Rais Magufuli ni muumini sana wa "quantity" na siyo "quality"

Rais Magufuli ni muumini sana wa "quantity" na siyo "quality"

Kwa hiyo ulitakaje labda kitokee, kwamba hawa watoto ni bora wake nyumbani mpaka hiyo unayoiita Elimu bora ipatikane au ni vipi?
Swali zuri hili.
lakin pia tujiulize kuna tofauti gani kati ya yule anayekaa nyumbani na yule anayemaliza darasa la 7 bila kujua kusoma na kuandika?
 
Wakuu,

Nimemsikia Rais Magufuli jana akihutubia wafanyakazi kuna vitu niliviona haviko sawa kabisa na wala sio vya kujisifia kwa uwingi wake.

1. "Viwanda zaidi ya 3000 vimeanzishwa tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani"

Sioni kama wingi wa viwanda hivi una tija ilhali ni viwanda vidogo vidogo kama vyerehani, blenda, saloon n.k sometimes unaweza kuwa na viwanda kumi tu vyenye tija vitakavyotoa ajira lukuki kwa wananchi.

2. "Wanafunzi zaidi ya milioni moja (alisema milioni moja mpaka mbili) wameandikishwa kujiunga na shule kutokana na elimu bure".

Hapa ndipo nilipochoka kabisa kumsikiliza.

1. Kuongezeka kwa wanafunzi, je Serikali imeongeza kiasi cha pesa kinachopelekwa shuleni?

2. Kuongezeka kwa wanafunzi takribani milioni mbili, je Serikali imeajiri walimu wangapi kuendana na ongezeko hili?

Quantitatively, wanafunzi wameongezeka ila ubora wa elimu ni lazima uporomoke Mara kumi zaidi.Imagine, mwalimu mmoja atahudumia wanafunzi wangapi?

Vitu vingine sio vya kujisifia kabisa.
JK alipeleka wanafunzi wasomee ualimu udom . jamaa kawafutilia mbali sidhani kama ile deficit ya walimu imekuwa covered mpaka sasa.....
 
Swali zuri hili.
lakin pia tujiulize kuna tofauti gani kati ya yule anayekaa nyumbani na yule anayemaliza darasa la 7 bila kujua kusoma na kuandika?

Tofauti ipo kbwa sana, ni bora mtoto aende shuleni hata kucheza tu na wenzake kuliko ashinde nyumbani kuanzia asubuhi mpaka jioni, kuna kitu atajifunza maadamu yuko shuleni hata tu nidhamu, kucheza na wengine, kufagia na kupanga madawati vyote hivi vitamsaidia kwa namna moja au nyingine maishani mwake klk kukaa nyumbani.

Binafsi kuna mambo nilifunza Shuleni nje ya darasani ambayo mpaka leo nayakumbuka na yananisaidia maishani mwangu!
 
Ni lazima ningetoa ajira kwa walimu na kupunguza kununua mapangaboi na kusimamisha ujenzi wa uwanja wa ndege chato.

Hao Walimu ungewatoa wapi? Kwa maana Walimu waliopo hawatoshi kukidhi haja ya watoto wote, Watoto ni wengi sana kuliko Walimu hivyo ni lazima kwanza ufundishe Walimu wapya na hilo linachukuwa muda, sasa wakati unasubiri Walimu wafuzu hawa watoto ungefanya nao nini?
 
Ange Balance kwakua Hpo mwanzo Tu Mtoto kabla yake pamoja na elimu ilkua sio Bure lakin kuna wakat mwanafunzi anafika mpka lasaba hajui Kuandka vzr hata jina lake hyo ni kutokana na Uchache wa walimu mishahara duni ya kukatisha tamaa walimu na pia Vitendea kazi Duni kabisa navyo pia ni vichache mnoo..Sasa pata Picha wanafunzi wameongezeka wengi alfu hakufanya balnsing Ya Kuongeza walimu ambao ni sawa na kuongeza nguvu kazi Ya kukabiliana na Ongezeko hilo au hata kupandisha mshahara yao ili kuwapa morali wafanye kazi yao kwa welidi na juhd kubwa..Sasa kwa Uelewa wako hpo Huoni wanafunzi weng watakua wanapta elimu duni ambyo ni sawsawa mtu ambaye hajasoma na kama in short ndo Kaua kabisa Sector ya elimu

Taizo ni kwamba hao Walimu hawapo! Hivyo ni lazima kwanza kuwapata na hili ni lazima walimu wafundishwe kwanza, sasa wakati unaelimisha Walimu hawa watoto unafanyanao nini?
Isitoshe kabla ya sisi kununua Ndege Je, watoto wote walikuwa wanakwenda Shuleni na kupata Elimu bora kama tatizo ni Ndege?
 
Ujasikia akiwambia wanafunzi eti kusoma sio kujua kiingereza? Eti private wanachuwaja, serikali inawapenda wanafunzi wote hakuna kuwachuja ili mradi walikanyaga darasani kha! Nimechoka kabisa.

Hii ni defensive mechanism. Sijui Samia asingekuwa anajua kiingereza ingekuwaje. Angeenda kwenye mikutano ya watu na kiswahili cha kizenji?
luckliney
 
Kwa hiyo ulitakaje labda kitokee, kwamba hawa watoto ni bora wake nyumbani mpaka hiyo unayoiita Elimu bora ipatikane au ni vipi?

Idadi ya wasiojua kusoma na kuandika imeongezeka sasa hata kabla yeye hajaingia madarakani. Je kwa kipindi hiki idadi ya kubwa kuongezeka ya wanafunzi na hakuna maandalizi yoyote. Je unategemea wanafunzi watapata kilicho bora kwenye elimu? Na idadi ya wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika haitaongezeka?
 
Wanafunzi zaidi ya milioni moja (alisema milioni moja mpaka mbili) wameandikishwa kujiunga na shule kutokana na elimu bure".

Hapa ndipo nilipochoka kabisa kumsikiliza.

1. Kuongezeka kwa wanafunzi, je Serikali imeongeza kiasi cha pesa kinachopelekwa shuleni?

2. Kuongezeka kwa wanafunzi takribani milioni mbili, je Serikali imeajiri walimu wangapi kuendana na ongezeko hili?
Hivi kweli unaamini hizo statistics. Kama ni kweli hiyo idadi (100 %) imeongezeka awamu hii ina maana karibu nusu ya Watanzania walikuwa hawaendi shule!! Then almost 50 % hawajui kusoma na kuandika kwa kuwa hawakuwa na access na elementary education.
 
Sasa Mkuu amepewa na ameziamini, ndio maana anajitapa
 
Haujajibu swali langu, ingekuwa wewe ungefanyaje katika hali kama hiyo, ungewaacha watoto nyumbani mpaka uweze kupata Walimu wa kutosha? Au ungefanyaje?

Swali rahisi mno. Kwa nchi kama yetu hakuna legacy ya maana kuliko elimu bora, huduma bora za afya na wakulima wanaozalisha kwa tija. Waalimu wako mtaani hawana ajira! Hakuna uwezo wa kuajiri waalimu kwa sababu sehemu kubwa ya bajeti ya serikali imeelekezwa kwenye maendeleo ya vitu badala ya maendeleo ya watu; reli, barabara, viwanja vya ndege, ndege, nk. Kupanga ni kuchagua. We are biting more than we can chew. Miundombinu inaweza kusubiri, lakini elimu ya watoto haiwezi kusubiri. Kwa hakika Stiegler's gorge inaweza kusubiri watoto wetu wakasoma. Nadhani hii ndiyo maana ya Ilani ya ccm kutoa elimu bure hadi sekondari; siyo kuandikisha tu wakacheze shuleni.
 
Siyo kweli kwamba kuna Walimu wa kutosha kwa sasa, huo ni Uongo!
 
Taizo ni kwamba hao Walimu hawapo! Hivyo ni lazima kwanza kuwapata na hili ni lazima walimu wafundishwe kwanza, sasa wakati unaelimisha Walimu hawa watoto unafanyanao nini?
Isitoshe kabla ya sisi kununua Ndege Je, watoto wote walikuwa wanakwenda Shuleni na kupata Elimu bora kama tatizo ni Ndege?
Bro Sizan Kama Hii Unacho Ongea umefanyia Uchunguzi Wa Kina Nacho Famahu Kuna Walimu Wengi Sana Ambao hawajapatiwa ajira kwanzia Walio Hitimu 2015 mpka leo na Kumbuka Vyuo Vinatema wahitimu wa Uwalimu takriban 4000 kila Mwaka Na Piga Hesabu toka 2015 mpaka leo wote hao hawana Ajira Na Tatizo Sio kua Walimhawapo tatizo ni Hajira hmna Kwa Ajili yao kwa kipind Kirefu Sasa
 
Back
Top Bottom