Rais Magufuli una ujasiri jukwaani tu

Mimi huwa nashangaa wanaposema tumuombee badala ya kushauri. Kitu ca kwanza katika uongozi ni kufuata taratibu na unapobainisha wazi unafuta taratobu unapongezwa na kuombewa.
 
Mimi huwa nashangaa wanaposema tumuombee badala ya kushauri. Kitu ca kwanza katika uongozi ni kufuata taratibu na unapobainisha wazi unafuta taratobu unapongezwa na kuombewa.
Mkuu ukisema ukweli hawa makondakta wa mwendokasi waliokua humu ndani wana panic sana
 
Kwa jinsi ulivyofunika akili yako kutokuona lolote baya la baba J, hata kama ungemkuta maungoni mwa mama yeyoo wako utatoka na kuhadithia kuwa baraka imekutembelea kwenye familia yako. Na mama yeyoo utampongeza na kumuuliza mtafanya tena lini.

Hoja huna umeishia matusi tu.... Dalili za kufilisika kisiasa...
 
Nchi yenye maliasili nyingi kuliko nchi nyingine yoyote Afrika Mashariki, na kumbe chama kinachoitawala tangu uhuru 'ni bora kabisa Afrika na Duniani kote' Halafu bado kiuchumi inazidiwa na nchi kama kenya, na watu wake wana hali mbaya balaa! Hivi jamani si muwe mnaona aibu hata kidogo basi?! Na huo ubora mnaojisifia kila siku, ni nini kimewafanya kushindwa hivi?!

Wewe si mmoja wa Watanzania ? Wewe unafanya nini kuhakikisha Tanzania inaendelea ? Kushinda unalalama na kukosoa bila kutuelezamchsngo wako haisaidii....
 
Nimpongeze mwandishi wa makala hii kwa kuushirikisha ubongo wake vyema. Najua ni mwandishi wa habari mwenye kuitumia kalamu yake ipasavyo.
Nilisema humu jana kuhusu washauri wa mkulu kuwa na hidden agenda au basi wamemchunia ili jumba bovu limdondokee mwenyewe. Au huenda mshauriwa ni mbishi na anayefikiri kuwa na weledi wa kila jambo.
Waandishi tambueni kuwa ninyi ni mhimili wa nne wenye wajibu wa kuiunganisha mihimili mingine pamoja na wananchi. Igeni uandishi huu usiomung'unya maneno na wenye kumshape kila ausomaye.
 
Lazima atakusoma ama kusomewa...........tatizo anatawala kwa mkakati aliojiwekea.
Demokrasia ya vyama vingi ndio imetufikisha hapa, kwenye umasikini wa kutupwa.
JPM anajaribu kujenga uchumi kupitia mfumo wa chama kimoja............labda tutatoka.
Akiona hii ya kuwabinya wapinzani haizai matunda, huenda tukashuhudia makubwa zaidi (Mungu aepushie mbali).
ushauri wangu; vyama vya siasa vyote vifutwe, sote turudi ccm tujenge nchi. Hapa Kazi Tu
Tulikuwa chini ya Chama kimoja TANU kuanzia mwaka 1961 hadi 1977 CCM ilipozaliwa. CCM iliendelea kutawala had I 1992 vyama vingi viliporuhusiwa. Tunafahamu maendeleo tuliyoyapata chini ya mfumo wa Chama kimoja CCM. Siyo sahihi unaposema vyama Vingi vinachelewesha maendeleo.
 
Nimpongeze mwandishi wa makala hii kwa kuushirikisha ubongo wake vyema. Najua ni mwandishi wa habari mwenye kuitumia kalamu yake ipasavyo.
Nilisema humu jana kuhusu washauri wa mkulu kuwa na hidden agenda au basi wamemchunia ili jumba bovu limdondokee mwenyewe. Au huenda mshauriwa ni mbishi na anayefikiri kuwa na weledi wa kila jambo.
Waandishi tambueni kuwa ninyi ni mhimili wa nne wenye wajibu wa kuiunganisha mihimili mingine pamoja na wananchi. Igeni uandishi huu usiomung'unya maneno na wenye kumshape kila ausomaye.
Nashukuru kwa kuelewa lakini hawa makondakta wa magari ya mwendo kasi wao wanajifanya hawaoni
 
Siwezi kuendelea kufanya hivyo....sasa nisome kitu gani tena hapo...Paragraphs tano tu, zinatosha kujua msimamo wa mtu...very boring indeed...kila siku kulaumu, kulalamika, kushutumu, kujenga hoja zinazopingana, zenye kejeli, dharau, ujivuni ...yaani mnataka kufanya nafasi ya Urais kuwa kama ya balozi wa nyumba kumi...hamjui kuwa nafasi ya urais ni nyeti...na kwamba Rais ni Head of State...na lazima aheshimiwe...

Nyerere baba wa Taifa aliwahi kusema heshima ya mtu katika jamii hutokana na huduma na matendo yake katika jamii husika. Heshima ya mtu haitokani na cheo alichonacho mtu huyo.
 
Mheshimiwa Rais John Magufuli, sijawahi kukuandikia barua, ama ya sanduku la posta au ya mtandaoni. Leo nakuandikia kupitia gazetini kwa sababu mbili, anaandika Ansbert Ngurumo.

Kwanza, natambua kuwa wewe ni msomaji wa magazeti. Naulishanithibitishia kuwa hukosi kusoma maandishi yangu. Kwa hiyo najua utasoma.

Bahati nzuri, ninachokuandika si siri. Ni barua ya wazi itakayosomwa na Watanzania wengine. Lengo la kuiweka wazi ni kukuhamasisha nawe utambue kuwa mawasiliano ya kujenga nchi hayahitaji kufanyikia sirini au gizani.

Hii itakufanya uelewe kwanini wananchi hawachoki kuhoji sababu za serikali yako kufuta matangazo ya bunge ya moja kwa moja. Nakwambia bila kificho kuwa, hata mjieleze vipi, wananchi hawako tayari kuelewa kuwa katika karne hii, bunge lao linaondolewa kwenye nuru na kuingizwa kwenye giza.

Mwanzoni, wananchi, wakiongozwa na wabunge, walimkasirikia Nape Nnauye, waziri uliyempa dhamana ya habari, sanaa, utamaduni na michezo, wakidhani ndiye aliamuru TBC, Shirika la Utangazaji la Taifa, lisitishe matangazo ya moja kwa moja kwa kisingizio cha gharama; kwa sababu ndiye aliyetoa tangazo hilo bungeni.

Lakini sasa wanaelewa kuwa Nape hawezi kufanya uamuzi mkubwa kama huo bila kutumwa na mkubwa wake wa kazi. Na kwa jinsi wanavyokufahamu wewe, kama Nape angekuwa amefanya uamuzi huo wa kijinga bila kukuhusisha au bila kutumwa na wewe, ungekuwa ama umetengua uamuzi huo au umemtumbua jipu.

Kwa sababu hiyo, wananchi wameachanana Nape, wanakuandama wewe, na sasa wanasema jipu hilo ni lako. Unaogopa kujitumbua kwa kuwa mganga hajigangi. Ndiyo maana nimeamua nikutumbue.

Pili, mimi na Watanzania wamegundua kuwa katika masuala mengi ya kitaifa, unadanganywa. Vijana wa mjini wanasema unaingizwa mkenge. Na ukishadanganywa, nawe unaibuka na kudanganya wananchi.

Naomba utambue kuwa kwa kusema haya siombi kazi kwako. Ninayo. Na sehemu ya majukumu yangu kwa taifa hili ni kuuambia wewe ukweli mchungu bila woga au upendeleo.

Tabia yangu hii inasaidia kuziba mapengo ya wasaidizi wako ambao, licha ya kwamba wapo katika majengo wanayoita ofisi, kimsingi hawapo kazini, kwa kuwa hawafanyi kazi yao, hasa ya kukushauri viizuri.

Na baadhi yao wanasema kwamba hushauriki, unafanya utakalo, mara nyingi, bila kupima madhara ya uamuzi wako.

Wanasema hii ndiyo sababu inayokufanya utoe kauli tata au zinazopingana mara kadhaa.

Kwa mfano, mtu mmoja ameandika kwenye mtandao wa kijamii, akinukuu kauli yako uliyotoa kwa hasira mwezi Februari 2016 baada ya MCC, Shirika la Changamoto za Milenia, la Marekani, kukata misaada kwa Tanzania kwa sababu ya wizi wa kura Zanzibar na kutunga sheria katili ya makosa ya mtandaoni.

Siku ile, ulisema hivi: “Haiwezekani nchi tajiri kama Tanzania tuwe ombaomba. Sisi ndio tunatakwa kuombwa misaada.”

Kauli yako ilizua gumzo nchi nzima. Baadhi ya wananchi, wakiwemo marais wastaafu, walisema kuwa misaada kutoka nje haikwepeki, na kwamba hata kama kauli yako ina ukweli wa kimantiki, si kweli katika uhalisia kwa kuwa serikali yako, haijajipanga kujitegemea na kujitosheleza.

Wengine walikudhihaki kuwa umetoa kauli hiyo mithili ya simulizi la sungura aliyeruka akashindwa kufikia mkungu wa ndizi, hatimaye akasema kwa hasira, “sizitaki mbichi hizi!!”

Vibaraka wako, wakiwamo wasaidizi wako, walitetea hoja yako. Mungu si Athuman, juzi umetoa kauli nyingine ulipotembelewa na Balozi wa Mareakani nchini, akaahidi kuipatia serikali yako msaada mkubwa wa dola milioni 800.

Katika furaha uliyokuwa nayo, ulisema hivi mbele ya waandishi wa habari:

“Amekuja balozi kutuhakikishia kwamba watatoa hela kwa ajili ya Tanzania, na anasema sasa hivi watatoa zaidi ya dola milioni 800, na mkataba mwingine tunaweza kusaini hata kesho wa dola milioni 410….Fedha za msaada kutoka Marekani ni muhimu mno kwa maendeleo ya Tanzania.”

Tuna marais wangapi? Februari ulisema hutaki misaada; Juni unasema misaada ni muhimu. Tunapouliza wasaidizi wako kwanini wanakuacha unatoa kauli za ajabu ajabu, wanasema hupendi kushauriwa.

Wanasema kuwa wanaogopa kukuambia usichotaka kusikia, kwa sababu wameshakusoma, unapenda kusikiliza sauti yako mwenyewe na kutanguliza hisia zako, badala ya kufanyia kazi ushauri wa wataalamu.

Eti wakati mwingine wanakuandikia hotuba za kirais katika matukio muhimu, ukishafika eneo la tukio unagoma kuzisoma; unatoa maoni yako ya kichwani, ambayo wakati mwingine yanakufanya uonekane kama kamanda wa polisi bada ya rais wa nchi.

Wanasema, kwa mfano, siku ya maadhimisho wa Wiki ya Sheria, maneno uliyotoa mbele ya wanasheria waliobobea, huku ukimwagiza jaji mkuu, yalikuwa yamekataa tenge, na hayatekelezeki kisheria; ni amri zisizofanana na mfumo wa kidemokrasia na utendaji wa kisheria.

Hawakukuambia pale pale, lakini walikuteta baadaye. Kwanini unaruhusu mambo haya yatokee wakati una nyenzo za kuyazuia?

Mmoja ameniambia wiki hii kuwa kwa jinsi anavyoona unazungumza na unatenda, una nia nzuri na taifa hili, lakini unakosa mbinu za kiuongozi. Anasema unatenda kama meneja, si kiongozi.

Anasema vitu vingine unavyoagiza, au unavyoamua, unavifanya kama mtawala, si kama kiongozi. Na kwa kukosa tunu ya uongozi, utafanya mambo mengi mazuri juu juu lakini hayatadumu kwa sababu hayakujengwa juu ya msingi imara.

Utakuwa umefanikiwa kufanya mambo mema kwa muda mfupi, lakini yatafutika kirahisi kwa kuwa mtindo uliotumika kuyatekeleza si endelevu, bali zima moto.

Wasaidizi wako wanakuficha mambo ya msingi. Wanasema umezidi ukali, na huna subira wala simile, kiasi kwamba unaweza kumwaibisha mtu yeyote mahali popote, bila kujali cheo au hadhi yake.

Na unawafanyia wenzako hivyo, lakini wewe hutaki kuguswa au kusahihishwa. Unalinda cheo chako, unadhalilisha vyeo vyao.

Kama ulikuwa hujajua, washauri wako sasa wana msimamo rasmi, kwamba watakushauri kwa kuzingatia kile unachotaka kusikia kutoka kwao.

Kama msimamo huu utadumu, mheshimiwa rais utaangamiza nchi. Kama unafurahia kuongoza nchi ya watu waoga, ujue nchi hiyo si Tanzania tunayotaka kujenga, au ile unayozungumzia kwenye hotuba zako.

Mazuri yote unayohubiri kwenye hotuba zako, yatatumika kukukejeli baada ya muda wako wa kukaa Ikulu kuisha.

Wanakutii, lakini hawakupendi. Na kwa sababu unawapuuza, wakipata fursa watakuhujumu.

Hata hivyo, wapo pia wanaodhani kwamba huna washauri wazuri. Mtu mmoja amesema; “Tatizo ninaloona sasa hivi, wasaidizi wa rais wanashindwa kutafsiri dira na ajenda yake. Hawamwelewi, naye haeleweki kwao.

“Apende asipende, anahitaji semina elekezi. Uamuzi unaochukuliwa na wasaidizi wake unatokana na tafsiri yao ya dira yake. Wengi wanafanya kwa woga na kulinda ajira zao tu.

“Panapohitajika ushauri wa kitaalamu wanapatwa na ugonjwa wa kupooza, kwa sababu wanaangalia matokeo ya kisiasa na uhusiano wao na rais. Tuanze kujiuliza, rais anaposema ‘Hapa Kazi Tu, ana maana gani?”

Huyu alisema hivi baada ya jeshi la polisi kuzuia mikutano ya wanasiasa kwa sababu zile zile za miaka nenda rudi. Hawakui. Hawaelimiki. Na baadhi ya wakuu katika jeshi la polisi wanadai kuwa “wamefanya hivyo kwa kufuata “maagizo kutoka juu.” Huko juu ni wapi kama si Ikulu?

Uamuzi huu wa kuzuia mikutano ya vyama vya siasa, kwa hofu kwamba itawafanya wananchi waelewe udhaifu wa serikali ya awamu ya tano, na kukuza upinzani ambao umesema mara kadhaa kwamba una nia ya kuuua, unakutia doa.

Uamuzi huu unakuondolea taswira ya ujasiri unayojijengea majukwaani unapokuwa unafoka. Sasa wananchi wanahoji: “Kumbe anafoka kuficha udhaifu wake!”

Ushauri, wangu kwako ni huu: Ongoza nchi, usiitawale. Acha wananchi wapumue. Zungumza nao, usiwahutubie. Sikiliza washauri wasiojikomba kwako.

Kumbuka kuwa nchi hii si ya rais na baraza la mawaziri, bali ni ya wananchi uliokuwa unawaomba kura na kuwaburudisha kwa maneno matamu na pushapu jukwaani. Hawa ndio waajiri wako. Wasikilize. Jifunze kwamba ubabe hautawali nchi yotote katika karne ya sasa.

Wananchi wanatazama mbele, hawatakubali kurudishwa nyuma, hata kwa mabavu.

Umemwaga usaa wote mkuu
 
Tumeipenda wenyewe.... Chaguo letu milele.... Nawavimbe wapasuke...... Watajijua wenyewe....... Achawaisome nambaeeeeee... Sisiemu mbelekwa mbeleee..... Naimba tu msinitolee macho.
 
Nyerere baba wa Taifa aliwahi kusema heshima ya mtu katika jamii hutokana na huduma na matendo yake katika jamii husika. Heshima ya mtu haitokani na cheo alichonacho mtu huyo.

Kwa hiyo kama alisema hivyo Baba wa Taifa sasa ninyi mumeelewa vipi?? Ni nani anaweza ku-question huduma na matendo ya JPM katika jamii yetu????!!!! Yaani ninyi 'wazungusha mikono' mna guts za kutumia kauli za Mwalimu kuhusu masuala ya uongozi wa sasa wa nchi hii?! Sijui umri wako, hivi wewe unamwelewa au ulikuwa unamwelewa vizuri Mwalimu? Yaani mnatumia kauli za Mwalimu ili zi-fit matakwa yenu? Hivi wewe unadhani Mwalimu Nyerere, Baba wa Taifa, angewafanya nini nyie 'wazungusha mikono' mnaokejeli mamlaka ya juu ya nchi hii? Mnadhani mngekaa kwa amani kweli? Sasa ngoja nikwambie kitu: Mwalimu Nyerere was a thinker, msomi, mchapa kazi, mwadilifu, mzalendo, mwana wa Tanzania na Afrika halisi, mchukia rushwa, asiyependa makuu, anayependa watu wake na pamoja na yote haya alikuwa 'disciplinarian'... Unafahamu aliwafanya nini wale wanafunzi wa chuo kikuu Dar es salaam waliogoma kwenda JKT na nadhani kukatwa mishahara na wakadai eti 'afadhali ya mkoloni?'....Fuatilia uambiwe alichofanya ndiyo utasema au kufahamu Mwalimu ni nani au alikuwa alikuwa nani...Mwalimu alikuwa ni mtu asiyependa upuuzi...Waulize wale Wabunge waliojiita G55 waliotaka Tanganyika... Upo wakati wabunge waligomea hoja ya serikali, Mwalimu akatangaza kutaka kuvunja Bunge, wote wakanywea...Mwalimu alikuwa hapendi mchezo, alikuwa mtu mzuri lakini hapendi upuuzi, alikuwa hataki 'utoto', alikuwa anaipenda nchi, alikuwa muumini wa sharia na taratibu...kwa hiyo msije mkanukuu vibaya hoja na kauli za Mwalimu, sisi wengine tumemuona Mwalimu na tumewezeshwa naye kielimu na kimaisha, alipofariki tulitokwa na machozi na machozi yale hayakuwa ya unafiki yalikuwa ya dhati...
 
Wewe si mmoja wa Watanzania ? Wewe unafanya nini kuhakikisha Tanzania inaendelea ? Kushinda unalalama na kukosoa bila kutuelezamchsngo wako haisaidii....
Ndugu, umeona comment ya mtu niliyemjibu?!
Naona wewe mwenyewe hufanyi hicho unachonidai mimi nifanye! Wewe umemueleza nani mchango wako kabla ya kunilalamikia na kunikosoa?!
 
sukari je na vifaa vya ujenzi bei zake zinakuwa hazikui, hata huku umeme sijauona ila nguzo tu.
Tulia kama uko kwa kinyozi. Mag ana miezi sita umeziona nguzo za umeme ambazo ulikuwa hujategemea kuziona kama tungeendelea na serikali ya matanuzi! Halikadhalika being za hivyo ulivyovitaja na vingine zitarekebika tu ndani ya serikali ya HAPA KAZI TU!!!
Bajeti hii unaonaje nyonge amejaliwa? sukari ipo nyingi kweli kweli? Kiwanja cha ndege chato tunabana matumizi... malizia nyingine
Kwa nini mnapenda kuchukua mambo madogo madogo na kuya amplify? Tunachoangalia hapa ni maslahi mapana ya Watanzania. Hivi kweli sukari inaweza ikawa na manufaa kwa mwananchi kuliko barabara ama madawati? Airstrip ikijengwa Chato kuna tatizo gani? Kuna mambo mengi ya kiusalama yanayoweza kusababisha uwepo ulazima wa kufanya hivyo. Ukiwasoma wengi wanaomkosoa Magufuli utaona ni kwa kiwango gani uzalendo umedidimia nchini. Inasikitisha.
 
G
Hivi wakati waziri Dr. Mpango anatoa hali ya uchumi Tanzania pale Bungeni hukumsikia akiongela umasikini kwa kutumia 'data' za last census na household budget survey zilizowekwa kwenye mtindo wa ramani i.e. poverty mapping'? Study ifanyike kujua kiwango cha wananchi wanaohitaji Bunge live au la, na uzito wa uhitaji huo kwa mitazamo yao badala ya kubwagiwa percentages hapa bila kujua zimetokea wapi zaidi ya kuzipata bila process/ approach inayokubalika.
Tatizo lenu watu kama nyie wapenda data mnataka Ku show off kwamba mmesoma! Tanzania hii majority ni watu maskini wa kawaida ambao hawahitaji data! Waziri Mpango anawajibika kutafuta na kuwa na data sahihi zitakazomuwezesha yeye na serikali kupanga mipango ya maendeleo vizuri. Mambo ya data za nani anataka bunge live na nani hataki ni longolongo za kisiasa tu. Ukweli unabaki palepale asilimia kubwa ya maskini wa Tanzania hawana muda wala hizo TV!
 
Tulioula wa chuya sio wa Bunge Live tu, hata aliyetaraji kushuka bei ya sukari naye kaula wa chuya. Kama mwanzo alinunua sukari kwa 2000 na leo anaitafuta mita 400 na akiipata analipa zaidi ya ile 2000 ya awali, ni chuya peke yake au chuya na mawe?

Baba YanguYangu, Bunge Live halileti maendeleo, eti? Sawa, lakini hujatuambia kama kulifuta ni maendeleo. Kwenye nchi hii hii, hotuba ya kuwananga watoto wa nchi wetu wenyewe ilirushwa live. Je, hotuba ile imeleta maendeleo? Tena niliwasahau hao watoto nao, hakika na wao wameula wa chuya. Walitaraji kupata diploma zao wakafundishe sayansi, sasa wako mtaani na jina jipya....******.

Baba YanguYangu, sijui umri wako na sijui ni lini umeanza kusikia neno 'umeme'. Harakati za kuusambaza umeme kwa kasi hazijaanza miezi sita iliyopita, ni muda sasa tunabembelezwa kuomba service line. Labda nikukumbushe tu, asilimia 20 inayokula wa chuya itaongezeka maradufu kila baada ya mwaka na sidhani kama uko mbali kufikiwa.
Bunge live kuleta maendeleo ni hoja mufilisi! Waziri Mkuu Majaliwa alipokuwa London alieleza vizuri sana kwamba madhumuni ya kutoonyesha Bunge live yalikuwa kutaka wananchi kufanya kazi badala ya kuacha kufanyakazi kuangalia bunge! Na hao wa udom kama waliingia kihalali there is nothing to worry about, wameambiwa watarudishwa chuoni na kuendelea na masomo. Kinachofanywa na Serikali ya Magufuli ni kurekebisha makosa na uozo uliofanywa huko nyuma ili angalau nchi irudi kwenye mstari kwa manufaa ya Watanzania kwa ujumla.
 
Ukiona kondo kama wewe umechepuka nje ya mstari jua kuna kitu mwilini kinawasha
Tatizo watanzania hatuna misimamo, na ni rahisi kutumika, leo imeingia serikali makini madarakani mnalia eti Rais anawaburuza, alivyo waachia Kikwete mfanye mtakalo mlimvua nguo na kumuita "dhaifu" na kila aina ya kejeli zilizo jaa dharau na utovu wa nidhani uliopitiliza. Hivi jiulize yule ni baba mwenye familia yake, ni kiongozi wa juu wa nchi, ni mtu mzima ambaye kwa yote haya alistahili heshima, mnamuita dhaifu? tena watoto wadogo kabisa akina Mnyika na wenzie. Aliwachia watanzania wote wafanye yote watakayo, mema na mabaya haikutosha mkamuona ni dhaifu, aliwaachia nyinyi waandishi mfanye mtakavyo hadi mkavuka mipaka ya uhuru wa wenu, lakini bado mbele yenu akawa dhaifu, sasa huo ndio ukawa wimbo wa watanzania hadi serikali nayo mkaiita dhaifu. Vyombo vya ulinzi na usalama vikawaacha watanzania wafanye watakalo kwa kulinda demokrasia, lakini kwenu ilikuwa ni udhaifu.
Ikafikia wakati sasa wakuhitaji Rais madhubuti, imara, mkali (maana Kikwete mlisema anachekacheka) na mlipita nchi yote mkidai mabadiliko...Ndugu yangu na watanzania wote, milichokuwa mnahitaji ni nini? Si Rais mwenye kuenenda na vitendo? Si Serikali Imara inayo jali maslahi ya Taifa kwa ujumla wake? Si Mabadiliko..sasa nini mnataka tena?
 
Nyie mnaolilia bunge live hadi leo mmeula wa chuya kwa sababu Rais Magufuli in kiongozi mweledi sana anayejua vizuri sana juu ya mahitaji ya asilimia 80 ya wananchi anaowaongoza. Hii asilimia 80 ya wananchi bunge live sio hitaji muhimu kwao! Kwa taarifa tu mie ni miongoni mwa hiyo asilimia 80 ya wananchi tusiohitaji hill Bunge live maana bunge live halituletei maendeleo. Sisi asililimia 80 tangu Magufuli aingie madarakani tunaona MAENDELEO LIVE kila kukicha! Kwa mfano maskini wa eneo letu tulikuwa hatuna ndoto ya kupata umeme tulikuwa tukiona nguzo za umeme zikienda kwa wenye fedha. Sisi tunaambiwa tukitaka umeme tununue nguzo kwa gharama ya laki tatu na zaidi. Lakini ameingia Magufuli nguzo zinatandazwa kwa kasi ya ajabu ambayo hatujawahi kuiona. Barabara zinakarabatiwa na mpya kujengwa kila Siku! Wanafunzi waliokuwa wanaketi chini miaka nenda rudi sasa wana matumainivya kuketi kwenye madawati ..... Ilimradi sasa tumepata Rais anayeleta maendeleo live kwa wananchi. Sasa hivi asilimia 80 ya wananchi maskini wa nchi hii wanaona na kujisikia wamepata Rais anayewajali kwa dhati na ambaye hajatokea tangu Nyerere aondoke madarakani! Enyi asilimia 20 hebu acheni ubinafsi wenu na muwahurumie asilimia 80 ambao Rais Magufuli ameamua kuwashughulikia na kuwasaidia kwa hali na Mali.

Hawawezi kuyaona unayoyaona.Fedha haramu imehamisha.Mwandishi ni mmoja kati ya watu ambao ukisoma makala zake alizoandika kuishia August,2015 na anachoandika na kukitetea sasa hutajua njia anayotaka tupite.
 
Back
Top Bottom