CHA The GREAT
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 651
- 853
Hakuna asiyelitakia mema taifa hili kupitia Rais wa nchi, John Pombe Magufuli. Kila mtu anataka kuona Tanzania yenye neema, Tanzania yenye huduma bora kabisa za afya, Tanzania yenye miundombinu bora kabisa, Tanzania yenye uchumi imara, watu imara, wenye afya imara na elimu imara. Ila yote haya hayawezi kuja iwapo tu, tutakuwa wanafiki. Tukiacha unafiki, tukaweka siasa pembeni yote hayo yanawezekana.
Kwa hali hii na mazingira haya, mawazo ya akina Tundu Lissu, yasipuuzwe na wana CCM waliopo madarakani, lazima yaangaliwe kwa jicho la tatu, kadhalika ni lazima tumkosoe Rais pale anapokosea ili tupite njia iliyo sahihi.
Mambo ya kumpongeza Rais kwa kila kitu hata kama ni cha hovyo, ni ujuha, unafiki, na uzezeta; halikadhalika, kupuuza kila wazo la Tundu Lissu kwa sababu tu ni mtu kutoka CHADEMA, pia ni ujuha, uzezeta, na unafiki uliovuka mipaka.
Ifike wakati tuheshimu mawazo ya kila mmoja kwenye jamii, kwani hivyo ndivyo wenzetu huko kulikoendelea wafanyavyo. Ifike wakati tutambue kuwa Rais si malaika kwamba kila atakalosema, kila atakalofanya ni sahihi; na yeye anahitaji kusahihishwa, na kushauriwa pia.
Tujifunze Kujifunza.
SIASA pembeni UTAIFA kwanza.