Rais Magufuli si malaika, Tundu Lissu si shetani.

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
652
1,000
Hakuna asiyelitakia mema taifa hili kupitia Rais wa nchi, John Pombe Magufuli. Kila mtu anataka kuona Tanzania yenye neema, Tanzania yenye huduma bora kabisa za afya, Tanzania yenye miundombinu bora kabisa, Tanzania yenye uchumi imara, watu imara, wenye afya imara na elimu imara. Ila yote haya hayawezi kuja iwapo tu, tutakuwa wanafiki. Tukiacha unafiki, tukaweka siasa pembeni yote hayo yanawezekana.

Kwa hali hii na mazingira haya, mawazo ya akina Tundu Lissu, yasipuuzwe na wana CCM waliopo madarakani, lazima yaangaliwe kwa jicho la tatu, kadhalika ni lazima tumkosoe Rais pale anapokosea ili tupite njia iliyo sahihi.

Mambo ya kumpongeza Rais kwa kila kitu hata kama ni cha hovyo, ni ujuha, unafiki, na uzezeta; halikadhalika, kupuuza kila wazo la Tundu Lissu kwa sababu tu ni mtu kutoka CHADEMA, pia ni ujuha, uzezeta, na unafiki uliovuka mipaka.

Ifike wakati tuheshimu mawazo ya kila mmoja kwenye jamii, kwani hivyo ndivyo wenzetu huko kulikoendelea wafanyavyo. Ifike wakati tutambue kuwa Rais si malaika kwamba kila atakalosema, kila atakalofanya ni sahihi; na yeye anahitaji kusahihishwa, na kushauriwa pia.

Tujifunze Kujifunza.

SIASA pembeni UTAIFA kwanza.

DM-Magufuli-100-days-Simon-Allison.jpg
TunduLissu.jpg
 
Attachments

Kipapatiro

JF-Expert Member
May 18, 2017
1,055
2,000
Hakuna asiyelitakia mema taifa hili kupitia Rais wa nchi, John Pombe Magufuli. Kila mtu anataka kuona Tanzania yenye neema, Tanzania yenye huduma bora kabisa za afya, Tanzania yenye miundombinu bora kabisa, Tanzania yenye uchumi imara, watu imara, wenye afya imara na elimu imara. Ila yote haya hayawezi kuja iwapo tu, tutakuwa wanafiki. Tukiacha unafiki, tukaweka siasa pembeni yote hayo yanawezekana. Kwa hali hii na mazingira haya, mawazo ya akina Tundu Lissu, yasipuuzwe na wana CCM waliopo madarakani, lazima yaangaliwe kwa jicho la tatu, kadhalika ni lazima tumkosoe Rais pale anapokosea ili tupite njia iliyo sahihi. Mambo ya kumpongeza Rais kwa kila kitu hata kama ni cha hovyo, ni ujuha, unafiki, na uzezeta; halikadhalika, kupuuza kila wazo la Tundu Lissu kwa sababu tu ni mtu kutoka CHADEMA, pia ni ujuha, uzezeta, na unafiki uliovuka mipaka. Ifike wakati tuheshimu mawazo ya kila mmoja kwenye jamii, kwani hivyo ndivyo wenzetu huko kulikoendelea wafanyavyo. Ifike wakati tutambue kuwa Rais si malaika kwamba kila atakalosema, kila atakalofanya ni sahihi; na yeye anahitaji kusahihishwa, na kushauriwa pia.

Tujifunze Kujifunza.

SIASA pembeni UTAIFA kwanza.

View attachment 524658 View attachment 524661
Jamaa Yako hataki kukosolewa anajiona ndugu yake Na "Yesu"
 
Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
12,590
2,000
Ukweli ndiyo huu, mtu anayejifanya ana uchungu sana na nchi hii amekuwa member wa baraza la mawaziri kwa kipindi choote hicho akishiriki kupitisha uwizi huu. Na wakati huo huo kwa kipindi choote hicho Tundu Lisu amekuwa akihangaishwa na kesi za uchochezi mahakamani kwa kupinga miradi hiyo, ambayo Leo yanaitwa ya uwizi!

Bahati mbaya kwa nchi yangu ni kuwa Rais akisema na kuagiza jambo hata kama halina mashiko, linaonekana ni la kizalendo na watu hushurutishwa kumuunga mkono. HUU NI UWENDA WAZIMU WA TAIFA LANGU TZ
 
South

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
3,483
2,000
Hapo kuna anayetumia akili na anayetumia nguvu na huyu wa kutumia nguvu atachoka si muda mrefu
 
Kikarara78

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
1,493
2,000
Boss CHA The GREAT una Hoja ya Kufikirisha sana. Hongera. Mimi Binafsi namuunga Mkono Rais, Na Vile Vile nawapongeza sana Wapinzani wote. Maana bila Upinzani Madhubuti hakuna Maendeleo.

Hakuna asiyelitakia mema taifa hili kupitia Rais wa nchi, John Pombe Magufuli. Kila mtu anataka kuona Tanzania yenye neema, Tanzania yenye huduma bora kabisa za afya, Tanzania yenye miundombinu bora kabisa, Tanzania yenye uchumi imara, watu imara, wenye afya imara na elimu imara. Ila yote haya hayawezi kuja iwapo tu, tutakuwa wanafiki. Tukiacha unafiki, tukaweka siasa pembeni yote hayo yanawezekana. Kwa hali hii na mazingira haya, mawazo ya akina Tundu Lissu, yasipuuzwe na wana CCM waliopo madarakani, lazima yaangaliwe kwa jicho la tatu, kadhalika ni lazima tumkosoe Rais pale anapokosea ili tupite njia iliyo sahihi. Mambo ya kumpongeza Rais kwa kila kitu hata kama ni cha hovyo, ni ujuha, unafiki, na uzezeta; halikadhalika, kupuuza kila wazo la Tundu Lissu kwa sababu tu ni mtu kutoka CHADEMA, pia ni ujuha, uzezeta, na unafiki uliovuka mipaka. Ifike wakati tuheshimu mawazo ya kila mmoja kwenye jamii, kwani hivyo ndivyo wenzetu huko kulikoendelea wafanyavyo. Ifike wakati tutambue kuwa Rais si malaika kwamba kila atakalosema, kila atakalofanya ni sahihi; na yeye anahitaji kusahihishwa, na kushauriwa pia.

Tujifunze Kujifunza.

SIASA pembeni UTAIFA kwanza.

View attachment 524658 View attachment 524661
 
tamuuuuu

JF-Expert Member
Mar 10, 2014
13,934
2,000
Tume huru idaiwe mapema ccm itoke vinginevyo watanzania mtapata tabu sana
 
Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,097
2,000
Mtu ambaye a naamini yeye peke yake Ndio atainyoosha Tanzania ni shida sana!
Matokeo yake kila atakae toa wazi mbadala anamuona mbaya!
 
kbosho

JF-Expert Member
Jun 4, 2012
13,020
2,000
Tatizo la Maisha kuwa Magumu limewafanya Watanzania kuwa na uwezo mdogo sana wa kufikiri. Wakisikia Rais kasema hiki nao kama upepo wanampongeza, wanasahau Rais ni Mwanasiasa.
 
Magonjwa Mtambuka

JF-Expert Member
Aug 2, 2016
22,465
2,000
Wajameni hebu tuendelee kumpaka Lisu mafuta kwa mgongo wa chupa hadi kichwa chake kivimbe na kipasuke. Msichoke tafadhali.
 
nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,567
2,000
kwangu toka magu atoe kauli ya vyombo vya habari kutomsema jk na mkapa nimevunjika moyo sana na jmp.
 
CHA The GREAT

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
652
1,000
Boss CHA The GREAT una Hoja ya Kufikirisha sana. Hongera. Mimi Binafsi namuunga Mkono Rais, Na Vile Vile nawapongeza sana Wapinzani wote. Maana bila Upinzani Madhubuti hakuna Maendeleo.
Kikarara78, nimekaa, nimetafakari na kugundua Wadanganyika tumeathiriwa sana na SIHASA. Eti wazo likitolewa na Tundu Lissu, hata kama ni zuri kiasi gani, utamsikia mtu kama Livingiston Lusinde mbaye hata form four hakufika, anapinga. Aya, sawa anapinga, ukimwambia alete hoja kwa nini anapinga wazo la Tundu Lissu, anabaki kusema 'hao wapinzani ni wapiga kelele tu'. Anasahau kwamba, hakuna kelele zisizo na sababu.
 
cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
24,515
2,000
Yaani kwa mazuri anayofanya Raisi wetu, inawapeleka wengi kuwa wanaropoka na kuweweseka kwa sababu maishani mwao hakuwahi kufikiri atatokea Rais nchini Tanzania wa kutenda anayotenda Mheshimiwa Magufuli. Raisi ambaye ni chaguo la Mungu kuokoa nchi hata kama hatapata muda wa kufanya mengiiiiii

Ila ni kiboko ya wengi, yaani ni kama hawaamini wapo nchini. Hivyo tutazidi kuona mengi na kuyasikia kwa sababu, wao ni kama vile ndoto kwao.

Magufuli 2020

Magufuli oyeeeeeeee
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom