Rais Magufuli nimekuvulia kofia

AUGUSTINO CHIWINGA

Verified Member
Apr 23, 2017
214
1,000
Na

Augustino Chiwinga

0756810804.

Naandika haya nikiwa ni mwingi wa furaha na faraja kubwa baada ya kushuhudia Taifa letu likipata maendeleo siku baada ya siku.

Rais Magufuli umekua ni mkombozi wa wanyonge walionyanyasika kwa muda mrefu haswa wachuuzi wadogo wadogo, tazama sasa umewaletea vitambulisho vitakavyowasfanya wasisumbuliwe tena na mgambo au watoza ushuru waliokosa utu.

Rais Magufuli kila napopita eneo la GEREZANI Kariakoo damu yangu ya kizalendo huwa inachemka kwa kasi pale napolion Daraja lililobeba reli ya kisasa ya Standard Gauge hakika huwa najisemea mwenyewe moyoni Tanzania imezaliwa upya.

Unazo sifa zote za uongozi bora kila mtu nchi nzima ana imani wewe, umekua ni kimbilio na msaada mkubwa kwa wananchi.Tangu ulipotangaza vijiji vilivyo ndani ya maeneo ya hifadhi visiondolewe ujue kwamba umegusa maisha ya jamii nyingi za kifugaji na wakulima zilizokua zinaishi kwa hofu ya kuondolewa katika maeneo hayo muda wowote. Shukrani zao kwao ni Baraka tosha kwako na ndio maana unalolifanya linafanikiwa.

Siku na nyakati za mateso kwa Watanzania zimeisha msaada kwa Wanachi unataka kwako wewe Rais wetu uliyeamua kuvaa mabomu na kujitoa muhanga mbele ya mabebebru na majahili majizi ili Raia wako wapone.Hakuna hakuna cha kukurudishia zaidi ya kukujazia kura nyingi pale mwaka 2020.

Ni mwaka wa tatu huu haujaenda nchi za nje, kwa sababu unataka utumie muda mrefu kushughulika na shida za Wananchi wa hapa nyumbani ambao ndio waliokuchagua.Huu ni uzalendo wa hali ya juu kuwahi kutokea nchini kwetu.

Usiogope wala kutetereka na maneno ya vibaraka waliokubali kununulika na kutumika na mabeberu kwa vipande vya fedha. Hakuna nchi ya kibeberu itakayokubali kuona Tanzania inakua nchi yenye uchumi wenye nguvu ndio maana wanawatumia vibaraka kama kina Tundu Lissu na Zitto Kabwe kuwapotosha wananchi ili kukupunguza kasi. Kwa msaada wa MUNGU umekua unashinda kila vita wanayokupiga watashindana lakini hawatashinda.

Chapa kazi onesha njia vijana hodari na wazalendo tupo pamoja na wewe katika kukuunga mkono kujenga nchi yetu nzuri Tanzania. Mti wenye matunda ndio unapigwa mawe. Hakika ungekua unafanya vibaya wasingekua wanakusema kwama wanavyofanya sasa hivi lakini kwa vile unafanya vizuri wanakusema ili wakutoe kweny right track yako.

Mambo mazuri unayofanya ni ushahidi mzuri kwa vizazi vya sasa mpaka vijavyo unaacha alama itakayoishi milele.

Songa mbele Rais Magufuli!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom