Vyuo vingi havina walimu bali vimekusanya wazee waliochoka waliostaafu kwenye vyuo vya umma na kusababisha Vijana wanaomaliza vyuo kupata ajira vyuo vikuu kwa taabu sana.
Utakuta Makamu Mkuu wa chuo ni mstaafu, Naibu Makamu mkuu wa chuo taaluma ni mstaafu, Naibu Makamu Mkuu wa chuo mipango na fedha ni msataafu, Bwana fedha (Bursar) ni mstaafu, wakuu wa vitivo ni wastaafu. Wastaafu hawa huwa wanapenda kuajiri wastaafu wenzao katika nafasi mbalimbali katika vyuo na kuacha kuwaajiri vijana kwa kuogopa eti vijana wanachangamoto nyingi zikiwemo za kuhoji hoji mambo na kuhitaji kuendelezwa kitaaluma. Hii inasababisha hasara zifuatazo kwa taifa.
1. Wazee wengi hawana jipa ila wanaendeleza kufundisha vijana kile wanachokifahamu tu na walichofanyiwa wao enzi zao hata kama hakikuleta manufaa kwa taifa.
2. Wazee wengi wamechoka sana, muda mwingi wanaumwa (mgongo, pressure, kisukari, macho, mifupa)
3. Taifa linawekeza (semina, mafunzo) kwa wazee tena ambao muda wao umekwisha badala ya kuwekeza kwa vijana ambao wana kesho nyingi.
4. Wazee wanapunja nafasi za ajira kwa vijana wanaotakiwa kurejesha mikopo bodi ya mikopo
5. Baadhi ta wazee hawapendi kuona vijana wanafaulu sana kwenye masomo ya fani zao ili kuepuka kuchukua nafasi zao. Yaani hawaandai warithi wao (succession plan).
6. Baadhi ya wazee wana frustrations mbalimbali zilizotokana na maisha waliyoishi siku za nyuma, hivyo kuwafundisha vijana namna ya kuichuikia nchi yao.
7. Wazee mara nyingi hawakai ofisini/hawafundishi kwasababu za kusafirisafiri sana, kifamila au kiafya.
8. Expire date (yale makuni 7) za wazee ziko karibu sana, hivyo, Misiba ya walimu (wazee) ya mara kwa mara vyuoni inavuruga ratiba za vipindi darasani.
Kifupi, vyuo vingi havina walimu vibrant wa kufundisha vijana vyuo vikuu ila wastaafu waliojikusanya kwenye vyuo binafsi kuganga njaa zao baada ya kutumika kwenye vyuo vya umma. Ni wazuri kwa kuwakumbusha vijana maadili ya taaluma (babu) lakini sio productive and innovative.
Lazima kutolewe muongozo kuhusu idadi ya wastaafu vyuoni ili kuinusuru taaluma yetu.