Rais Magufuli punguza wazee vyuo vikuu

4. Wazee wanapunja nafasi za ajira kwa vijana wanaotakiwa kurejesha mikopo bodi ya mikopo
Acha umbumbumbu ndugu. Unajua maana ya mwanataaluma wewe? Hakuna nchi duniani inayochezea uzoefu na ubobezi wa hawa watu unaowaita wazee. Halafu hili wazo la eti mtu ameziba ajira ni wazo la kimaskini. Badala ya kuleta mawazo ya kutengeneza nafasi za kazi zaidi (job creation) unaleta mawazo mfu eti fulani atoke mimi niingie. Ukitaka taifa life leo kitaaluma, achisha kazi hawa wataalamu unaowaita wazee waliochoka uone. Huko nje wanasukumwa hata kwenye vibaiskeli ili tu afike darasani afundishe halafu wewe unaleta upoyoyo hapa.
 
Wakongwe wana uzoefu mkubwa acha kubagua wazee nao wali kuwa vijana. Bora profesa mzee huwa hawana longolongo kwanza kuwatoa wote vyuoni nchi hii bado INA uhaba mkubwa wa ma profesa
 
Utaalamu wa chuo ni tofauti na utumishi mmngine kadri unavyokaa ndio unavyohitajika Zaidi, kwani unaendelea kugundua vitu vingine zaid na zaid katika utafiti . Sio suala la kufikisha miaka 60 na kupisha. Hapa unazungumzia utafiti na contribution of knowledge to the world.
Kama nguvu na akili hizo bado unazo anzisha taasisi yako basi na wewe ili utoe ajira kwa vijana pamoja na kuendelea kufanya tafiti zako huko huko kwenye taasisi yako, kwanini lazima uwajiriwe upya tena na mtu ndio ufanye utafiti? Ninamuona Dk. Kaushik anajitegemea lakini anaitwa vyuoni na kwenye mikutano pia akatoe uzoefu wake. Prof. Shivj anaitwa sehemu nyingi bpamoja na kustaafu kwake, kulikoni kwa akina.....
 
Mmmh!kwa kiasi flan uko sawa.Ila ungeweka vizur uzee upi unaouzungumzia hapa.Mi naamini prof.mwenye miaka 60's huyo bado anamsaada mkunwa Sn kwny research hasa theoretical part ktk field aliyobobea akiachwa huyu ni hasara kubwa Sn kwa ustaw wa eneo alilobobea. Uzee wa kuanzia 70 hapo prof. Anaweza pumzika.huku ulaya unakuta maprof wastaaf()(emeritus prof) idaran wanakua na ofisi ila hawafanyi kaz, Zaid ya kusimamia mitihan na kaz zingne ndogondogo huku wakipata allowance fulan

Tatizo garama za huduma kwao imekuwa kubwa mno na kusema ukweli kinachowaweka wazee ni kwakua pension ni mbovu. Na kwakuaogopa kukosa contract hawa support vijana ki grow kwenye carrier badala yake wamekuwa wakwamishaji au kimkakati au kwamatumizi ya malipo yao ambayo yanakielemea chuo kwakiasi kikubwa...

Wazee wetu ni muhimu sana na wanamahitaji yakuangaliwa ila pia lazima kuwe na balance kwakua hata tungewapenda vipi wengi wao mika kumi hawataweza ijayo hawataweza tena kuwa productive at the same time hatutakuwa tumepata vijana wanaoweza kuziba pengo. Hii linahitaji serikali kuingilia kati. Ukiwaachia viongozi wa vyuo ku deal navyo nao wapo kwenye kundi hilo hilo hutapata muafaka wa swala hilo. Utakuta wanatumia muda mwingi kutafuta justifications za wao kuendelea kubaki badala ya kutengeneza pragmatic solutions.
 
Kama nguvu na akili hizo bado unazo anzisha taasisi yako basi na wewe ili utoe ajira kwa vijana pamoja na kuendelea kufanya tafiti zako huko huko kwenye taasisi yako, kwanini lazima uwajiriwe upya tena na mtu ndio ufanye utafiti?
Mmmh! Unatia shaka ya uelewa wa elimu ya juu.Ndio shida ya kubaki mmejifungia Tanzania.Njooni dunia muone mambo yalivyo.
 
Utakuta miaka kumi umeajiriwa chuo lakini wimbo ni ule ule ooo hatuna professor wakutosha huku ukiangalia kuna vijana wana machapisho mara mbili na wamefanya kazi za maana za kitaaluma zaidi ya mara tatu ya hao wanaoitwa ma prof lakini kila mara goli la criteria to promotion linahamishwa na hao hao wanaolalamika hakuna ma prof...ni hakuna kweli au wanasababisha wasiwepo kwa malengo yao? Hivi tukifanya uchunguzi wa CVs za waajiriwa ukazilinganisha na hao ambao tayari leo ni ma Prof na wale ambao wanaitwa vijana ambao hawawezi kuziba pengo hatuwezi kuona mlingano wa kweli nani ana stahili kuwa prof kati ya kijana na huyo mzee prof?

Viongozi watambue kiwa siasa ipo pia kwenye academics na hii siyo kwetu tu ni dunia nzima...hizo gap zinazoongelewa nyakati zingine deep down ni complains za wazee kuwa pension haitoshi. Pengine kuwapa incentives wazee pension vyuo vikuu iboreshwe na wale wenye hiari ya kustaafu wapewe incentive ya kukubali kustaafu badala ya contract.

Kwa ufupi swala hili lifanyiwe uchunguxi wa kina!
 
Mmmh! Unatia shaka ya uelewa wa elimu ya juu.Ndio shida ya kubaki mmejifungia Tanzania.Njooni dunia muone mambo yalivyo.
Utahitaji tu affiliation lakini sio ukuu wa idara tena na subject mater.
 
Ukiwa na vigezo na uwezo.utatafutwa, pia hivyo vyyo vya binafsi vingi havisomeshi sana wao wanatangaza mtu mwenye sifa .
Unaweza ukatamani uwe muhadhili na ukajiona unafaa ila wansohitaji wakakuona haufai.
Mm binafsi wazee wenye phd niliwaona walimu wazuri kuliko vijana wenye phd zaid ya majigambo yao na kushindani mabinti au kushikana kwa bifu nje ya taaluma.( niliyoshuudia nikiwa undergraduate) japo kuna vijana wanaweza kuwa wazuri tu.pia km wakenya na wengine wanakuja kwetu kwa nn usiende nchi za nje.?
 
Haku
Utakuta miaka kumi umeajiriwa chuo lakini wimbo ni ule ule ooo hatuna professor wakutosha huku ukiangalia kuna vijana wana machapisho mara mbili na wamefanya kazi za maana za kitaaluma zaidi ya mara tatu ya hao wanaoitwa ma prof lakini kila mara goli la criteria to promotion linahamishwa na hao hao wanaolalamika hakuna ma prof...ni hakuna kweli au wanasababisha wasiwepo kwa malengo yao? Hivi tukifanya uchunguzi wa CVs za waajiriwa ukazilinganisha na hao ambao tayari leo ni ma Prof na wale ambao wanaitwa vijana ambao hawawezi kuziba pengo hatuwezi kuona mlingano wa kweli nani ana stahili kuwa prof kati ya kijana na huyo mzee prof?

Viongozi watambue kiwa siasa ipo pia kwenye academics na hii siyo kwetu tu ni dunia nzima...hizo gap zinazoongelewa nyakati zingine deep down ni complains za wazee kuwa pension haitoshi. Pengine kuwapa incentives wazee pension vyuo vikuu iboreshwe na wale wenye hiari ya kustaafu wapewe incentive ya kukubali kustaafu badala ya contract.

Kwa ufupi swala hili lifanyiwe uchunguxi wa kina!
Hakuna pension inayoyosha.kujipanga tu pia mkataba ni hiyari sio lazima
 
Sasa naona walau inaelekea. Kuwa Prof. tu inatosha ukuu wa idara wa kazi gani .... Ukiwa na vyeo vingi unakosa muda wa kufanya utafiti
huku kwetu sisi mtu wa miaka 75 anabisha hodi kwenye taasisi (chuo) anatafuta ajira ya kufundisha, kuwa mkuu wa kitivo, au kuwa chochote kile kama vile vijana waliomaliza shule wanavyotafuta ajira. Kwakuwa TCU wanasema lazima uwe na Professor hapo, basi jamaa huyu atapewa ajira tu fasta fasta ili kufunika kombe mwanaharamu apite. Akishapewa kazi ana kuwa 'mono', kufundisha tu basi na notes zake za long kitambo ndizo hizo hizo akidhani anafahamu sana ....we used to.... we used to..... and too much wordy in class sessions and meetings. akichoka stories politics kwa sana. we acha 2 bana.
 
huku kwetu sisi mtu wa miaka 75 anabisha hodi kwenye taasisi (chuo) anatafuta ajira ya kufundisha, kuwa mkuu wa kitivo, kuwa.... na chochote kile kama vile vijana waliomaliza shule wanavyotafuta ajira. Kwakuwa TCU wanasema lazima uwe na Professor hapo, basi jamaa huyu atapewa ajira tu fasta fasta ili kufunika kombe mwanaharamu apite.
That is too much. Pension utakula saa ngapi?
 
Mnataka mfundishane kuvaa mlegezo siyo taaluma,,
Vijana wengi SAS HV hamjielewi bila kuwepo wazee wa kuwakemea hamuoni haya kutembea Uchi Kama Mbuzi,,so wasichana wala si wavulana wote fahari yenu ni kutembea Uchi tu.

Hatuwezi kuwaachia Vyuo vyetu kwa sabb bado hamjielewi na milegezo yenu hiyo ya Suruali.
 
Kama vijana wenyewe ndio wanaofikiria kama wewe basi kuna haja ya hawa wazee kuendelea kuwepo vyuoni kusaidia hiki kizazi cha kata K.
 
Acha mawazo mgando wewe kwa taarifa yako hao washusha suluali hawawezi kufundisha kuliko wazee.......

Yaani unamlinganisha Mzee aliyepata degree Oxford univesty mwaka 1970 na hawa waliopata degree St Joseph university juzi?.....

Acha wazee wafundishe ndio wenye experience sio hawa vijana wa mwendokasi..

Nafikiri wasomi wananiekewa ........
Yaani technically kama ulikuwa kwenye kichwa changu! Hilo hilo la mitepesho ndilo nilitaka kuulizia! Halafu sijui unazungumzia chuo gani huyu zombie? Mbona vyuo vingi tu wakuu wa idara ni vijana? Au anamaanisha hata wale wenye miaka 46 wasipewe ukuu wa idara?
 
Vijana wenyewe wahuni wahuni

Kwenye Academics mtu alie na miaka mingi ndio demanded kuliko kijana
 
Vyuo vingi havina walimu bali vimekusanya wazee waliochoka waliostaafu kwenye vyuo vya umma na kusababisha Vijana wanaomaliza vyuo kupata ajira vyuo vikuu kwa taabu sana.

Utakuta Makamu Mkuu wa chuo ni mstaafu, Naibu Makamu mkuu wa chuo taaluma ni mstaafu, Naibu Makamu Mkuu wa chuo mipango na fedha ni msataafu, Bwana fedha (Bursar) ni mstaafu, wakuu wa vitivo ni wastaafu. Wastaafu hawa huwa wanapenda kuajiri wastaafu wenzao katika nafasi mbalimbali katika vyuo na kuacha kuwaajiri vijana kwa kuogopa eti vijana wanachangamoto nyingi zikiwemo za kuhoji hoji mambo na kuhitaji kuendelezwa kitaaluma. Hii inasababisha hasara zifuatazo kwa taifa.

1. Wazee wengi hawana jipa ila wanaendeleza kufundisha vijana kile wanachokifahamu tu na walichofanyiwa wao enzi zao hata kama hakikuleta manufaa kwa taifa.

2. Wazee wengi wamechoka sana, muda mwingi wanaumwa (mgongo, pressure, kisukari, macho, mifupa)

3. Taifa linawekeza (semina, mafunzo) kwa wazee tena ambao muda wao umekwisha badala ya kuwekeza kwa vijana ambao wana kesho nyingi.

4. Wazee wanapunja nafasi za ajira kwa vijana wanaotakiwa kurejesha mikopo bodi ya mikopo

5. Baadhi ta wazee hawapendi kuona vijana wanafaulu sana kwenye masomo ya fani zao ili kuepuka kuchukua nafasi zao. Yaani hawaandai warithi wao (succession plan).

6. Baadhi ya wazee wana frustrations mbalimbali zilizotokana na maisha waliyoishi siku za nyuma, hivyo kuwafundisha vijana namna ya kuichuikia nchi yao.

7. Wazee mara nyingi hawakai ofisini/hawafundishi kwasababu za kusafirisafiri sana, kifamila au kiafya.

8. Expire date (yale makuni 7) za wazee ziko karibu sana, hivyo, Misiba ya walimu (wazee) ya mara kwa mara vyuoni inavuruga ratiba za vipindi darasani.

Kifupi, vyuo vingi havina walimu vibrant wa kufundisha vijana vyuo vikuu ila wastaafu waliojikusanya kwenye vyuo binafsi kuganga njaa zao baada ya kutumika kwenye vyuo vya umma. Ni wazuri kwa kuwakumbusha vijana maadili ya taaluma (babu) lakini sio productive and innovative.

Lazima kutolewe muongozo kuhusu idadi ya wastaafu vyuoni ili kuinusuru taaluma yetu.
Toa mfano ni chuo gani hicho ambacho kimejaa menejiment ya wastaafu
 
Acha mawazo mgando wewe kwa taarifa yako hao washusha suluali hawawezi kufundisha kuliko wazee.......

Yaani unamlinganisha Mzee aliyepata degree Oxford univesty mwaka 1970 na hawa waliopata degree St Joseph university juzi?.....

Acha wazee wafundishe ndio wenye experience sio hawa vijana wa mwendokasi..

Nafikiri wasomi wananiekewa ........
We ni mpumbavu na mshenzi tu!
 
Acha umbumbumbu ndugu. Unajua maana ya mwanataaluma wewe? Hakuna nchi duniani inayochezea uzoefu na ubobezi wa hawa watu unaowaita wazee. Halafu hili wazo la eti mtu ameziba ajira ni wazo la kimaskini. Badala ya kuleta mawazo ya kutengeneza nafasi za kazi zaidi (job creation) unaleta mawazo mfu eti fulani atoke mimi niingie. Ukitaka taifa life leo kitaaluma, achisha kazi hawa wataalamu unaowaita wazee waliochoka uone. Huko nje wanasukumwa hata kwenye vibaiskeli ili tu afike darasani afundishe halafu wewe unaleta upoyoyo hapa.
Hao wazee wamesaidia nini zaidi ya kunenepeana tu kama vifaru?
 
Si wazo zuri Elimu duniani kote vikongwe ndo huwa Waliimu wa Vyuo Vikuu mi naona wako sahihi Ualimu wa vyuo safari yao huanza Wakiwa na Miaka 50 kuendelea na ndo wanakua wazuri sana. Yaani Serikali imteme Professor wa Muhimbili University aliyefanya Successful Operations/Surgery 1000 na Kumuajiri Kijana mwenye miaka 30
Vyuo vikuu vingine profesa anafundisha mpaka anakufa. Naunga mkono waendelee kufundisha lakini wasipewe nafasi za uongozi
 
Back
Top Bottom