Rais Magufuli una ujasiri jukwaani tu

Rais Magufuli una ujasiri jukwaani tu

Baba J is visionless , huyu alitakiwa awe mwalimu wa shule ya msingi asubiri kupangiwa Ratiba tu.

Nchi haiendeshwi kama anavyofikiri
 
Huyu Ngurumo anajuaje kwamba Magufuli anadanganywa?

Mengine yuko spot on.
 
Nyie mnaolilia bunge live hadi leo mmeula wa chuya kwa sababu Rais Magufuli in kiongozi mweledi sana anayejua vizuri sana juu ya mahitaji ya asilimia 80 ya wananchi anaowaongoza. Hii asilimia 80 ya wananchi bunge live sio hitaji muhimu kwao! Kwa taarifa tu mie ni miongoni mwa hiyo asilimia 80 ya wananchi tusiohitaji hill Bunge live maana bunge live halituletei maendeleo. Sisi asililimia 80 tangu Magufuli aingie madarakani tunaona MAENDELEO LIVE kila kukicha! Kwa mfano maskini wa eneo letu tulikuwa hatuna ndoto ya kupata umeme tulikuwa tukiona nguzo za umeme zikienda kwa wenye fedha. Sisi tunaambiwa tukitaka umeme tununue nguzo kwa gharama ya laki tatu na zaidi. Lakini ameingia Magufuli nguzo zinatandazwa kwa kasi ya ajabu ambayo hatujawahi kuiona. Barabara zinakarabatiwa na mpya kujengwa kila Siku! Wanafunzi waliokuwa wanaketi chini miaka nenda rudi sasa wana matumainivya kuketi kwenye madawati ..... Ilimradi sasa tumepata Rais anayeleta maendeleo live kwa wananchi. Sasa hivi asilimia 80 ya wananchi maskini wa nchi hii wanaona na kujisikia wamepata Rais anayewajali kwa dhati na ambaye hajatokea tangu Nyerere aondoke madarakani! Enyi asilimia 20 hebu acheni ubinafsi wenu na muwahurumie asilimia 80 ambao Rais Magufuli ameamua kuwashughulikia na kuwasaidia kwa hali na Mali.
Sukari mnapata?
 
Wengine hata vikishuka hamjui Na uwezo WA kujenga haupo. Kwa tarifa fupi Tu bei cement Dar August 2015 ilikuwa 13500 kwa sasa inauzwa kati ya 10000 na 11000 kwa reja reja. Ishuke kwa kiwango gani.au ni mkumbp tu
Hujui unachokiandika ww, nyie ndo mnaompeleka baba j.esikha pabaya
 
Ukiona wapinzani wako wanakuandama kwamba wewe ni mbaya.... Jua kuwa wewe ni mzuri haijapata kutokea...
 
Sio suala la kusifiwa tu ni suala la kutaka Rais apewe nafasi afanye aliyodhamiria kufanya kwa manufaa ya maskini wa nchi hii. Mngelikuwa mnajua ukali wa maisha ya wanyonge wa nchi hii na kama kweli mnayo nia njema ya kutaka wanyonge nao wanufaike angalau kidogo tu mngeelewa juhudi za Magufuli na kumsaidia.
Juhud za kuzuia sukar ya nje ili ya ndan ipande bei? sukar ilikua 1800 saiv 3000 na baba jesca yuko kimya tu kama haoni akat hili tatizo alilianzisha yeye. Acha kunya, andika hoja zenye msingi.
 
Kuiongoza Tanzania kwa ilipofikia hakuhitaji kuuungwa mkono ila nia njema tu inatosha na utashi wa kufanya hivyo. Wananchi walikuwa wezi, viongozi walikuwa wezi na vibaka na watu wa dili, wafanyakazi hewa, ten percent, vyama vyote vilikuwa kwa ajili ya maslahi yao, watu walikuwa wanafanya biashara haramu, kwa kifupi mambo mengi yaliyokuwa yanaendelea ni haramu na watu wengi ni haramu, sasa unatarajia kuungwa mkono na hawa watu ulikatisha ulaji wao haramu? Ni jambo la kushangaza unamkuta Mtanzania anamshukuru Mungu biashara yake inaenda vizuri eti kwasababu kawapiga chenga TRA, kapata kazi nzuri kwa kuhonga, analipwa mshahara wakati hafanyi kazi, kajenga nyumba na kununua gari kwasabubu kaiba hela za miradi ya maendeleo au kaiibia kampuni anayofanyia kazi, kapata degree bila kuisomea na GPA yake ni ya juu, kaenda ulaya kufanya manunuzi kwa kudanganya anaenda semina, hawa ndio Watanzania wanaomini katika ujanjaujanja na wana vivuli vingi sana na wanajua jinsi ya kukimbia vivuli vyao.
Rais atakayetaka kufanikiwa na kuja kukumbukwa na vizazi vijavyo achague kuchukiwa na Watanzania, ajitoe mhanga kutowasikiliza kabisa, ila aongozwe na dira tu, nchi yote ni ya wanaharakati, wajuaji na kila Mtanzania kwa bahati nzuri anajua sababu za sisi kuwa masikini ila hajui njia za kuondoa umasikini.
Pole sana Rais, unayo safari ndefu sana, na kama hutauvaa ukichaa basi nchi hii utaiacha masikini zaidi kuliko ulivyoikuta
Unataka kusema raisi anapingana na mafisadi? bac eleza kwann hatak swala la nyumba za serikal kuongelewa bungen na swala la lugumi
 
Kumbe maneno yote hayo kumbe hoja ni bunge live. Mabadiliko ya kweli ndicho raisi anachofanya na alikiahidi. Mabadiliko haya ya kweli ni pamoja na tunavyoendesha siasa zetu, likiwemo hili la bunge kuonyeshwa live 24 hours lililoanzishwa katika awamu ya nne.

Mjadala wa bunge live ulishafungwa kitambo, mtazoea tu. Ukweli ni kuwa hakuna ko kote duniani ambako bunge huonyeshwa live. Only in Tanzania ilikuwa ikifanyika hivyo. Serikali ya awamu hii inajitahidi kunyoosha nchi, wengine lazima maumivu yawapate. Tuiache ifanye hayo mabadiliko, tutaipima 2020.
Mkuu, hivi tatizo ni hilo la 'hakuna kokote duniani....' au ni nini? Kama tuna nia ya dhati ya kuiga kwa wenzetu kwa nini hatuweki adhabu ya kunyongwa kwa wote wanaopatikana na hatia ya ufisadi na rushwa kubwa kwa mfano kama China?! Mbona hatuigi nchi ambazo rais akitoka madarakani hana kinga ili kama alitumia ofisi vibaya ashitakiwe? Huko duniani mnakosema inakuwaje ikitokea kiongozi amedanganya taifa?
 
Wananchi gani hao wenye kutazama mbele....hawa
1.Walioahidiwa milioni 50 Kila kijiji wakasahau kudai? (Ahadi ni deni)
2. Hawa hawa waliopotezwa kwenye hoja muhimu kama za sukari, Lugumi?
3. Na nyingine nyingi?

Wadanganyika tunayo safari ndefu.....
Failure State...... Hahahahahaaaaaaaaa....eeeeeeeheheheheheeeeeeeeeeee!!!!!!!
 
Ukiona wapinzani wako wanakuandama kwamba wewe ni mbaya.... Jua kuwa wewe ni mzuri haijapata kutokea...
Dah mkuu! Taratibu basi... Kwa mtazamo wako huu kikwete alikuwa mzuri haijapata kutokea... na magufuli ni mzuri haijapata kutokea! Na kumbuka serikali ya ccm na vyombo vyake vyote wanawaandama sana wapinzani kwamba ni wabaya.... Kwa hiyo na wao pia ni wazuri haijapata kutokea!
Kama tumekuwa/tuna viongozi wazuri kiasi hicho, huu mkwamo kwa kila sekta unatoka wapi?!
 
Lazima atakusoma ama kusomewa...........tatizo anatawala kwa mkakati aliojiwekea.
Demokrasia ya vyama vingi ndio imetufikisha hapa, kwenye umasikini wa kutupwa.
JPM anajaribu kujenga uchumi kupitia mfumo wa chama kimoja............labda tutatoka.
Akiona hii ya kuwabinya wapinzani haizai matunda, huenda tukashuhudia makubwa zaidi (Mungu aepushie mbali).
ushauri wangu; vyama vya siasa vyote vifutwe, sote turudi ccm tujenge nchi. Hapa Kazi Tu
Kazi ipo kama mawazo yenyewe ndio haya,kwani ni lini hii nchi imewahi ongozwa na upinzani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom