Rais Magufuli una ujasiri jukwaani tu

Rais Magufuli una ujasiri jukwaani tu

Kuna cha kujifunza kwenye makala hii,ila ni kwa yule mwenye kuzingatia
 
CCM kitaendelea kuwa chama bora kabisa barani africa na duniani kote.
Nchi yenye maliasili nyingi kuliko nchi nyingine yoyote Afrika Mashariki, na kumbe chama kinachoitawala tangu uhuru 'ni bora kabisa Afrika na Duniani kote' Halafu bado kiuchumi inazidiwa na nchi kama kenya, na watu wake wana hali mbaya balaa! Hivi jamani si muwe mnaona aibu hata kidogo basi?! Na huo ubora mnaojisifia kila siku, ni nini kimewafanya kushindwa hivi?!
 
Sina shaka na maandiko ya waandishi hawa wachumia tumbo, ambao walitumika sana katika kinyang'anyiro cha Urais huku wakiwa wamepewa ahadi lukuki.. Kwa hiyo anacho kiandika ni matokeo ya njaa Kali anayo ipitia sasa hivi na maumivu ya kutotimia kwa ahadi alizo ahidiwa.
Watanzania tuwapuuze waandishi wenye kutumiwa na kutekeleza matakwa ya njaa zao, sisi watanzania ni wakati Wa kuijenga nchi, ni wakati Wa kuleta maendeleo kwa vitendo. Kama unataka kurekebisha au kujenga upya palipo haribika... Ni lazima ubomoe kwanza ndipo ujenge upya. Anacho kifanya Rais Magufuli ni kubomoa na kujenga upya...acheni kulia lia, nchi haijengwi siku moja.
 
Magufuli sometimes anatia huruma
manake hajui jinsi ambavyo ni rahisi kwake kuingizwa mkenge...

umuhimu wa yeye kupata taaarifa sahihi nje ya watu waliomzunguka ni mkubwa sana..
vinginevyo siku moja anaweza jikuta ame ongea vitu vya kumuaibisha sana

Kikwete siku ile anahutubia habari za mapanki ilikuwa aibu kupita maelezo
nchi nzima haikumuelewa anakataa nini na washauri wake wanamshauri nini...

Alipaswa kuisoma ile hadithi ya 'Mfalme aliekuwa anaambiwa umependeza kupita kiasi'
kumbe Mfalme yuko uchi.....

Shida ya washauri wa Rais Magufuli ndo wanashauriwa na rais mwenyewe.
 
Huyu mtu ni mchambuzi makini na mwenye akili sana sijui ni kijana au mzee ila ni mfano wa kuigwa nimemuelewa sana nini lengo la ujumbe wake kwa hadhira. narudia Asante sana Mkuu
 
Teh Teh habari nzima imejaa fikra za vijiweni oooh wanasema ooooh wanasema ooh wanasema..
Hii taka taka peleka kwa Mbowe na Lowasa Rais hana muda wa kusoma huu upuuzi!

Wakati wa mikutano si sasa subirini kipindi cha uchaguzi 2020!
Kwa jinsi ulivyofunika akili yako kutokuona lolote baya la baba J, hata kama ungemkuta maungoni mwa mama yeyoo wako utatoka na kuhadithia kuwa baraka imekutembelea kwenye familia yako. Na mama yeyoo utampongeza na kumuuliza mtafanya tena lini.
 
Magufuli ni Rais mzuri na mchapakazi, kama binadamu hakosi mapungufu, na mapungufu ndiyo kama haya ambayo watu wanalia kila kona wakiomba awasikilize. Nashauri baadhi ya shauri zenye manufaa azichukue na kuzifanyia kazi ili nchi isonge mbele.
 
Kumbe maneno yote hayo kumbe hoja ni bunge live. Mabadiliko ya kweli ndicho raisi anachofanya na alikiahidi. Mabadiliko haya ya kweli ni pamoja na tunavyoendesha siasa zetu, likiwemo hili la bunge kuonyeshwa live 24 hours lililoanzishwa katika awamu ya nne.

Mjadala wa bunge live ulishafungwa kitambo, mtazoea tu. Ukweli ni kuwa hakuna ko kote duniani ambako bunge huonyeshwa live. Only in Tanzania ilikuwa ikifanyika hivyo. Serikali ya awamu hii inajitahidi kunyoosha nchi, wengine lazima maumivu yawapate. Tuiache ifanye hayo mabadiliko, tutaipima 2020.
Ukiwa na akili nusu kijiko siyo rahisi kuelewa
 
Sina shaka na maandiko ya waandishi hawa wachumia tumbo, ambao walitumika sana katika kinyang'anyiro cha Urais huku wakiwa wamepewa ahadi lukuki.. Kwa hiyo anacho kiandika ni matokeo ya njaa Kali anayo ipitia sasa hivi na maumivu ya kutotimia kwa ahadi alizo ahidiwa.
Watanzania tuwapuuze waandishi wenye kutumiwa na kutekeleza matakwa ya njaa zao, sisi watanzania ni wakati Wa kuijenga nchi, ni wakati Wa kuleta maendeleo kwa vitendo. Kama unataka kurekebisha au kujenga upya palipo haribika... Ni lazima ubomoe kwanza ndipo ujenge upya. Anacho kifanya Rais Magufuli ni kubomoa na kujenga upya...acheni kulia lia, nchi haijengwi siku moja.
Ukiona kondo kama wewe umechepuka nje ya mstari jua kuna kitu mwilini kinawasha
 
We ni mbwiga kabisa kutokea duniani... Hivi content yote hiyo hilo ndio umeona swali kweli!..... We ni wa mwisho duniani.

Hili ndilo tatizo kubwa la binadamu wenye a borderline analytical mind!!!

We kwa mawazo yako unafikiri size/ukubwa wa content ni always directly propotional na maandishi yenye substance - kama una amini hivyo basi nasikitika kukwambia kwamba "YOU ARE DEAD WRONG."

Wewe uoni kwamba mleta mada ni master of disguise anajaribu kutumia a diplomatic language mwanzoni kuwachota watu akili lakini ukweli wa mambo lengo lake kuu ni kubeza beza effort za Dk.Magufuli, oh yes amukatishe tamaa JPJM, as far as mleta mada is concern everything Magufuli kina walakini!!! Ndio baadhi ya binadamu wenzetu tulivyo.

Ndio maana ninesena kama hakumpigia kura ya ndio Dk.Magufuli hatutaki kusikia ushauri wake wa kinafiki, subirini zamu yenu mkifanikiwa kwenda Magogoni fanyeni miujiza yenu ya kuzunguka Dunia in eight Days.
 
Hili ndilo tatizo kubwa la binadamu wenye a borderline analytical mind!!!

We kwa mawazo yako unafikiri size/ukubwa wa content ni always directly propotional na maandishi yenye substance - kama una amini hivyo basi nasikitika kukwambia kwamba "YOU ARE DEAD WRONG."

Wewe uoni kwamba mleta mada ni master of disguise anajaribu kutumia a diplomatic language mwanzoni kuwachota watu akili lakini ukweli wa mambo lengo lake kuu ni kubeza beza effort za Dk.Magufuli, oh yes amukatishe tamaa JPJM, as far as mleta mada is concern everything Magufuli kina walakini!!! Ndio baadhi ya binadamu wenzetu tulivyo.

Ndio maana ninesena kama hakumpigia kura ya ndio Dk.Magufuli hatutaki kusikia ushauri wake wa kinafiki, subirini zamu yenu mkifanikiwa kwenda Magogoni fanyeni miujiza yenu ya kuzunguka Dunia in eight Days.
Mbon mkifika kwenye swala la ukweli au kukosolewa mnatoka povu sana?
 
Mheshimiwa Rais John Magufuli, sijawahi kukuandikia barua, ama ya sanduku la posta au ya mtandaoni. Leo nakuandikia kupitia gazetini kwa sababu mbili, anaandika Ansbert Ngurumo.

Kwanza, natambua kuwa wewe ni msomaji wa magazeti. Naulishanithibitishia kuwa hukosi kusoma maandishi yangu. Kwa hiyo najua utasoma.

Bahati nzuri, ninachokuandika si siri. Ni barua ya wazi itakayosomwa na Watanzania wengine. Lengo la kuiweka wazi ni kukuhamasisha nawe utambue kuwa mawasiliano ya kujenga nchi hayahitaji kufanyikia sirini au gizani.

Hii itakufanya uelewe kwanini wananchi hawachoki kuhoji sababu za serikali yako kufuta matangazo ya bunge ya moja kwa moja. Nakwambia bila kificho kuwa, hata mjieleze vipi, wananchi hawako tayari kuelewa kuwa katika karne hii, bunge lao linaondolewa kwenye nuru na kuingizwa kwenye giza.

Mwanzoni, wananchi, wakiongozwa na wabunge, walimkasirikia Nape Nnauye, waziri uliyempa dhamana ya habari, sanaa, utamaduni na michezo, wakidhani ndiye aliamuru TBC, Shirika la Utangazaji la Taifa, lisitishe matangazo ya moja kwa moja kwa kisingizio cha gharama; kwa sababu ndiye aliyetoa tangazo hilo bungeni.

Lakini sasa wanaelewa kuwa Nape hawezi kufanya uamuzi mkubwa kama huo bila kutumwa na mkubwa wake wa kazi. Na kwa jinsi wanavyokufahamu wewe, kama Nape angekuwa amefanya uamuzi huo wa kijinga bila kukuhusisha au bila kutumwa na wewe, ungekuwa ama umetengua uamuzi huo au umemtumbua jipu.

Kwa sababu hiyo, wananchi wameachanana Nape, wanakuandama wewe, na sasa wanasema jipu hilo ni lako. Unaogopa kujitumbua kwa kuwa mganga hajigangi. Ndiyo maana nimeamua nikutumbue.

Pili, mimi na Watanzania wamegundua kuwa katika masuala mengi ya kitaifa, unadanganywa. Vijana wa mjini wanasema unaingizwa mkenge. Na ukishadanganywa, nawe unaibuka na kudanganya wananchi.

Naomba utambue kuwa kwa kusema haya siombi kazi kwako. Ninayo. Na sehemu ya majukumu yangu kwa taifa hili ni kuuambia wewe ukweli mchungu bila woga au upendeleo.

Tabia yangu hii inasaidia kuziba mapengo ya wasaidizi wako ambao, licha ya kwamba wapo katika majengo wanayoita ofisi, kimsingi hawapo kazini, kwa kuwa hawafanyi kazi yao, hasa ya kukushauri viizuri.

Na baadhi yao wanasema kwamba hushauriki, unafanya utakalo, mara nyingi, bila kupima madhara ya uamuzi wako.

Wanasema hii ndiyo sababu inayokufanya utoe kauli tata au zinazopingana mara kadhaa.

Kwa mfano, mtu mmoja ameandika kwenye mtandao wa kijamii, akinukuu kauli yako uliyotoa kwa hasira mwezi Februari 2016 baada ya MCC, Shirika la Changamoto za Milenia, la Marekani, kukata misaada kwa Tanzania kwa sababu ya wizi wa kura Zanzibar na kutunga sheria katili ya makosa ya mtandaoni.

Siku ile, ulisema hivi: “Haiwezekani nchi tajiri kama Tanzania tuwe ombaomba. Sisi ndio tunatakwa kuombwa misaada.”

Kauli yako ilizua gumzo nchi nzima. Baadhi ya wananchi, wakiwemo marais wastaafu, walisema kuwa misaada kutoka nje haikwepeki, na kwamba hata kama kauli yako ina ukweli wa kimantiki, si kweli katika uhalisia kwa kuwa serikali yako, haijajipanga kujitegemea na kujitosheleza.

Wengine walikudhihaki kuwa umetoa kauli hiyo mithili ya simulizi la sungura aliyeruka akashindwa kufikia mkungu wa ndizi, hatimaye akasema kwa hasira, “sizitaki mbichi hizi!!”

Vibaraka wako, wakiwamo wasaidizi wako, walitetea hoja yako. Mungu si Athuman, juzi umetoa kauli nyingine ulipotembelewa na Balozi wa Mareakani nchini, akaahidi kuipatia serikali yako msaada mkubwa wa dola milioni 800.

Katika furaha uliyokuwa nayo, ulisema hivi mbele ya waandishi wa habari:

“Amekuja balozi kutuhakikishia kwamba watatoa hela kwa ajili ya Tanzania, na anasema sasa hivi watatoa zaidi ya dola milioni 800, na mkataba mwingine tunaweza kusaini hata kesho wa dola milioni 410….Fedha za msaada kutoka Marekani ni muhimu mno kwa maendeleo ya Tanzania.”

Tuna marais wangapi? Februari ulisema hutaki misaada; Juni unasema misaada ni muhimu. Tunapouliza wasaidizi wako kwanini wanakuacha unatoa kauli za ajabu ajabu, wanasema hupendi kushauriwa.

Wanasema kuwa wanaogopa kukuambia usichotaka kusikia, kwa sababu wameshakusoma, unapenda kusikiliza sauti yako mwenyewe na kutanguliza hisia zako, badala ya kufanyia kazi ushauri wa wataalamu.

Eti wakati mwingine wanakuandikia hotuba za kirais katika matukio muhimu, ukishafika eneo la tukio unagoma kuzisoma; unatoa maoni yako ya kichwani, ambayo wakati mwingine yanakufanya uonekane kama kamanda wa polisi bada ya rais wa nchi.

Wanasema, kwa mfano, siku ya maadhimisho wa Wiki ya Sheria, maneno uliyotoa mbele ya wanasheria waliobobea, huku ukimwagiza jaji mkuu, yalikuwa yamekataa tenge, na hayatekelezeki kisheria; ni amri zisizofanana na mfumo wa kidemokrasia na utendaji wa kisheria.

Hawakukuambia pale pale, lakini walikuteta baadaye. Kwanini unaruhusu mambo haya yatokee wakati una nyenzo za kuyazuia?

Mmoja ameniambia wiki hii kuwa kwa jinsi anavyoona unazungumza na unatenda, una nia nzuri na taifa hili, lakini unakosa mbinu za kiuongozi. Anasema unatenda kama meneja, si kiongozi.

Anasema vitu vingine unavyoagiza, au unavyoamua, unavifanya kama mtawala, si kama kiongozi. Na kwa kukosa tunu ya uongozi, utafanya mambo mengi mazuri juu juu lakini hayatadumu kwa sababu hayakujengwa juu ya msingi imara.

Utakuwa umefanikiwa kufanya mambo mema kwa muda mfupi, lakini yatafutika kirahisi kwa kuwa mtindo uliotumika kuyatekeleza si endelevu, bali zima moto.

Wasaidizi wako wanakuficha mambo ya msingi. Wanasema umezidi ukali, na huna subira wala simile, kiasi kwamba unaweza kumwaibisha mtu yeyote mahali popote, bila kujali cheo au hadhi yake.

Na unawafanyia wenzako hivyo, lakini wewe hutaki kuguswa au kusahihishwa. Unalinda cheo chako, unadhalilisha vyeo vyao.

Kama ulikuwa hujajua, washauri wako sasa wana msimamo rasmi, kwamba watakushauri kwa kuzingatia kile unachotaka kusikia kutoka kwao.

Kama msimamo huu utadumu, mheshimiwa rais utaangamiza nchi. Kama unafurahia kuongoza nchi ya watu waoga, ujue nchi hiyo si Tanzania tunayotaka kujenga, au ile unayozungumzia kwenye hotuba zako.

Mazuri yote unayohubiri kwenye hotuba zako, yatatumika kukukejeli baada ya muda wako wa kukaa Ikulu kuisha.

Wanakutii, lakini hawakupendi. Na kwa sababu unawapuuza, wakipata fursa watakuhujumu.

Hata hivyo, wapo pia wanaodhani kwamba huna washauri wazuri. Mtu mmoja amesema; “Tatizo ninaloona sasa hivi, wasaidizi wa rais wanashindwa kutafsiri dira na ajenda yake. Hawamwelewi, naye haeleweki kwao.

“Apende asipende, anahitaji semina elekezi. Uamuzi unaochukuliwa na wasaidizi wake unatokana na tafsiri yao ya dira yake. Wengi wanafanya kwa woga na kulinda ajira zao tu.

“Panapohitajika ushauri wa kitaalamu wanapatwa na ugonjwa wa kupooza, kwa sababu wanaangalia matokeo ya kisiasa na uhusiano wao na rais. Tuanze kujiuliza, rais anaposema ‘Hapa Kazi Tu, ana maana gani?”

Huyu alisema hivi baada ya jeshi la polisi kuzuia mikutano ya wanasiasa kwa sababu zile zile za miaka nenda rudi. Hawakui. Hawaelimiki. Na baadhi ya wakuu katika jeshi la polisi wanadai kuwa “wamefanya hivyo kwa kufuata “maagizo kutoka juu.” Huko juu ni wapi kama si Ikulu?

Uamuzi huu wa kuzuia mikutano ya vyama vya siasa, kwa hofu kwamba itawafanya wananchi waelewe udhaifu wa serikali ya awamu ya tano, na kukuza upinzani ambao umesema mara kadhaa kwamba una nia ya kuuua, unakutia doa.

Uamuzi huu unakuondolea taswira ya ujasiri unayojijengea majukwaani unapokuwa unafoka. Sasa wananchi wanahoji: “Kumbe anafoka kuficha udhaifu wake!”

Ushauri, wangu kwako ni huu: Ongoza nchi, usiitawale. Acha wananchi wapumue. Zungumza nao, usiwahutubie. Sikiliza washauri wasiojikomba kwako.

Kumbuka kuwa nchi hii si ya rais na baraza la mawaziri, bali ni ya wananchi uliokuwa unawaomba kura na kuwaburudisha kwa maneno matamu na pushapu jukwaani. Hawa ndio waajiri wako. Wasikilize. Jifunze kwamba ubabe hautawali nchi yotote katika karne ya sasa.

Wananchi wanatazama mbele, hawatakubali kurudishwa nyuma, hata kwa mabavu.
 
Nyie mnaolilia bunge live hadi leo mmeula wa chuya kwa sababu Rais Magufuli in kiongozi mweledi sana anayejua vizuri sana juu ya mahitaji ya asilimia 80 ya wananchi anaowaongoza. Hii asilimia 80 ya wananchi bunge live sio hitaji muhimu kwao! Kwa taarifa tu mie ni miongoni mwa hiyo asilimia 80 ya wananchi tusiohitaji hill Bunge live maana bunge live halituletei maendeleo. Sisi asililimia 80 tangu Magufuli aingie madarakani tunaona MAENDELEO LIVE kila kukicha! Kwa mfano maskini wa eneo letu tulikuwa hatuna ndoto ya kupata umeme tulikuwa tukiona nguzo za umeme zikienda kwa wenye fedha. Sisi tunaambiwa tukitaka umeme tununue nguzo kwa gharama ya laki tatu na zaidi. Lakini ameingia Magufuli nguzo zinatandazwa kwa kasi ya ajabu ambayo hatujawahi kuiona. Barabara zinakarabatiwa na mpya kujengwa kila Siku! Wanafunzi waliokuwa wanaketi chini miaka nenda rudi sasa wana matumainivya kuketi kwenye madawati ..... Ilimradi sasa tumepata Rais anayeleta maendeleo live kwa wananchi. Sasa hivi asilimia 80 ya wananchi maskini wa nchi hii wanaona na kujisikia wamepata Rais anayewajali kwa dhati na ambaye hajatokea tangu Nyerere aondoke madarakani! Enyi asilimia 20 hebu acheni ubinafsi wenu na muwahurumie asilimia 80 ambao Rais Magufuli ameamua kuwashughulikia na kuwasaidia kwa hali na Mali.

Tulioula wa chuya sio wa Bunge Live tu, hata aliyetaraji kushuka bei ya sukari naye kaula wa chuya. Kama mwanzo alinunua sukari kwa 2000 na leo anaitafuta mita 400 na akiipata analipa zaidi ya ile 2000 ya awali, ni chuya peke yake au chuya na mawe?

Baba YanguYangu, Bunge Live halileti maendeleo, eti? Sawa, lakini hujatuambia kama kulifuta ni maendeleo. Kwenye nchi hii hii, hotuba ya kuwananga watoto wa nchi wetu wenyewe ilirushwa live. Je, hotuba ile imeleta maendeleo? Tena niliwasahau hao watoto nao, hakika na wao wameula wa chuya. Walitaraji kupata diploma zao wakafundishe sayansi, sasa wako mtaani na jina jipya....vilaza.

Baba YanguYangu, sijui umri wako na sijui ni lini umeanza kusikia neno 'umeme'. Harakati za kuusambaza umeme kwa kasi hazijaanza miezi sita iliyopita, ni muda sasa tunabembelezwa kuomba service line. Labda nikukumbushe tu, asilimia 20 inayokula wa chuya itaongezeka maradufu kila baada ya mwaka na sidhani kama uko mbali kufikiwa.
 
Dalili ya mvua ni mawingu kama sukari imekua mwendokasi ndio viwanda
Kabla hujazama kwenye ukosoaji jaribu kutafuta data zaidi ili ujue serikali inafanya nini inatarajia kufanya nini. Na huo ndio uandishi wa habari wenye kuzingatia maadili ya taaluma, tafuta habari kutoka pande zote ili unachoadnika kisiwe kimeegemea upande mmoja tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom