tatum
JF-Expert Member
- Jan 16, 2018
- 5,786
- 4,490
Rais Magufuli umekuwa makini sana katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na miundombinu bora kabisa ya barabara,madaraja,reli ya kisasa,bandari,ndege kwa hilo unastahili pongezi kwasababu maendeleo ya kweli lazima uwe na miundombinu bora na ya uhakika.
Huduma za afya zinaenda vizuri lakini masuala ya vifaa vya kisasa bado ni mtihani mkubwa kwenye vituo vingi vya huduma.
Huduma za elimu inakwenda vizuri lakini vitendea kazi bora kwa walimu nalo ni tatizo kubwa sana
Suala la kilimo kiukweli naona kama umelisahau Mh Rais pamoja na kuhimiza watu kufanya kazi au kulima lakini kiukweli hakuna hatua yoyote inayopigwa ili kupata tunachotakiwa kupata kutoka kwenye sekta ya kilimo.
Kwanza kabisa uwekezaji katika mbegu bora huoni mikakati ya kweli,Uwekezaji katika kilimo cha umwagiliaji ambacho mataifa mengi wanakitumia kwa hapa nchini huoni mikakati yoyote katika kuanisha mashamba makubwa ya umwagiliaji.
Namna gani tunaboresha kilimo kwa wakulima wadogo wadogo yaani wananchi wa kawaida kuhusu pembejeo za kisasa,mbegu bora elimu kwa wakulima huoni mikakati zaidi ya kuhumiza tu watu walime.
Matokeo yake kilimo kimekuwa cha kubahatisha tu na mvua isiponyesha kwa uhakika basi baa la njaa linakuwa kubwa na kuanza kuomba chakula nje.
Mazao ya biashara ambayo ndiyo malighafi kwenye viwanda huoni mikakati yake kiasi ambacho tungeondokana na kuagiza raw materials nje ya nchi ili kuvifanya viwanda nchini viweze kuzalisha kwa uhakika na gharama ndogo.
Ushauri wangu tuna wataalam wa kutosha kabisa wa kilimo tunaowapika pale SUA Morogoro lakini maajabu ya nchi yetu hatuwatumii katika mikakati ya kitaifa ya kuboresha kilimo nchi.
'Tumekuwa wazuri sana wa kuwa mipango kwenye makaratasi kuliko utendaji kwa vitendo'