Ki Mun
JF-Expert Member
- Oct 6, 2014
- 3,443
- 4,386
Kuna mchungaji wangu mmoja siku moja katika mahubiri kanisani aliwakemea watu wenye tabia ya kutafuna "Big G" wakati wa ibada kanisani na baadaye kutema uchafu wao huo sakafuni au kwenye viti kwamba tabia yao hiyo ilimaanisha "KUKOSA KUJIAMINI". Ni miaka mingi sana na tangu wakati huo nimelielewa neno KUJIAMINI kwa namna ya tofauti sana!
Kwamba KUJIAMINI kunamaanisha kutokutenda jambo lolote kinyume na matajirio ya wengi, kwamba kujiamini hakumaanishi kutokuwa mwoga, hakumaanishi kuwa mtu wa mashindano, mbishani, mkaidi, jeuri, mnyanyasaji, mbabe na kuwa mtu asiyejali hisia ama maumivu ya watu wengine. Kujiamini kunamaanisha kinyume ya haya!!!
Sasa sisi tuanendelea kutoa tu rai kwa kiongozi wetu Rais Magufuli kwamba anaposema anajiamini basi awe anamaanisha kuwa yeye ni kiongozi mwadilifu, mwenye kutenda kwa haki, mwingi wa maarifa, upendo na mwenye kuwajaza matumaini watu wake. Kinyume na hivi ni kujitafutia anguko lisilokusudiwa, na kushindwa kunakoepukika
Mungu ibariki Tanzania