Nani angeweza misimamo hii ya Rais Magufuli?

JOYOPAPASI

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
250
408
NANI ANGEWEZA MISIMAMO HII YA RAIS MAGUFULI?

Na Bwanku M Bwanku

Leo ngoja nizungumze kidogo kuhusu mambo mbalimbali ya taifa letu. Yani leo niwe muwazi kabisa kwenu. Mimi kwa umri wangu huu wa miaka 23 tu nimekutana, kuonana, kusikia na kuwasoma watu mashujaa wengi sana hapa duniani waliopita na wengi tu wa kizazi chetu. Nimesikia na kusoma sana habari za mashujaa wakubwa wa dunia waliopambana kwa ajili ya watu. Akina Martin Luther King Jr, William Sylvester, Malcolm X, William Du Bois, Marcus Garvey na Wamarekani weusi wengi tu mashujaa waliopambana kufa na kupona mpaka wengine kupoteza uhai wao ili kutafuta haki ya mtu mweusi duniani.

Wanaharakati na wanamapinduzi wakubwa wa ukombozi wa bara la Afrika kutoka kwenye uonevu na unyonyaji wa kikoloni. Akina Mwalimu Nyerere, Kwame Nkurumah, Patrice Lumumba, Nelson Mandela ambao waliweka rehani mpaka uhai na maisha yao kwa ajili ya watu wao lakini kutoka moyoni huyu mtu kwangu ni kiboko.

Lakini leo kidogo nitammulika kidogo shujaa na jasiri wa Kiafrika kwasasa. Kwangu Rais Magufuli ni moja ya mashujaa na majasiri wachache sana ambao dunia imewahi kuwashuhudia kwenye zama hizi za kisasa na kibeberu hasa kwa kuangalia mfumo wa kimataifa ulivyo. Kwakweli kama kuna watu sitawasahau kwa ujasiri, misimamo na ushujaa wao hasa linapokuja suala lenye maslahi ya watu wao wengi basi sidhani kama nitapata kumwona mwingine wa kumzidi Rais Magufuli, mtu aliye tayali kwa lolote linapokuja suala la nchi bila kuwa na woga wala kuangalia sura ya yeyote yule.

Hebu fikilia misimamo yake kwenye gonjwa na balaa la Corona tu. Wakati dunia nzima ikiamini na ikihamasishana kufungia watu ndani (Lockdown) kama njia ya kupambana na ugonjwa huo Rais Magufuli yeye alikataa katukatu kuingia kwenye mtego huo wa kuua uchumi na watu. Yeye akahamasisha watu sana kuendelea kuchukua tahadhari zote za Corona na zaidi akalikabidhi taifa kwenye mikono ya Mungu lakini sio kufungia mtu.

Taifa likamtumainia Mungu, Rais Magufuli akahamasisha watu kuomba na kufunga kwa ajili ya taifa kukomboka na Corona na hakuna nyumba ya ibada iliyofungwa. Dunia nzima kuanzia Shirika la Afya duniani (WHO), mataifa ya nje na mpaka majirani zetu wa Afrika wakabeza sana njia tunazotumia kupambana na Corona na wakaanza kuipigia kelele Tanzania kwa namna inavyopambana na Corona lakini bado Rais Magufuli aliendelea kusimamia msimamo wake wa kutofunga mji wowote wala cha Lockdown.

Watu wakaendelea kufanya shughuli zao kwa tahadhari kubwa sana na kufuata taratibu zote. Leo wakati dunia nzima na majirani zetu waliotupigia kelele kwa njia tunazochukua wakiendelea kuteswa na Corona sisi Tanzania Corona imeshakuwa historia na kila mtu anaendelea na shughuli zake. Corona imepotea na imeshaisha. Nani angeweza kuendelea na misimamo ile licha ya kila mtu kubeza huku wengine wakitutabiria kuokota maiti kila sehemu. Leo wapi Tanzania kumeokotwa maiti ya Corona? Wapi Rais huyu alitetereka na kukubaliana na wapiga kelele? Ushujaa wa namna gani huu.

Tuachane na ishu ya Corona twende kwenye msimamo wake kwenye madini. Nadhani tunakumbuka namna sekta ya madini ilivyokuwa kama shamba la bibi kwa kila mtu kuchuma madini ya Tanzania tu bila woga wowote ule. Mfano tu kwenye madini ya Tanzanite ambayo yanapatikana hapa Tanzania tu dunia nzima ila nchi yetu wala haikuwa kwenye orodha ya nchi zinazouza kwa wingi madini hayo duniani. Hapa palithibitisha ushujaa mkubwa wa mtoto huyu wa kweli wa Afrika, Rais Magufuli.

Unalikumbuka sakata la mchanga wa madini la Makinikia kati yetu na Kampuni ya madini ya Acacia. Baada ya ripoti mbili za Prof Mruma na Prof Osoro kuthibitisha wizi mkubwa na wa muda mrefu wa madini kwenye migodi mitatu ya North Mara, Bulyanhuru na Buzwagi, Tanzania tulidai fidia yetu ya kikodi kutoka kwa Acacia. Baada ya ripoti zile majadiliano yakaaza ili kampuni hiyo ilipe fidia zake za kodi. Ghafla tukaanza kutishiwa na Watanzania wenzetu waliosema tusingelipwa fedha hizo na kwamba tungelitafutia matatizo taifa kwa kushindana na mabeberu.

Rais Magufuli akaweka msimamo mkali wa kutaka lazima tulipwe fedha zote licha ya vitisho na hofu tuliyopata kutoka kwa Watanzania wenzetu waliotutisha kwamba tungeshtakiwa na kwamba tusingeshinda kesi hiyo.

Leo misimamo ya Rais Magufuli kwenye madini imelifaidisha taifa na sasa taifa limeshanza kulipwa fedha zote za malimbikizo ya kikodi na Kampuni ile ya Acacia kupitia Barrick. Zaidi Acacia yenyewe iliyohusika kwenye wizi ule wa madini imekufa na Serikali kuunda Kampuni moja ya madini ya Twiga na Barrick kwa kugawana faida sawa ya madini na Tanzania, kuongeza asilimia zake za hisa kwenye Kampuni hiyo mpya mpaka kufikia 16 kutoka 0 na faida nyingine nyingi sana za kiuchumi huku mapato ya sekta ya madini yakipanda kutoka chini ya Billion 170 mwaka 2015 mpaka Billion 470 kwa sasa. Nani angeweza misimamo hii?

Nawaza kwa ujasiri na misimamo hii ya Rais Magufuli kama tungepata walau marais watano kama yeye hapa Afrika tungekuwa wapi? Hivi hawa mabeberu wanaolinyanyasa na kulibagaza bara la Afrika kwa maslahi yao binafsi wangepata upenyo huo kweli?

Vipi kuhusu suala la ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Stiglers Gorge (Bwawa la Mwalimu Nyerere) kule Rufiji. Adhima ya Serikali kujenga bwawa hili la kuzalisha umeme pale hifadhi ya Selous kwenye Mto Rufiji liliibua maneno na minong'ono mingi sana kutoka ndani na nje ya nchi kwa kile kilichodaiwa mradi huo ungeenda kuharibu na kuathiri viumbe hai na binadamu waishio eneo hilo. Mfuko wa mazingira wa kimataifa (WWF) ulipinga vikali mradi huo kwa kudai mradi huo ungesababisha mmonyonyoko mkubwa wa ardhi, kupunguza rutuba ya eneo la Rufiji na mengine mengi sana.

Licha ya yote Rais Magufuli aliendelea kuweka msimamo mkali na kusisitiza kwamba mradi huo ni lazima ujengwe na kutekelezwa kwasababu kukamirika kwake tu kutapunguza gharama ya umeme kwa kiwango kikubwa cha mpaka shilingi 36 kuliko hali ilivyo sasa ambapo umeme wa nyuklia tunalipa shilingi 65 kwa uniti, umeme wa jua 103.05, umeme wa upepo 103.05, makaa ya mawe 118, gesi asilia 147 na mafuta 426 kwa uniti hivyo kupunguza kwa kiwango kikubwa sana bei ya bidhaa za Tanzania.

Rais Magufuli aliusoma mchezo wa mabeberu ambao moja kwa moja walijua ujenzi wa mradi huu wa umeme ungeacha nchi yetu kununua umeme wao ambao ni gharama kubwa sana hivyo wakaanzisha kelele hizo ili kuuzuia usitekelezwe kwasababu moja kwa moja ulikuwa unaweka rehani maslahi yao.

Rais alisimama na msimamo wake wenye maslahi makubwa sana kwa nchi na mradi huo mpaka hapa tunapozungumza mradi unaendelea kujengwa kwa fedha zetu za ndani Trillion 2.6 ambapo zaidi ya megawati 2115 zinaenda kuzalishwa hivyo kumaliza kabisa tatizo la umeme nchini huku kwa kiwango kikubwa nchi ikipunguza ukataji wa miti hovyo kwani kwa mwaka nchi hupoteza miti zaidi ya Million 30 kwa mkaa. Ina maana mradi ule wa Stieglers Gorge unaenda kutupa umeme wa uhakika ambapo moja kwa moja tutapunguza utumiaji wa mkaa na hivyo kulinda mazingira yetu.

Huu ulikuwa msimamo mkubwa sana kwa taifa hasa kipindi hichi ambacho tunataka kujenga uchumi wa viwanda kwahiyo umeme wa uhakika ni muhimu sana.

Misimamo kwa wakandarasi wazembe. toka kuingia madarakani kwa Serikali ya awamu ya 5 Rais alikuwa mkali sana na kuweka misimamo sana kwa wakandarasi wazembe wasiokamilisha miradi mbalimbali ya maji, barabara na majengo kwa wakati na nyakati nyingine chini ya kiwango. Kwa maslahi ya Tanzania, Rais alifikia kuwatimua na kuvunja mikataba na wakandarasi wazembe wanaochelewesha sana miradi ya umma. Hakuna alipoogopa wala kuangalia sura zao wala kuhofu mataifa yao makubwa yenye nguvu ya kila aina.

Hapo hujagusa misimamo kwenye kupambana na mafisadi, wala rushwa, watumishi hewa na wazembe ambao mamia kwa mamia wamechukuliwa hatua ikiwemo kufukuzwa kazi. Jamani nani angeweza haya? Ushujaa gani huu.

0657475347
IMG-20200829-WA0495.jpg
 
Bwaku M Bwaku huwa nakutana naye kwenye magroup ya WhatsApp. Anapenda sana kuandika.

Anyway kwenye hili namuunga mkono. Kule WhatsApp huwa tunamfokea akianza kutangaza magazeti yenye makala zake, si ajabu akatangaza na hii sledi
BWAKU bhana
 
Back
Top Bottom