Rais Magufuli, unateua kwa lengo la kupambana na wapinzani au kuleta maendeleo?

Magufuli si mwanasiasa na naamini kaiona jana au leo hii siasa, anawaweka hawa anaoamini watamsaidia kwa kujihami lakini hajui kuwa anajiharibia. Anawaweka hao wanaoitwa waropokaji kama mifano yao uliowataja ili sauti za wapinzani zisisikike. Siasa ya namna kama hii alikua nayo Komandoo Dr. Salmini na leo yuko wapi? Zanzibar nzima aliihariu akawaharibu na Wazanzibar wakawa hawajuani zikawa na fitna watu wakaanza kususiana sasa haya anataka kuyaleta Magufuli Tanganyika. Ninamshauri sana aachane na Wanasiasa, Kwanza watampotezea muda wake na pia ajue hapo alipo yuko kwa muda mfupi tu hasa kwa hizi sera zake anazozitumia, kwakua kama ataamua kukaa na wapinzani vizuri hawa ndio wanaweza wakamsaidia kwenye muda wake wa mwisho wa uongozi, hayo yaliwahi pia kutokea Zanzibar kipindi cha Amani Karume. Seif alikuwa anaomba sana Amani aongezewe muda ili aendelee kutawala kutokana na Umoja wa watu ulivokua umeshamiri.


magufuli si mwanasiasa ina maana chama kilichompa ridhaa ya kugombea urais sio cha kisiasa? Alipoacha kazi yake ya ualimu wa chemistry na kugombea ubunge wa jimbo la chato tayar alishajiingiza katika siasa.
 
Kojoa ukalale. Mwache mkulu apige kazi


sioni kama lugha chafu zinamantiki ktk mijadala hizo lugha zilikuwa nzur kipindi tunajifunza kutumia social network kwa sasa hazina maana tena.
 
Mimi naona wakuu wa mikoa wawe wanachaguliwa kwa kupigiwa Kura MAANA naona watu vichwa maji ndio wanapewa hiyo kazi .iwe kama Kenya,Nigeria Na Africa kusini unapambana kwenye kampeni Na uchaguzi ndio inakuwaje mkuu wa mikoa sio cheo CHA kupewa kama bia ya safari au kiroba
 
Mimi naona wakuu wa mikoa wawe wanachaguliwa kwa kupigiwa Kura MAANA naona watu vichwa maji ndio wanapewa hiyo kazi .iwe kama Kenya,Nigeria Na Africa kusini unapambana kwenye kampeni Na uchaguzi ndio unakuwa mkuu wa mikoa sio cheo CHA kupewa kama bia ya safari au kiroba
 
Kuteuliwa kwa kijana makini na machachari, mchapa kazi Mrisho Gambo kunatuma Ujumbe kwa Lema kuwa aache papara maana ataumia bure.
Ajirlekeze kufanya kazi tu kama rais alivyosema.
[HASHTAG]#KapaKaziTu[/HASHTAG].
Hana lolote gambo ataisoma tu namba kwa Lema,mchezo wa mieleka unahitaji timing
 
Back
Top Bottom