Rais Magufuli si malaika, Tundu Lissu si shetani.

Yaani kwa mazuri anayofanya Raisi wetu, inawapeleka wengi kuwa wanaropoka na kuweweseka kwa sababu maishani mwao hakuwahi kufikiri atatokea Rais nchini Tanzania wa kutenda anayotenda Mheshimiwa Magufuli. Raisi ambaye ni chaguo la Mungu kuokoa nchi hata kama hatapata muda wa kufanya mengiiiiii

Ila ni kiboko ya wengi, yaani ni kama hawaamini wapo nchini. Hivyo tutazidi kuona mengi na kuyasikia kwa sababu, wao ni kama vile ndoto kwao.

Magufuli 2020

Magufuli oyeeeeeeee
wewe endelea kumshangilia tu ilhali huku mtaani maisha ni magumu. pia angekuwa na dhamira ya dhati asingezuia jk na kikwete wasiandikwe na magazeti kuhusu makinikinia. watanzania tunadanganywa sana.
 
Yaani kwa mazuri anayofanya Raisi wetu, inawapeleka wengi kuwa wanaropoka na kuweweseka kwa sababu maishani mwao hakuwahi kufikiri atatokea Rais nchini Tanzania wa kutenda anayotenda Mheshimiwa Magufuli. Raisi ambaye ni chaguo la Mungu kuokoa nchi hata kama hatapata muda wa kufanya mengiiiiii

Ila ni kiboko ya wengi, yaani ni kama hawaamini wapo nchini. Hivyo tutazidi kuona mengi na kuyasikia kwa sababu, wao ni kama vile ndoto kwao.

Magufuli 2020

Magufuli oyeeeeeeee
sio kwamba anafanya vibaya bali anafanya vibaya na vizuri at the same time hapo tu ndo tunaona unafiki wa mkuu
 
Tunarudia kusema Ndugu yake Yesu hua hakosolewii..
Mimi naendelea kushangilia..
 
Unajua kuna vitu vinachekesha kuna viumbe hawataki kukosolewa mpaka kutishia malaika washuke kufunga mitandao.

Huyu ambaye hapendi kukosolewa yeye ndio kazi yake kila siku..ni kulia lia tu na kufoka foka.

Tujiulize hao wenzake walio mtangulia kama wasinge kosolewa leo kina EPA, RICHMOND, NBC, KIWIRA, ESCOROW tungezifahamu kweli? Si wangeiba mara mia ya hapo kama watu wangekaa kimya na kukubali bora liende tu?
 
Naomba sana mzalendo Mh. Tundu Lissu asilinganishwe na majizi yoliyoliibia taifa
miaka nenda rudi halafu leo yanadai eti yako vitani kulinyosha taifa.

Hii video imenifurahisha na kunihuzunisha.

Wakati Tundu Lisu anaongea namuona Chenge anatikisa kichwa halafu anapitia makabrasha ya wizi wao wa Escorow hapo moyoni atakuwa alikuwa anamuambia Lisu " Son you don't know what you are talking about, you are wasting your energy for no reasons "

Na kweli Chenge alikuwa sahihi kwani kafanywa nini baada ya huo wizi?

Leo yupo tena kwenye Makinikia

Dah Tanzania yangu hii.
 
Hakuna asiyelitakia mema taifa hili kupitia Rais wa nchi, John Pombe Magufuli. Kila mtu anataka kuona Tanzania yenye neema, Tanzania yenye huduma bora kabisa za afya, Tanzania yenye miundombinu bora kabisa, Tanzania yenye uchumi imara, watu imara, wenye afya imara na elimu imara. Ila yote haya hayawezi kuja iwapo tu, tutakuwa wanafiki. Tukiacha unafiki, tukaweka siasa pembeni yote hayo yanawezekana.

Kwa hali hii na mazingira haya, mawazo ya akina Tundu Lissu, yasipuuzwe na wana CCM waliopo madarakani, lazima yaangaliwe kwa jicho la tatu, kadhalika ni lazima tumkosoe Rais pale anapokosea ili tupite njia iliyo sahihi.

Mambo ya kumpongeza Rais kwa kila kitu hata kama ni cha hovyo, ni ujuha, unafiki, na uzezeta; halikadhalika, kupuuza kila wazo la Tundu Lissu kwa sababu tu ni mtu kutoka CHADEMA, pia ni ujuha, uzezeta, na unafiki uliovuka mipaka.

Ifike wakati tuheshimu mawazo ya kila mmoja kwenye jamii, kwani hivyo ndivyo wenzetu huko kulikoendelea wafanyavyo. Ifike wakati tutambue kuwa Rais si malaika kwamba kila atakalosema, kila atakalofanya ni sahihi; na yeye anahitaji kusahihishwa, na kushauriwa pia.

Tujifunze Kujifunza.

SIASA pembeni UTAIFA kwanza.

View attachment 524658 View attachment 524661
Tz ina mtu mmoja 2 mbishi mwenye malengo naye tunfu lissu
 
Yaani kwa mazuri anayofanya Raisi wetu, inawapeleka wengi kuwa wanaropoka na kuweweseka kwa sababu maishani mwao hakuwahi kufikiri atatokea Rais nchini Tanzania wa kutenda anayotenda Mheshimiwa Magufuli. Raisi ambaye ni chaguo la Mungu kuokoa nchi hata kama hatapata muda wa kufanya mengiiiiii

Ila ni kiboko ya wengi, yaani ni kama hawaamini wapo nchini. Hivyo tutazidi kuona mengi na kuyasikia kwa sababu, wao ni kama vile ndoto kwao.

Magufuli 2020

Magufuli oyeeeeeeee
Hakuna Rais ambaye ni chaguo la Mungu. Na haijawahi kutokea Afrika, Uropa, America, Asia na kwingineko. Hayo ni mawazo ya watu wenye ubongo mdogo sana, kwamba, Rais ni chaguo la Mungu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom