Congo
JF-Expert Member
- Mar 13, 2008
- 2,075
- 2,316
Katika hotuba yako kuhusu matokeo ya kamati ya kuchunguza mchanga ulio katika makontena, hukuzungumzia hatua zozote zinazopasawa kuchukuliwa dhidi ya kampuni ya Acacia iliyoshiriki kwa kiwango kikubwa kwenye huu udanganyifu.
Ni kampuni hii iliyowandanganya maofisa wa serikali wakasababisha upotevu huu kufanyika. Rais, wachukulie hatua watu hawa wa Acacia. Kibaya zaidi wameanza kutoa taarifa kupingana na taarifa ya serikali. Hawana aibu hawa. Nilitazamia wafungashe virago waondoke. Wametuibia kiasi cha kutosha. Mkataba wao sio wa kuliibia taifa.
Pili, nakuomba uangalie jambo jingine. Baada ya uchimbaji wa madini kwenye migodi mikubwa kama GGM na Nyamongo ndege zilizobeba madini huruka moja kwa moja kutoka viwanja vilivyoko kwenye mogodi yao kwenda nje ya nchi?
Ninachojua dhahabu inatakiwa kuhifadhiwa Benki Kuu, wakitaka kuiuza wanauza. Inatunzwa kama zinavyotunzwa fedha. Inaifanya BOt kuwa na healthy Balance Sheet hivyo kuimarisha thamani ya fedha zetu.
Liangalie hili. Unaweza.