Rais Magufuli umesahau kabisa uwekezaji kwenye kilimo cha kisasa

Unaanzaje kupeleka fedha zaidi eneo ambalo pembejeo zililiwa na mchwa watu?
Pambana na mchwa watu kwanza ndio upeleke fedha ya miradi mikubwa.
by the way ni dhambi sana kuongelea kilimo cha umwagiliaji ilihali tunashindwa kutumia mvua na mafuriko ya Mungu kulima ...tusitafute mikakati na miradi mikubwa kama tunaishi jangwani tutumie baraka ya Mwenyezi Mungu kuzalisha bidhaa za kilimo.

Tuache uvivu tufanye kazi...mimi mwaka huu lazima nivune!!
True!
Wenyeji ni shida kubwa, yaani kuna kazi haswa ya kuwaelimisha.
Mola tusaidie kwa kweli
 
Waisraeli wanakuja kuwekeza kilimo kikubwa cha kisasa.

Wewe ni kiazi kwaiyoo serekali ikae isifanye kitu isubiri waisraeli?
Ata waisrael wakija hawatalima zaidi ya ekari 1000. Wakati ekar 1000 mkiungana watu wawili mnalima. Tuna ongelea kilimo wewe bwana mdogo acha kukalia akili.
 
Nchi yetu ni maskini, na tunayo mambo mengi muno ya kufanya na yote ni ya muhimu sana, lakini hatuna uwezo wa kuyafanya ypote kwa wakati mmoja na hivyo lazima tuchague na tupange tunaanza na lipi. Unless kama hoja yako ni kuwa unashauri tulitakiwa tuanze na kilimo cha kisasa, ila tu ninachojaribu kusema hapa ni kuwa tuseme kwa mfano tungeanza na kilimo bora, kuna kitu kingine muhimu ambacho kwa sasa kinafanyika, kisingeweza kufanyika. Hatuna uwezo huo wa kuvichukua vitu vyote kwa pamoja, lazima tufanye baadhi na tukishakamilisha hivyo tunavyofanya kwa muda huu, tunaanza vingine tena.
Pesa inayotumika kwa mambo ya hovyo hovyo, kuwanunua wabunge, madiwani kurudia chaguzi kwa gharama kubwa, uchakachuaji, kuwabambikia kesi, kuwapiga Risasi, kuwafunga jela Wapinzani, kujenga Chato Airport, 10% ununuzi wa ndege na 10% kuikomboa ndege Canada ni pesa nyingi sana, ni pesa ambazo zingeweza kuendeleza kilimo na Tanzania ikiweza kulisha Afrika nzima na chakula kikabaki kingi na kugawa bure kwa masikini, kikundi cha wasiojulikana cha Naibu Rais Maliyamungu Bashite peke yake kinakula mabilioni ni pesa ambayo ingeweza kuyafufua yale mashamba makubwa yaliyokuwa yakimilikiwa na serikali ambayo mengi ni mapori na mengine yamevamiwa na wananchi wamejenga nyumba.
 
Pesa zote za kuendekeza kilimo zimepelekwa kwa wasiojulikana ili kudhoofisha chadema na kuua CUF na kurejesha mfumo wa chama kimoja.
 
Kuitenga wizara ya kilimo katika kuitengea bajeti finyu ya bilion 170 wakati unasisitiza Tanzania ya viwanda hiyo ni ndoto kwani malighafi yanatoka wapi? Kama sio shambani labda kama mnataka kujenga viwanda visivyo kuwa na malighafi endelevu kutoka shambani.kwa bajeti hii tujiandae viwanda kuwa white elephant
 
Pesa inayotumika kwa mambo ya hovyo hovyo, kuwanunua wabunge, madiwani kurudia chaguzi kwa gharama kubwa, uchakachuaji, kuwabambikia kesi, kuwapiga Risasi, kuwafunga jela Wapinzani, kujenga Chato Airport, 10% ununuzi wa ndege na 10% kuikomboa ndege Canada ni pesa nyingi sana, ni pesa ambazo zingeweza kuendeleza kilimo na Tanzania ikiweza kulisha Afrika nzima na chakula kikabaki kingi na kugawa bure kwa masikini, kikundi cha wasiojulikana cha Naibu Rais Maliyamungu Bashite peke yake kinakula mabilioni ni pesa ambayo ingeweza kuyafufua yale mashamba makubwa yaliyokuwa yakimilikiwa na serikali ambayo mengi ni mapori na mengine yamevamiwa na wananchi wamejenga nyumba.
Mimi sasa haya mengine unayoyasema hapa nilikuwa siyajui au nayasikia tu kama tetesi, na siwezi ku-relie on tetesi!. Nyie sasa watu wa intelijensia ndiyo munaoweza kutuhakikishia sisi wengine, ila mimi siyajui na sijui kama serikali wenyewe wameshakiri kwamba yako kama vile wewe unavyodai. Je, una uhakika gani kwamba haya unayoyasema ni kweli yanafanyika kama vile unavyodai wewe? Unaweza ku-prove kwamba yako vile kama unavyodai?
 
Rais Magufuli umekuwa makini sana katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na miundombinu bora kabisa ya barabara,madaraja,reli ya kisasa,bandari,ndege kwa hilo unastahili pongezi kwasababu maendeleo ya kweli lazima uwe na miundombinu bora na ya uhakika.

Huduma za afya zinaenda vizuri lakini masuala ya vifaa vya kisasa bado ni mtihani mkubwa kwenye vituo vingi vya huduma.

Huduma za elimu inakwenda vizuri lakini vitendea kazi bora kwa walimu nalo ni tatizo kubwa sana

Suala la kilimo kiukweli naona kama umelisahau Mh Rais pamoja na kuhimiza watu kufanya kazi au kulima lakini kiukweli hakuna hatua yoyote inayopigwa ili kupata tunachotakiwa kupata kutoka kwenye sekta ya kilimo.

Kwanza kabisa uwekezaji katika mbegu bora huoni mikakati ya kweli,Uwekezaji katika kilimo cha umwagiliaji ambacho mataifa mengi wanakitumia kwa hapa nchini huoni mikakati yoyote katika kuanisha mashamba makubwa ya umwagiliaji.

Namna gani tunaboresha kilimo kwa wakulima wadogo wadogo yaani wananchi wa kawaida kuhusu pembejeo za kisasa,mbegu bora elimu kwa wakulima huoni mikakati zaidi ya kuhumiza tu watu walime.

Matokeo yake kilimo kimekuwa cha kubahatisha tu na mvua isiponyesha kwa uhakika basi baa la njaa linakuwa kubwa na kuanza kuomba chakula nje.

Mazao ya biashara ambayo ndiyo malighafi kwenye viwanda huoni mikakati yake kiasi ambacho tungeondokana na kuagiza raw materials nje ya nchi ili kuvifanya viwanda nchini viweze kuzalisha kwa uhakika na gharama ndogo.

Ushauri wangu tuna wataalam wa kutosha kabisa wa kilimo tunaowapika pale SUA Morogoro lakini maajabu ya nchi yetu hatuwatumii katika mikakati ya kitaifa ya kuboresha kilimo nchi.

'Tumekuwa wazuri sana wa kuwa mipango kwenye makaratasi kuliko utendaji kwa vitendo'
Kilimo ni mufilisi kabisa mkuu.Kwa mfano mwaka huu Maize Stalk Borers wametu-terorize sana wakulima,lakini nikiri kwamba mabwana shamba/mabibi shamba hawakutoa msaada tangible
kwetu.Nadhani nao sijui ni vihiyo kwa hiyo hawajui wajibu wao!?Hivi ile sera ya kilimo ni uti wa mgongo ili endaga wapi?It was so appropriate.

Frankly we need to allocate enough resources for the development of the agricultural sector,vinginevyo watu wetu watazidi kuwa maskini. Lakini as you have rightly said,we are extremely good in devising good plans,implementation capacity zero.Hivi wataalam wetu given enough resources wanashindwa kuzalisha mbegu zinazostahimili mashambulizi ya Maize Stalk Borers kwa mfano kweli?Jamani tuwe serious kidogo.
 
Nadhani siasa zetu zisizo na mbele wala nyuma zinatuangusha ...kila jambo tumeingiza siasa badala ya utekelezaji wa kitaalamu.

Just imagine leo Mkuu wa Majeshi anamlalamikia Mh Rais kuwa SUMA JKT wanadai Taasisi binafsi bilion 40 na Taasisi za serikali bilion 3.5 unafikiri hiyo SUMA JKT itaendelea au itakufa tu.Na nakumbuka madeni hayo ni wakatu ule Dr Kikwete ameleta power tillers na matrekta na watu wakakopeshwa lakini ndo hivyo hawajalipa madeni what do you expect
 
Tupo kwenye sera ya viwanda kwanza...

Tunaboresha mazingira ya upatikanaji wa vyuma vya kujengea viwanda, mengine baadae...

Cc: mahondaw
 
Nadhani siasa zetu zisizo na mbele wala nyuma zinatuangusha ...kila jambo tumeingiza siasa badala ya utekelezaji wa kitaalamu.

Just imagine leo Mkuu wa Majeshi anamlalamikia Mh Rais kuwa SUMA JKT wanadai Taasisi binafsi bilion 40 na Taasisi za serikali bilion 3.5 unafikiri hiyo SUMA JKT itaendelea au itakufa tu.Na nakumbuka madeni hayo ni wakatu ule Dr Kikwete ameleta power tillers na matrekta na watu wakakopeshwa lakini ndo hivyo hawajalipa madeni what do you expect
Na usikute waliokopa ni watumishi wa ngazi za juu serikalini kama ilivyokuwa Twiga Bank,ndio maana wanapata kigugumizi kuyafuatilia.Shame on us.Maana baada ya kusikia hili sakata, nimejiuliza,lakini kwa nini deni liwe kubwa kiasi hiki?Na kwa nini lisilipwe?
 
Back
Top Bottom