Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A Man of The People!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,574
Wanabodi,

Kadri siku zinavyokwenda, ndivyo Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli anavyozidi kuzikonga nyonyo za Watanzania, wanaopenda reality, simplicity, genuinely na down to earth, ndivyo wanavyozidi kumkubali huyu jamaa, na kitendo cha leo kupiga simu kwenye kipindi cha Clouds TV cha 360, ndio kimenimaliza kabisa!.

Japo Magufuli ni kiongozi dikiteta na katili na asiye na huruma kabisa kwa mafisadi, wabadhirifu na walarushwa, lakini udikiteta wake ni a Benevolent Dictator, anayefanya udikiteta kwa nia njema, moyo safi na dhamira thabiti ya kujenga, ila ni Magufuli huyo huyo pia ni very genuine, very truthfully, very open and transparent, ni mtu wa reality na very down to earth!.

Wanasiasa wengi sio genuine ni ma actorsna ma pretenders tuu wakijifanya wanajali matatizo ya wananchi ili tuu waonekane wanajali for political gain kupata political mileage, ila in reality na genuinely hawajali kitu, lakini Magufuli ni very real na very genuine!. Just imagine jinsi Balozi Sefue ilivyojituma kumtumikia rais Magufuli kwa karibu, lakini siku faili la mambo yake Sefue lilipotua tuu mezani kwa Magufuli, bila kukopesha wala kupepesa macho, alilitumbua tuu hilo jipu, japo huu ni ukatili, reality na genuinely ilimfanya Magufuli kufanya kweli bila kukopesha, hivyo huu ni uthibitisho, this man is for real!.

Kimadaraka Rais ndie top citizen number 1, yuko top kule juu kabisa kwenye top seat, kwenye kilele cha top power mountain, akiwa amezungukwa na wasaidizi, watumishi, washauri, walinzi, wapambe, etc, hivyo hadi aje kushuka mpaka kuwafikia watu wa chini kabisa ni shughuli!, lakini Magufuli huyu huyu, anaangalia TV, tena Kipindi cha kawaida kabisa, kama Kipindi cha makorokocho cha shilawadu, ambacho mimi sikiangalii, yeye sio tuu anaangalia shilawadu, bali anachukua simu, anawapigia waendesha kipindi ambao ni watu wa kawaida kabisa!, anazungumza nao!, anawapongeza!, hii ni uthibitisho Magufuli sio mtu anayejisikia, ni mtu simple, humble na down to earth, kitendo hiki kinatufanya sisi wananchi wa kawaida kumuona Magufuli, japo ni rais wetu, ila pia ni mwenzetu!.

Pongezi zake kwa Clouds Media pia zimetuma ujumbe mzito silently kwa TBC ambayo ndio TV yake na Redio Yake, kama Rais anatazama TV ya watu wengine na kuipongeza kwa kazi nzuri, vipi kuhusu TV yake ya TBC?!, Kama rais hatazami TBC, na badala yake anatazama Clouds TV, na kuipongeza, then nani anatazama TBC?!.

Kitendo cha mwenye TV kutoiangalia TV yake, kinatuma ujumbe kuwa jee kuna uwezekano rais haangalii TBC kwa sababu TBC inaboa?!, hivyo anaangalia Clouds kwa sababu imechangamka?!, ndio maana ameipigia simu kuipongeza?!.

Au kunauwezekano, rais anaangalia Clouds TV na pia anaangalia tv nyingine ikiwemo TV yake ya TBC, na TBC pia inafanya vizuri, na inastahili pongezi za rais, lakini kwa kufuata kanuni ya usijisifu mwenyewe, bali subiri kusifiwa na wengine, then hata TBC ifanye vizuri kiasi gani, haitasifiwa rais, bali wengine wakifanya vizuri, ndio watasifiwa!, hivyo Clouds imestahili kusifiwa kwa sababu imefanya vizuri kuliko hata ilivyotarajiwa?!.

Au pia inawezekana ni tabia tuu na yale mazoea ya mtu kudharau chake na kuthamini cha mwenzie?!.

Hongera sana Rais Dr. John Pombe Magufuli japo ni dictator , benevolent dictator, hongera sana for reality, simplicity, genuine na being down to earth, ukiwa ni mtu mwenye huruma sana, unaejali sana matatizo ya Watanzania, you are simply, just a man of the people!. Big up sana for this!.

NB-Rejea.Kwa vile humu jf kila siku kuna wageni humu, na kuna watu wenye chuki tuu na Magufuli, hivyo kwao wanataka kila siku Magufuli akosolewe tuu, ukimsifia tuu Magufuli kwa mazuri yoyote anayoyafanya, wenye chuki dhidi yake, watakunyooshea kidole na utaambiwa lengo ni kujipendekeza kwa rais Magufuli, ili kuteuliwa DC!, hivyo nawawekea rejea kuwa Magufuli, sijaanza kumzungumzia leo, na yote niliyozungumza nyuma bado sijabadili kitu chochote!.
Magufuli Kama Nyerere:Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi


Kufuatia watu waliofilisika kwa hoja kuwa lengo la uzi huu ni kujipalilia ili kuukwaa U-DC
Naomba nijitambulishe ili tufahamiane.
Mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, ninamiliki ka ofisi fulani kadogo maeneo ya mjini kati, na nimeajiri vijana 10 fulltime job.
Ka ofisi kangu kako jengo la NHC, kodi tuu pekee ya pango ninayolipa NHC kila mwezi ni zaidi ya mshahara wa Mhe., Bwana DC, ukijumlisha na mishahara ya vijana wangu, nikiwa kwenye peak time, naweza kuwalipa mishahara ma DC watano!.


Ila pia lazima nikiri kuwa tofauti ya mimi na DC ni mamlaka na marupurupu, nikimaanisha kuna watu kibao wanapato kipato kikubwa kuliko rais wa JMT, na wanaweza kuwaajiri watu kibao na kuwalipa hata zaidi ya rais wetu anavyolipwa, lakini ukweli unabaki kuwa rais wetu ni mtu muhimu nambari moja kwa taifa hili, RC ndio raia namba moja wa mkoa husika, na DC ndie raia number moja wa wilaya husika!.

Acheni hizo!.

Paskali
 
We needed him so much.
We have him now,ila wengine wataumia.

Na huku kwetu kunaukaguzi wa vyeti vya kitaaluma aka kukagua wafanyakazi halisi kuepusha malipo hewa.
 
1)Mimi ni rais wa wote
2) Watanzania mniombee
3) Watanzania mnatakiwa mfurahie nchi yenu

Alichokizungumza Tabata Kinyerezi ndio rangi halisi

Kipande hiki toka kwa Mwita

"Baadae alimkaribisha Raisi aliyekuja na kituko cha mwaka. Aliendelea kutambulisha mabalozi na wawekezaji, mkewe, mbunge Zungu (Ilala), mbunge Kessy (Nkasi Kaskazini) akamruka Anatropia wa CDM, akamwita mbele mbunge Bona na kumsifia sana akisema kwamba wananchi wa Segerea walifanya vizuri kuchagua mbunge wa ccm kama na yeye alivyo wa ccm na kwamba kwa kufanya hivyo watapata maendeleo kwa sababu ati hawezi kumpa mtoto wa jirani chakula wakati wakwake yupo!

Kama hiyo haikutosha akampa nafasi ya kusalimia wananchi! Haikuishia hapo akasema amemchagua mkuu wa mkoa Makonda kwa vile ni mchapakazi na kwamba wengine walikuwa wakigombana naye na kujidai kukataa fedha za maendeleo sasa yeye kampa ukuu wa mkoa awe bosi wao sasa aone "
 
simuelewagi
ila nisemee clouds kuna vipindi vyake vizuri sana sana sanaa japo kuna vingine watangazaji anaenda pale wakiwa mitungi wanaongea utumbo esp kibonde
 
Isije kuwa ndio Mesi wa MMM katika bandiko lake jipya la ngeli, manake Pasco umewagusa wanaotaka kuamisha magoli lakini ni wakati sasa kukubali japo kwa wakati huu mdogo kwamba JPM ameanza vyema bado yuko relini. Nakubaliana na wewe kwamba jamaa ni mwenzetu na ametokana miongoni mwetu hana mbwata wala kunyanyua makwapa.

Akiwa kazini anamaanisha kazi tu!
 
Hutuba yake jana pale Kinyerezi(mitambo ya tanesco) imenifumbua macho kuwa kumbe Pombe ni rais wa wana ccm tu, na sio wa watanzania wote kama ambavyo huwa ajipambanua. Maana alionyesha yaliyo moyoni mwake, kuwa kwa yeye atahudumia majimbo yenye wabunge wa ccm pekee
 
Wanabodi,

Kadri siku zinavyokwenda, ndivyo Rais John Pombe Magufuli anavyozidi kuzikonga nyonyo za Watanzania, wanaopenda reality, simplicity, genuinity na down to earth, ndivyo wanavyozidi kumkubali huyu jamaa, na kitendo cha leo kupiga simu kwenye kipindi cha Clouds TV cha 360, ndio kimenimaliza kabisa!.

Japo Magufuli ni kiongozi dikiteta na katili na asiye na huruma kabisa, na mafisadi, wabadhirifu na walarushwa, lakini udikiteta wake ni a Benevolent Dictator, na Magufuli huyo huyo pia ni very genuine, very truthfully, ni mtu wa reality na very down to earth!.

Wanasiasa wengi sio genuine ni ma actors tuu wakijifanya wanajali matatizo ya wananchi ili tuu waonekane wanajali for political gain kupata political mileage, ila in reality na genuinity hawajali kitu, lakini Magufuli ni very real na very genuine!. Just imagine jinsi Balozi Sefue ilivyojituma kumtumikia Magufuli kwa karibu, lakini faili la madudu ya Sefue lilipotua tuu mezani kwa Magufuli, bila kukopesha wala kupepesa alilitumbua tuu hilo jipu, japo huu ni ukatili, realty na genuinity ilimfanya Magufuli kufanya kweli bila kukopesha, hivyo huu ni uthibitisho, this man is for real!.

Kimadaraka Rais ndie top citizen number 1, yuko top kule juu kabisa kwenyo top seat, kwenye kilele cha top power mountain, akiwa amezungukwa na wasaidizi, watumishi, washauri, walinzi, wapambe, etc, hivyo aje kushuka mpaka kuwafikia watu wa chini kabisa ni shughuli, lakini Magufuli huyu, anaangalia TV, anachukua simu, anawapigia waendesha kipindi ambao ni watu wa kawaida kabisa, anazungumza nao, anawapongeza, hii ni uthibitisho Magufuli sio mtu anayejisikia, ni mtu simple na down to earth, kitendo hiki kinatifanya sisi wananchi wa kawaida kumuona Magufuli, japo ni rais wetu, ila pia ni mwenzetu!.

Pongezi zake kwa Clouds Media pia zimetuma ujumbe mzito silently kwa TBC ambayo ndio TV yake na Redio Yake, kama Rais anatazama TV ya watu wengine na kuipongeza kwa kazi nzuri, vipi kuhusu TV yake?!, Kama rais hatazami TBC, na badala yake anatazama Clouds TV, na kuipongeza, then nani anataza TBC?!. Kitendo cha mwenye TV kutoiangalia TV yako, kinatuma ujumbe kuwa jee kuna uwezekano rais haangalii TBC kwa sababu inaboa!, hivyo anaangalia Clouds kwa sababu imechangamka, ndio maana amaipigia simu kuipongeza?, au kunauwezekano, rais anaangalia Clouds TV na pia anaangalia tv nyingine ikiwemo TV yake ya TBC, na TBC pia inafanya vizuri, inastahili pongezi za rais, lakini kwa kufuata kanubi ya usijisifu, bali subiri kusifiwa, then hata TBC ifanye vizuri kiasi gani, haistahili kusifiwa na rais, bali Clouds ndio imestahili kwa sababu imefanya viruri kuliko ilivyotarajiwa?!

Au pia inawezekana ni ni tabia tuu na yale mazoea ya mtu kudharau chake na kuthamini cha mwenzie?!.

Hongera sana Rais Dr. John Pombe Magufuli japo ni dictator , ni benevolent dictator, hongera sana for reality, simplicity, genuinity na being down to earth, you are just A man of the people!.


Pasco.
NB-Rejea.Kwa vile humu jf kilasiku kuna wageni, kuna watu wanaweza kudhania bandiko hili ni la kujipendekeza kwa rais Magufuli, hivyo nawawekea rejea kuwa Magufuli, sijaanza kumzungumzia leo, na yote niliyozungumza nyuma bado sijabadili kitu chochote!.
Magufuli Kama Nyerere:Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 ni John Pombe Magufuli.

Yajue Makundi 10 Top Ten wa CCM, Ambamo Watatoa Top 5, Top 3 na Rais wa 5 wa JMT.
Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli,...
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa ku

ENL, CHADEMA na UKAWA, Tuyakubali Matokeo!,

Pasco

Pasco
Terrible font! Unalazimisha kukuelewa? Next time you can present your views like a miss Barack Obama street 1
 
Hapa kwa kweli ndo na mm napoona anakosea,viongoz wanapaswa kujua kuwa nchi itajengwa na watu wote na ukawa wapo na ni watu smart sana na wako kila sehemu, inawezekana hata ikulu wapo ni watu wanaomin kwenye mabadiliko, hata vyuoni watu smart wengi ni wapinzani, hawa wenzenu wengi ni watu walionufaika tu na mfumo basi, kifupi hakuna wanachojua. Hebu mh. aachane na mambo ya ccm, kuna watu wengine ukitaja ccm mtu anackia kichefuchefu kabisa, sababu ni watu wanaojifanya kuunganisha nguvu ili baadae wakumbukwe, au biashara zao zisiguswe, sasa namna hii hatuwez kwenda hata rais angetoka mbinguni

1)Mimi ni rais wa wote
2) Watanzania mniombee
3) Watanzania mnatakiwa mfurahie nchi yenu

Alichokizungumza Tabata Kinyerezi ndio rangi halisi

Kipande hiki toka kwa Mwita

"Baadae alimkaribisha Raisi aliyekuja na kituko cha mwaka. Aliendelea kutambulisha mabalozi na wawekezaji, mkewe, mbunge Zungu (Ilala), mbunge Kessy (Nkasi Kaskazini) akamruka Anatropia wa CDM, akamwita mbele mbunge Bona na kumsifia sana akisema kwamba wananchi wa Segerea walifanya vizuri kuchagua mbunge wa ccm kama na yeye alivyo wa ccm na kwamba kwa kufanya hivyo watapata maendeleo kwa sababu ati hawezi kumpa mtoto wa jirani chakula wakati wakwake yupo!

Kama hiyo haikutosha akampa nafasi ya kusalimia wananchi! Haikuishia hapo akasema amemchagua mkuu wa mkoa Makonda kwa vile ni mchapakazi na kwamba wengine walikuwa wakigombana naye na kujidai kukataa fedha za maendeleo sasa yeye kampa ukuu wa mkoa awe bosi wao sasa aone "
 
Back
Top Bottom