Rais Magufuli, this is serious. Tafadhali usiruhusu hili!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Mhe. Rais,nina ujumbe mfupi tu kwako. Tafadhali usiruhusu Serikali yako kuwa ya visasi,kuchongeana na 'kucheza na jukwaa'. Pale ambapo watumishi wa umma watapaswa kushughulikiwa,Sheria za Utumishi wa Umma na zile za Ajira zisiwekwe kando na hasira,malengo na uharaka wa kutumbua majipu.

Utumbuaji wa aina ya wa Wilson Kabwe unatweza na kuchora picha ya visasi na kuchongeana. Watumishi wa umma wapewe nafasi kujieleza kabla ya kushughulikiwa. Kwa hali inayoendelea,it is serious and the country is heading to unpleasant situation.

Watumbuliwaji nao wanastahili staha na faragha! Kwanini heshima ilindwe kwa watumishi wa BOT tu?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
NAUNGA MKONO KABWE KUTUMBULIWA.

By Malisa GJ,

Kwa mijibu wa RC Paul C. Makonda, Wilson Kabwe alisainisha mikataba miwili kwa wamiliki wa mabasi kwa sheria mbili tofauti (ya mwaka 2004 na 2006). ByLaw ya 2004 inataka bus likitoka Ubungo lilipe Sh.4,000/= na ya 2006 inataka bus lilipe Sh.8,000/=.

Wamiliki wa mabasi walisainishwa kulipa 8,000/= lakini jiji likarekodi kuwa wanalipa Sh.4,000/=. Maana yake ni kuwa kila bus lilikua likilipa Sh.8,000/=, lakini zilizokua zikiingia Halmashauri ya jiji ni Sh.4,000/= tu. Nyingine ziliingia mfukoni kwa Kabwe.

Kwahiyo katika magari 400 yanayotoka Ubungo kwa siku Kabwe alikua anaingiza 1,600,000/= kila siku mfukoni mwake. Hizi ni sawa na Milioni 48 kwa mwezi. Sawa na milioni 576 kwa mwaka.

Hii ni moja ya tuhuma kadhaa alizozieleza Makonda. Kwa kifupi Kabwe ni mpiga dili. Hata kule Mwanza alipiga dili nyingi akawa analindwa na "mkwere".. Kupitia dili hizo alijenga vitega uchumi kadhaa ikiwemo Hoteli ya kifahari ya "Royal Sunset Beach" kule Luchelele.

Hebu jiulize kama kwenye dili moja tu ya mabasi Ubungo anatengeneza Milioni 576 kwa mwaka, ukijumlisha na hizo dili nyingine ana earn kiasi gani? Ni ajabu kama tutamtetea mtu mwenye tuhuma kama hizi.

Yani wakati wewe una mwaka wa 4 unatafuta kazi bila mafanikio hata nauli ya kutembeza CV yako huna, mwenzio anaingiza Milioni 500+ kwa mwaka kupitia dili moja tu. Hakika utakua "zwazwa wa shahada ya juu ya uzamivu (PhD)" kama utamtetea.

Najua kuna "principle of natural justice" lakini hizi natural justice ndio zimetuharibia nchi na kutufikisha hapa tulipo. Mtu anaiba hela halafu anaundiwa Tume imchunguze na tume inalipwa tena hela. No. Si sawa.!

Naunga mkono Maamuzi ya Rais Magufuli kumuweka kando huyu Mkurugenzi mwenye tuhuma lukuki. Tangu akiwa jiji la Mbeya, Mwanza na hatimaye Dar amekuwa akituhumiwa tu.

Ezekia Wenje amewahi kumlalamikia bungeni, Kiwia amewahi kumlalamikia bungeni, viongozi na wananchi kibao wamewahi kumlalamikia lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi yake. Leo kaambiwa akae pembeni kupisha uchunguzi mnamtetea? Mtakuwa mmelogwa walahi.!

Kwanini atuhumiwe yeye tu? Haiwezekani watu wote wamchukie yeye tu.

Makonda kafanya jambo la msingi sana leo kuliko wakati mwingine wowote ktk historia yake. Katetea machozi ya wanyonge. Kakatisha dili za watawala kujishibisha kwa kutumia migongo ya maskini.

Mkumbuke huyu Kabwe ndiye aliyemvua Uraia Ezekiah Wenje mwaka 2010 kwenye uchaguzi mkuu ili Lawrence Masha apite bila kupingwa. Akasema Wwnje ni raia wa Kenya. Ktk kutetea haki yake Wenje akapeleleka malalamiko yake Makao makuu ya NEC na baada ya kupitia vielelezo wakadhibitisha Wenje ni raia. Sasa mtu wa aina hii bado mnamtetea?

Alipokua Mbeya alituhumiwa akahamishiwa Mwanza. Alipokuwa Mwanza alituhumiwa akahamishiwa Dar. Akiwa Dar ametuhumiwa, sasa mnataka ahamishwe tena? Eti principle of Natural justice. Sasa mnataka natural justice kwny tuhuma zilizo wazi?

Hata hivyo tujiulize Kabwe ni kweli Kabwe hajapewa haki ya kusikilizwa as per principle of Natural Justice?? Wanaojenga hoja hii labda hawaelewi vizuri maana ya Natural Justice.

Napenda kuwakumbusha kuwa Kabwe hajahukumiwa bado. Amewekwa kando kupisha uchunguzi. Kuhusu nafasi ya kujitetea ataitwa na kuhojiwa adhering na abtapewa hiyo haki ya "natura justice" mnayoitaka.

Alichokifanya Rais ni kumpumzisha Kabwe ili ahojiwe akiwa nje ya nafasi yake. Akichunguzwa akiwa bado kwny kiti cha ukurugenzi ataathiri uchunguzi. Kwahiyo ni vema akae pembeni kwanza ili achunguzwe vizuri kwa uhuru. Atendewe haki.!

Lakini im very sure hawezi kupona. Hii ndio byebye.!

Nimeichukua kwa (Malisa GJ.!)
 
Tatizo nini kwani?
Ina maana hujamuelewa? Pamoja na kumuunga mkono JPM kuwawajibisha wabadhirifu na wazembe, njia inayotumika kwa sasa siyo sahihi kabisa. Hakuna malaika duniani,sote tu wakosaji. Sheria ichukue mkondo wake. Sijui familia ya Kabwe leo itajisikiaje leo. Siyo vizuri kuona mwingine akipata kadhia tena kwenye kadamnasi.
 
Mkuu JPM hanaga na haelewi kuwa kuna mamlaka za utumishi kanuni na sheria husika. Kweli mmetuletea mchapa kazi, lakini mngempa stadi za uongozi kwa sababu za utendaji tayari anazo. Kumbukeni nchi inaongozwa na maono yanayoelekeza utendaji. Nchini kwetu kwa sasa nchi inaongozwa na utendaji usio na maono.

Kama ulivyosema huko tunakoelekea hakueleweki; ni mshike mshike jahazi kuzama. Tulipoyasema haya hamkutaka kutusikiliza, ila sisi tutaendelea kuwa wananchi watiifu hatutaki vurugu ingawa tunavurugwa.
 
Ina maana hujamuelewa? Pamoja na kumuunga mkono JPM kuwawajibisha wabadhirifu na wazembe, njia inayotumika kwa sasa siyo sahihi kabisa. Hakuna malaika duniani,sote tu wakosaji. Sheria ichukue mkondo wake. Sijui familia ya Kabwe leo itajisikiaje leo. Siyo vizuri kuona mwingine akipata kadhia tena kwenye kadamnasi.
Kuna muda huwa sikuelewi hasa unasimamia kitu gani......
 
Ile level iliyofanyika pale Is too low friends,yaani yule makonda alipoanza kujieleza nilizima TV ni aibu jamani ebu tuendehe nchi kwenye level nyingine bwana
 
Ina maana hujamuelewa? Pamoja na kumuunga mkono JPM kuwawajibisha wabadhirifu na wazembe, njia inayotumika kwa sasa siyo sahihi kabisa. Hakuna malaika duniani,sote tu wakosaji. Sheria ichukue mkondo wake. Sijui familia ya Kabwe leo itajisikiaje leo. Siyo vizuri kuona mwingine akipata kadhia tena kwenye kadamnasi.

Hiyo familia walikuwa wanajisikiaje wakiwa wanakula hizo hela kwani? Tuache mzaha. Kipindi cha mtu kuiba na kuchekewa kimekwisha. Tufike sehemu tuone na kukubali kwamba Cheo in dhamana. Kwanza arudishe hiyo peas ya wananchi. It is so disguisting. Watu wanaaminiwa na kupewa madaraka wanafanya project kujitajirisha. Haikubaliki.
 
Asilolijiua ni kuwa atawafanya hata wale waliokuwa hawaamini kuwa anafanya haya kwa sifa nao waanze kuamini.Kuna ulazima gani wa kumsimamisha mtu kazi mbele ya Akadamnasi kama ile?

Fukuza/simamisha watu kazi lakini usipende kufanya hivyo kila wakati ukiwa mbele ya camera.
 
Mhe. Rais,nina ujumbe mfupi tu kwako. Tafadhali usiruhusu Serikali yako kuwa ya visasi,kuchongeana na 'kucheza na jukwaa'. Pale ambapo watumishi wa umma watapaswa kushughulikiwa,Sheria za Utumishi wa Umma na zile za Ajira zisiwekwe kando na hasira,malengo na uharaka wa kutumbua majipu.

Utumbuaji wa aina ya wa Wilson Kabwe unatweza na kuchora picha ya visasi na kuchongeana. Watumishi wa umma wapewe nafasi kujieleza kabla ya kushughulikiwa. Kwa hali inayoendelea,it is serious and the country is heading to unpleasant situation.

Watumbuliwaji nao wanastahili staha na faragha! Kwanini heshima ilindwe kwa watumishi wa BOT tu?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

chief Tupax2... umesahau falsafa ya mkulu wetu ni ile ya "shoot first and apologise later"?
 
Hiyo familia walikuwa wanajisikiaje wakiwa wanakula hizo hela kwani? Tuache mzaha. Kipindi cha mtu kuiba na kuchekewa kimekwisha. Tufike sehemu tuone na kukubali kwamba Cheo in dhamana. Kwanza arudishe hiyo peas ya wananchi. It is so disguisting. Watu wanaaminiwa na kupewa madaraka wanafanya project kujitajirisha. Haikubaliki.
Hayo wewe si umeyasikia tu, unaushahidi familia ilikula hela? Hadi uchunguzi useme, kwa sasa kasimamishwa, lakini ingetosha kusimamishwa kwa utaratibu wa kawaida kwa kuita press, na siyo kwenye watu wengi, unaweza kuua mtu kwa shinikizo, jambo ambalo siyo zuri. By the way, huo ni ushabiki usio na maana, think globally!
 
Ndio maana wengine wenye kumbukumbu za siasa zetu tunashangaa wapiganaji wenzetu wanapoanza kulalamika kwenye issues kama hizi ...huyu Kabwe aliisumbua sana CHADEMA ...saaana ...alafu leo kwasababu ya chuki zako kwa CCM unamtetea eti hakupewa fursa ya kujitetea ....huyu watu wa Mwanza wa wanajua vyema fitna zake kwa upinzani ...
 
Ndio maana wengine wenye kumbukumbu za siasa zetu tunashangaa wapiganaji wenzetu wanapoanza kulalamika kwenye issues kama hizi ...huyu Kabwe aliisumbua sana Chadema ...saaana ...alafu leo kwasababu ya chuki zako kwa CCM unamtetea eti hakupewa fursa ya kujitetea ....huyu watu wa Mwanza wa wanajua vyema fitna zake kwa upinzani ...
Hapana, hayo mambo ya vyama hayawez kuondoa undugu tulio nao kama Taifa
 
Mhe. Rais,nina ujumbe mfupi tu kwako. Tafadhali usiruhusu Serikali yako kuwa ya visasi,kuchongeana na 'kucheza na jukwaa'. Pale ambapo watumishi wa umma watapaswa kushughulikiwa,Sheria za Utumishi wa Umma na zile za Ajira zisiwekwe kando na hasira,malengo na uharaka wa kutumbua majipu.

Utumbuaji wa aina ya wa Wilson Kabwe unatweza na kuchora picha ya visasi na kuchongeana. Watumishi wa umma wapewe nafasi kujieleza kabla ya kushughulikiwa. Kwa hali inayoendelea,it is serious and the country is heading to unpleasant situation.

Watumbuliwaji nao wanastahili staha na faragha! Kwanini heshima ilindwe kwa watumishi wa BOT tu?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
naunga mkono hoja asilimia 100
 
Back
Top Bottom