Rais Magufuli punguza wazee vyuo vikuu

Rais Magufuli punguza wazee vyuo vikuu

Vyuo vingi havina walimu bali vimekusanya wazee waliochoka waliostaafu kwenye vyuo vya umma na kusababisha Vijana wanaomaliza vyuo kupata ajira vyuo vikuu kwa taabu sana.

Utakuta Makamu Mkuu wa chuo ni mstaafu, Naibu Makamu mkuu wa chuo taaluma ni mstaafu, Naibu Makamu Mkuu wa chuo mipango na fedha ni msataafu, Bwana fedha (Bursar) ni mstaafu, wakuu wa vitivo ni wastaafu. Wastaafu hawa huwa wanapenda kuajiri wastaafu wenzao katika nafasi mbalimbali katika vyuo na kuacha kuwaajiri vijana kwa kuogopa eti vijana wanachangamoto nyingi zikiwemo za kuhoji hoji mambo na kuhitaji kuendelezwa kitaaluma. Hii inasababisha hasara zifuatazo kwa taifa.

1. Wazee wengi hawana jipa ila wanaendeleza kufundisha vijana kile wanachokifahamu tu na walichofanyiwa wao enzi zao hata kama hakikuleta manufaa kwa taifa.

2. Wazee wengi wamechoka sana, muda mwingi wanaumwa (mgongo, pressure, kisukari, macho, mifupa)

3. Taifa linawekeza (semina, mafunzo) kwa wazee tena ambao muda wao umekwisha badala ya kuwekeza kwa vijana ambao wana kesho nyingi.

4. Wazee wanapunja nafasi za ajira kwa vijana wanaotakiwa kurejesha mikopo bodi ya mikopo

5. Baadhi ta wazee hawapendi kuona vijana wanafaulu sana kwenye masomo ya fani zao ili kuepuka kuchukua nafasi zao. Yaani hawaandai warithi wao (succession plan).

6. Baadhi ya wazee wana frustrations mbalimbali zilizotokana na maisha waliyoishi siku za nyuma, hivyo kuwafundisha vijana namna ya kuichuikia nchi yao.

7. Wazee mara nyingi hawakai ofisini/hawafundishi kwasababu za kusafirisafiri sana, kifamila au kiafya.

8. Expire date (yale makuni 7) za wazee ziko karibu sana, hivyo, Misiba ya walimu (wazee) ya mara kwa mara vyuoni inavuruga ratiba za vipindi darasani.

Kifupi, vyuo vingi havina walimu vibrant wa kufundisha vijana vyuo vikuu ila wastaafu waliojikusanya kwenye vyuo binafsi kuganga njaa zao baada ya kutumika kwenye vyuo vya umma. Ni wazuri kwa kuwakumbusha vijana maadili ya taaluma (babu) lakini sio productive and innovative.

Lazima kutolewe muongozo kuhusu idadi ya wastaafu vyuoni ili kuinusuru taaluma yetu.

Vilaza wenzio huenda hata wao wasikuelewe.
 
Utakuta Makamu Mkuu wa chuo ni mstaafu, Naibu Makamu mkuu wa chuo taaluma ni mstaafu, Naibu Makamu Mkuu wa chuo mipango na fedha ni msataafu, Bwana fedha (Bursar) ni mstaafu, wakuu wa vitivo ni wastaafu. Wastaafu hawa huwa wanapenda kuajiri wastaafu wenzao katika nafasi mbalimbali katika vyuo na kuacha kuwaajiri vijana kwa kuogopa eti vijana wanachangamoto nyingi zikiwemo za kuhoji hoji mambo na kuhitaji kuendelezwa kitaaluma. Hii inasababisha hasara zifuatazo kwa taifa.
Toa mifano
 
Acha mawazo mgando wewe kwa taarifa yako hao washusha suluali hawawezi kufundisha kuliko wazee.......

Yaani unamlinganisha Mzee aliyepata degree Oxford univesty mwaka 1970 na hawa waliopata degree St Joseph university juzi?.....

Acha wazee wafundishe ndio wenye experience sio hawa vijana wa mwendokasi..

Nafikiri wasomi wananiekewa ........
Ndiyo nyie unaosema wanamuziki wa zamani walikuwa wazuri kuliko wasanii wa sasa. Lakini wanamusic wa sasa ni matajiri kuliko wa zamani
 
Acha umbumbumbu ndugu. Unajua maana ya mwanataaluma wewe? Hakuna nchi duniani inayochezea uzoefu na ubobezi wa hawa watu unaowaita wazee. Halafu hili wazo la eti mtu ameziba ajira ni wazo la kimaskini. Badala ya kuleta mawazo ya kutengeneza nafasi za kazi zaidi (job creation) unaleta mawazo mfu eti fulani atoke mimi niingie. Ukitaka taifa life leo kitaaluma, achisha kazi hawa wataalamu unaowaita wazee waliochoka uone. Huko nje wanasukumwa hata kwenye vibaiskeli ili tu afike darasani afundishe halafu wewe unaleta upoyoyo hapa.
Tusingetosha duniani kama wengine wasingekufa. Ndio maana kuna kustaafu basi wangeacha hadi watu wafie kazini wenyewe. Taasisi zote zilizokumbatia wazee wengi lazima zitadumaa Tu. Wazee wako slow kwenye decision making na kunyumbulika, change kwao nibadui namba 1, adui namba 2 ni kukosolewa.
 
Mnataka mfundishane kuvaa mlegezo siyo taaluma,,
Vijana wengi SAS HV hamjielewi bila kuwepo wazee wa kuwakemea hamuoni haya kutembea Uchi Kama Mbuzi,,so wasichana wala si wavulana wote fahari yenu ni kutembea Uchi tu.

Hatuwezi kuwaachia Vyuo vyetu kwa sabb bado hamjielewi na milegezo yenu hiyo ya Suruali.
Kama mgonjwa na dk wote tumevaa milegezo kuna ubaya gani? Hicho ni kizazi chetu na magonjwa yetu. Wazee wakapunzike watoe ushauri wakitokea nyumbani, consultancy tyuu sio kuwa na position
 
Duuuhhhh, kazi kweli kweli.

Huenda una chuki binafsi na wazee. Leo umeanza na wahadhiri "wazee", kesho itakuwa madaktari, kesho kutwa itakuwa wanasiasa, n.k.

Mtu mwenye sifa ya kufundisha UDSM ana sifa ya kufundisha hata ng'ambo. Kwa nini hao vijana wasiwe na ujasiri wa kutoka nje ya mipaka ya Tanzania.
wewe umenena kama sifa ni zile zile kwanini wanataka hapa tu kuwaondoa wazee.
 
Back
Top Bottom