzani?

Mzee Tupatupa, Dar es Salaam
Shalom mzee tupatupa!!!!!hahahaha naota kama vile hufai kukaa lumumba!!!!!!!!!
 
Jamani mbona hivyo? Msiwastue ngojeni wazidi kujikanyaga, hilo ndiyo kaburi lao, maguvu ya dola hayajawahi kuwa suluhisho hata siku moja, kila siku watu ndiyo wanazidi kupata ujasiri na wao ndiyo wanazidi kujichafua mbele ya jumuia ya kimataifa.
Ni kweli, maguvu ya dola hayajawahi kuwa suluhisho hata siku moja.
 
Back
Top Bottom