Leo ndio leo, ni deadline ya Barrick kutangaza kifo cha Acacia kwa neno moja tuu "PUSU" (Put Up or Shut Up). ni kubali ufe, kataa ufe!, no option!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
38,402
2,000
Wanabodi,
Leo ndio leo, asemaye kesho muongo. Leo ndio siku ya mwisho ya deadline ya PUSU ya Barrick kwa Acacia, PUSU ni "Put Up or Shut Up", yaani kubali ufe, kataa ufe!.

Kati ya vifo vyote vya biashara, kifo kibaya kabisa ninaitwa "hostile take over", ambapo biashara inakabwa koo kwa kunyongwa hadi kufa bila kutaka kwa kuuzwa juu kwa juu. Kifo hiki ndicho kinakwenda kuikuta kampuni ya Acacia, ambapo leo ndio siku ya mwisho kwa Barrick kutoa tangazo la kifo cha Acacia kwa kutangaza offer ya mwisho kuinunua Acacia, Acacia lazima ikubali, ife kifo cha heshima kwa kupata chochote, ikikataa, inakufa kifo cha lazima kwa kukosa yote.

Chronology of events ni kama ifuatavyo.

Mgogoro wa Baba na Mtoto, alianza kama ifuatavyo
 1. Rais Magufuli alisimamisha kusafirisha mchanga wa makinikia ya dhahabu baada ya kuhisi tunaibiwa.
 2. Akaunda tume mbili, zikathibisha ni kweli tunaibiwa, TRA wakapiga hesabu ya tulichoibiwa, bili ikaja tunawadai Dola bilioni 190, fedha inayotosha kumnunulia kila Mtanzania gari aina ya Noah.
 3. Baba wa Acacia, Barrick akaingilia kati, tukafanya mazungumzo, yalipofika katikati, Barrick akaahidi kutulipa kishika uchumba cha dola milioni 300, wakati tukijadiliana jinsi ya kulipa mahari kamili ya ile dola bilioni 190.
 4. Mazungumzo yalipofika mwisho, serikali yetu ikaamua kwa nia njema kabisa, kuwasamehe Acacia lile deni kubwa la bilioni 190, na badala yake, sasa tutalipwa kifuta machozi cha kile kishika uchumba cha dola milioni 300.
 5. Acacia itavunjwa na kuundwa kampuni mpya ya ubia, na Tanzania, ambapo tutamiliki hisa za asilimia 16%
 6. Tutagawana manufaa ya kiuchumi pasu kwa pasu, 50/50.
 7. Kabla Acacia hajapelekewa mapendekezo haya, Serikali ikaziandikia barua migodi mitatu ya Acacia kuwa haiitambui Acacia, hivyo kuokoa jahazi, Barrick akaonyesha nia ya kuinunua Acacia kwa fedha kiduchu, kwa kuwagaiya wanahisa wote wa Acacia hisa za Barrick.
 8. Acacia akagoma kununuliwa kwa bei kiduchu, hivyo Barrick wakaomba muda zaidi kabla hawajatoa bei ya mwisho, Acacia akakubali kuipa muda zaidi Barrick wapandishe dau.
 9. Barrick, akamwaga ugali hadharani kuwa wametoa dau dogo kwa sababu Acacia haina thamani kivile, na bado ni very risk.
 10. Baada ya Barrick kumwaga ugali, Acacia akakasirika, na yeye akamwaga mboga, kwa kujionyeshea ana thamani kubwa sana hivyo Barrick lazima aongeze dau.
 11. Ndipo leo Barrick kajibu mapigo kuwa hakuna kipya chochote Acacia alichokisema, hawataongeza hata senti tano.
 12. Tarehe ya mwisho ya PUSU ya Barrick kutoa offer rasmi ni leo tarehe 9 Julai.
 13. Acacia sasa kufa rasmi, Barrick itaimiliki Acacia asilimia 100/100
 14. Kazi ya kwanza baada ya kifo cha Acacia, ni yale Makubaliano ya serikali yetu na Barrick kusainiwa
 15. Baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, Barrick watatupatia kile kifuta machozi cha dola milioni 300, kutufuta machozi ya zile dola bilioni 190 zetu za Noah zetu tulizowasamehe.
 16. Barrick wataunda kampuni mpya kuchukua nafasi ya Acacia ambapo makao makuu ya kampuni hiyo yatakuwa Tanzania, na sio London.
 17. Tanzania tutakuwa na shares 16% kwenye kampuni hiyo mpya.
 18. Bodi ya kampuni hiyo mpya itakuwa na Watanzania.
 19. Menejimenti ya kampuni hiyo itakuwa na Watanzania.
 20. Tutagawana manufaa ya kiuchumi 50/50 na kwa mara ya kwanza, ndio Tanzania tutaanza kufaidi rasilimali dhahabu yetu.
Kilichopelekea haya
Uamuzi huu wa Barrick kuinunua Acacia, ni kufuatia Serikali Yetu, Kuwatosa rasmi Acacia Kwa kuandika barua rasmi za kutowatambua, kutakakopelekea kifo rasmi cha Acacia, Huu Ndio Uanaume!. Haiwezekani madini yetu, Tanzania inazungumza na Baba Mtu, Barrick, halafu wewe mtoto tuu, Acacia kila siku ni kuleta nyodo. Sasa Acacia Itakula Jeuri Yake, it Faces a Hostile Take Over from Barrick, and Soon Itakuwa Kwishney!. A thing of the past, a history!.

Mpaka hapa ninapoandika, serikali yetu bado haijatoa taarifa rasmi kwetu sisi Watanzania, hatua hii ni long overdue, hivyo kama ni kweli, serikali yetu did the right thing kwa sababu situation ya Acacia ni hii

Historical Background
Tangu kutokea mgogoro wa makinikia ya Acacia, kwanza sisi wazalendo wa kweli wa taifa hili, tulipongeza hatua ya rais Magufuli kuuzuia mchanga wa makinikia Kuzuia Mchanga wa Dhahabu, Magufuli Anastahili Pongezi. Tusiishie ...

Baada ya kuzuiliwa kwa mchanga, Rais Magufuli akaunda Tume zake mbili, zikamletea ripoti zake mbili, baada ya kushuhudia live presentation ya tume ya pili, nilitoa opinion yangu Sensationalism kwenye Professional Presentations inakubalika? Ni ...

Ripoti za tume hizo zikaosnyesha kuwa siku zote, tumekuwa tukiibiwa, TRA wakaja na bili ya ajabu ya deni ya Dola Bilioni 190 US $ sawa na TZS 424 trilioni kwa fedha za madafu, kuhusu deni hili, sisi wachumi wa Sultani Mangungo wa Msovero ya JF, tukamweleza rais wetu kuwa anadanganywa na kumsihi asidanganyike.
Maendeleo ya kweli TZ Yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye ...

Baada ya deni hilo kuwekwa wazi, Acacia wakatugomea kuwa hawadaiwi na hawalipi. Baba wa Acacia, Barrick akaingilia kati kwa Mwenyekiti wao kuja nchini kuonana na rais Magufuli na kukubali kuwa watalipa, hivyo mazungumzo yakaanza.

Maungumzo yakaisha rasmi na tukatangaziwa makubaliano, kikiwemo sisi kulipwa dola milioni 300 za kuonyeshea nia njema ya kulipa. Katika makubaliano hayo Barrick alionyesha kuwa makubaliano hayo yatatekelezwa baada ya kukubali na Acacia.

Acacia kwanza akatoa taarifa kuwa hayatambui makubaliano hayo kwa vile hakushirikishwa, Hivi Hawa Acacia Wana Adabu Kweli?, Baba Akiishasema Kitu, Mtoto ...lakini siku chache baadae akatoa taarifa ya kukubali kila kitu.
Habari Njema Kutoka Acacia: Wakubali Kila Kitu Ikiwemo Kulipa ...

Sisi wahojaji tukaendelea kuhoji sio tuu uwezo wa Acacia kulipa deni letu la dola bilioni 190, bali hata uwezo Acacia kulipa tuu hata hizo dola milioni 300 za goodwill. Dola milioni 300, siku 90, sentano kipande haijalipwa! acacia ...
Pia tukahoji, kama Acacia ndio determinant wa kutulipa, kwa nini hakushirikishwa kwenye mazungumzo?. Je, wajua kuwa mazungumzo yetu na Barrick ni mazungumzo tu? Mwenye ...

Mapendekezo ya makubaliano ya mwisho yalitolewa na Barrick kuwa sasa Acacia watalipa ile dola milioni 300 tuu na deni lote la dola bilioni 190, tukasamehe, Acacia akaibuka na kuikana Barick kuwa wao hawajui chochote kwa vile hawakushirikishwa, hivyo wanasubiri taarifa rami ya Barrick ndipo watangaze uamuzi. Acacia Yaikana Barrick Mchana Kweupe!. Yatoa Press Release na ...

Acacia wakaibuka kuwa bado hawajapewa makubaliano. Kwanini Mapendekezo ya Makubaliano yetu na Barrick bado hayajafika ...

Siku ya Jumapili, tarehe 19th May 2019, serikali yetu ikafunga kazi!, licha ya kuwa ni Jumapili, sio siku ya kazi, huwezi kuandika barua za kiserikali siku ya Jumapili, lakini kwa serikali ya Magufuli ya Hapa Kazi Tuu, hakuna cha Jumapili wala sikukuu, ni kazi tuu, ikitokea kazi ya urgency kama hizi barua za kutoitambua Acacia, serikali yetu inaingia kazini, Jumapili ya juzi, serikali imeingia kazini, imeziandikia barua migodi ya Bulyanhulu Gold Mine Limited, North Mara Gold Mine Limited na Pangea Minerals Limited, kuwaeleza kuwa hawaitambui Acacia, hali iliyoilazimu Barrick kutoa offer ya hostile take over kwa Acacia kuzinunua hisa zote za Acacia, ambazo hazimilikiwa na Barrick, itake isitake, hivyo kuimeza rasmi Acacia kuwa sehemu ya Barrick. na wana hisa wote wa Acacia wamepewa offer ya kuwa wanahisa wa Barrick. Kwa Tanzania Hostile take over iliwahi kutokea kwa kiwanda cha Bia cha Kibo kule Moshi. Tofauti ya hostile take over ile na hii, migodi ya Bulyanhulu Gold Mine Limited, North Mara Gold Mine Limited na Pangea Minerals Limited, itaendelea kuwepo, hakuna atakayepoteza kazi na uzalishaji unaendelea, kitakachokufa ni Acacia tuu, ambayo ni kampuni ya uendeshaji tuu, yaani a management tuu, nafasi yake inachukuliwa na Barrick, everything else stays the same.

Kitendo hiki kilichofanywa na serikali yetu kui disown Acacia ni kitendo cha kishujaa sana na huu ndio uanamme. Haiwezekani madini yetu, mtu anayetambulika nchini kama ni mmiliki ni Barrick kupitia Bulyanhulu Gold Mine Limited, North Mara Gold Mine Limited na Pangea Minerals Limited, huyu Acacia ni mtu wa kuja tuu, hatambuliwi halafu analeta nyodo kibao.

Japo Acacia ni mtoto wa Barrick, huyu ni mwana mkaidi, kama kawaida ya mwana mkaidi hafaidi mpaka siku ya iddi, hivyo siku ya Iddi ya Acacia imewadia. Funzo tunalolipata hapa ni siku zote
kiburi sii maungwana. Acacia alikuwa jeuri, sasa anakula jeuri yake, soon Acacia itabaki kuwa ni historia, kwishney ila naomba kutoa angalizo muhimu kwa serikali yetu, hii saga yote ya Acacia na Barrick, mara kimepanda, mara kimeshuka, its all a game that people play. Hawa ni baba na mwana, na huu ni mchezo tunachezewa, the bottom line ni lile deni letu la kodi kutoka US$190 bilioni hadi just $300milioni, this is peanut, ila tukiamua kuiita ndio a win win situation for the sake ya uzalendo kwa uwezo wa viongozi wetu ku negotiate, then Watanzania tutawakubalia, na kujifunza somo kuwa kuwa, timu kuwa na wanasheria nguli tuu peke yake bila watu ambao ni negotiators, hakutoshi. Hapa tunapigwa mchana kweupe huku tunajiangalia.

Conclusion.
Leo Watanzania tukae mkao wa kula kusubiria Tangazo la mwisho la PUSU kwa Acacia kutoka kwa Barrick kuinunua Acacia na kuifungasha virago, sasa Tanzania tuanze kufaidi rasilimali zetu.

Paskali.
Update
Acacia na Barrick bado wanavutana,
PUSU deadline ya leo imefutwa, Acacia wametoa taarifa kwenye tovuti yao kuwa Barrick wameomba kuongezewa muda wa deadline nyingine ya PUSU kwa
siku 10 zaidi, hivyo Acacia wamekubali kuongezwa huo muda hivyo sasa hii ngoma itakuwa Tarehe 19/07/2019 5:00pm kwa saa za London.


Barrick nao wametoa taarifa hapa

P.
 

cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
25,192
2,000
Umefanya vizuri kutukumbusha tulipotoka na sakata hili.. naamini kuna watu wapo wanalia maana na wafata upepo wa humu wasiojua kufikiria eeeeh... wameumbuka kuona hao Acacia yao yamefika hapa.
 

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
3,980
2,000
Tusidanganyane wewe, watu wote wanaishi Canada na wote ni matajiri. Unafikiri umemsokota mmoja ili agombane na mwingine?
Huo ni ujuha!
Umefanya vizuri kutukumbusha tulipotoka na sakata hili.. naamini kuna watu wapo wanalia maana na wafata upepo wa humu wasiojua kufikiria eeeeh... wameumbuka kuona hao Acacia yao yamefika hapa.
 

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
15,128
2,000
Umefanya vizuri kutukumbusha tulipotoka na sakata hili.. naamini kuna watu wapo wanalia maana na wafata upepo wa humu wasiojua kufikiria eeeeh... wameumbuka kuona hao Acacia yao yamefika hapa.
Inaelekea zile milioni 50 za kila kijiji, za kijijini kwenu ulipewa wewe ugaie wenzako...choko channel inapatikana king'amuzi kipi?
 

flulanga

JF-Expert Member
Jul 1, 2016
4,567
2,000
Ningependa kujua Barrick walitaka wawape dau kiasi gani acacia, ili nifananishe nahicho kifuta machozi ambacho Barrick watatupa ambacho tulistahili kupewa na acacia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom