Balozi Nchimbi: Kazi kubwa anayoifanya Rais Samia ni moja ya kumuenzi na kumheshimisha Hayati Magufuli

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Aug 29, 2022
228
556
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesema kazi kubwa anayoifanya Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiyo namna sahihi ya kumuenzi na kumheshimisha Hayati Dkt. John Joseph Pombe Magufuli.

Balozi Nchimbi amezitaja mojawapo ya kazi hizo kubwa zilizofanywa na na Rais Samia kuwa ni kuendeleza na kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya kitaifa kwa ujumla na mingine katika Mkoa wa Geita na Wilaya ya Chato, iliyoanzishwa wakati wa uongozi wa Rais Magufuli.

Katibu Mkuu wa CCM amesema hayo jana August 11, 2024, wakati wa sala fupi ya kumuombea Hayati Magufuli iliyofanyika kwenye kaburi la Kiongozi huyo.

Balozi Nchimbi amerejea maneno yake hayo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Stendi ya Zamani, Mjini Chato, akitaja baadhi ya miradi, ikiwemo ujenzi wa Treni ya Kisasa (SGR), Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere na jinsi ambavyo Serikali inayoongozwa na Rais Samia imeshusha kiasi cha TSh. bilioni 123 kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Chato.
.
“Sote ni Mashahidi na tunatambua mchango mkubwa wa Hayati Magufuli kwa Chama chetu na Nchi yetu, kazi hiyo kubwa aliyofanya iliashiria uzalendo mkubwa aliokuwa nao, nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais Samia kwa kuendeleza miradi yote iliyoachwa na hayati Magufuli, kama kuna kitu kizuri katika kumuenzi na kuendeleza kazi kubwa ya Hayati Magufuli ilikuwa ni kuendeleza na kumaliza miradi mbalimbali mikubwa, hiyo imekuwa ni heshima kubwa kwake Hayati Magufuli, miradi imeendelezwa na kufanyiwa kazi kama ilivyokuwa ndoto zake”
 
Hawadanganyiki hao
 
Aisee ila wakati mnaingia madarakani kazi ilikua moja tu kumpa kila lililo baya.
 
Na kweli tunaona utekaji, utesaji, watu kupotezwa na kuuwawa ndiyo order of the day
 
Ni kweli. Amemuenzi Mwenda zake kwa kuendeleza aliyoyaasisi ikiwemo kuteka watu, kukamata wapinzani wake na leo ameenda mbali Zaidi amezuia mikutano ya hadhara hadi mikutano ya ndani. Amekuwa Dikteta namba 2 baada ya Dikteta namba moja kuondolewa na Mungu kwa kutesa na kuua watu hovyo. Kilichobaki kwake kwa sasa ni kuvunja rekodi ya mtangulizi wake kwa kuanza na yeye kuua na kutesa watu.
Mungu tu atuokoe km alivyotuokoa mwanzo. Watanzania hatuna Umoja wala uwezo wa kuyakabili mateso Haya. Tunamuachia Mungu tu.
 
Siku zake za mwishoni akiwa pale mbezi alipolalamikiwa suala la bei ya 500 kwenye choo cha stand akasema “ Kama hutaki kutoa 500 baki na mavi yako”...😜🤣
 
Back
Top Bottom