Rais Magufuli ni muumini sana wa "quantity" na siyo "quality"

Rais Magufuli ni muumini sana wa "quantity" na siyo "quality"

herzegovina

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2015
Posts
3,155
Reaction score
4,744
Wakuu,

Nimemsikia Rais Magufuli jana akihutubia wafanyakazi kuna vitu niliviona haviko sawa kabisa na wala sio vya kujisifia kwa uwingi wake.

1. "Viwanda zaidi ya 3000 vimeanzishwa tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani"

Sioni kama wingi wa viwanda hivi una tija ilhali ni viwanda vidogo vidogo kama vyerehani, blenda, saloon n.k sometimes unaweza kuwa na viwanda kumi tu vyenye tija vitakavyotoa ajira lukuki kwa wananchi.

2. "Wanafunzi zaidi ya milioni moja (alisema milioni moja mpaka mbili) wameandikishwa kujiunga na shule kutokana na elimu bure".

Hapa ndipo nilipochoka kabisa kumsikiliza.

1. Kuongezeka kwa wanafunzi, je Serikali imeongeza kiasi cha pesa kinachopelekwa shuleni?

2. Kuongezeka kwa wanafunzi takribani milioni mbili, je Serikali imeajiri walimu wangapi kuendana na ongezeko hili?

Quantitatively, wanafunzi wameongezeka ila ubora wa elimu ni lazima uporomoke Mara kumi zaidi.Imagine, mwalimu mmoja atahudumia wanafunzi wangapi?

Vitu vingine sio vya kujisifia kabisa.
 
.ye huwa anaangalia kitu kinenunuliwa ama la....tena bila kujali kimenunuliwa kifisadi ama la!...ndio maana alinunua ile boti feki ya bagamoyo ikafa kabla hata haijatumika....achilia mbali ma bombardier feki anayojitapa kuyanunua kwa cash...naskia yameshaanza kufa...
..huwa najiuliza huyu jamaa nani huwa anamshauri...ama anatumia akili gani kufanya maamuzi??....so sad yani...ama ndio ile issue ya ushamba wa kisukuma alosema zitto???...maamuzi mengi ya mhutu yana walakini...
 
herzegovina Kwa hiyo ulitakaje labda kitokee, kwamba hawa watoto ni bora wake nyumbani mpaka hiyo unayoiita Elimu bora ipatikane au ni vipi?
 
Ujasikia akiwambia wanafunzi eti kusoma sio kujua kiingereza? Eti private wanachuwaja, serikali inawapenda wanafunzi wote hakuna kuwachuja ili mradi walikanyaga darasani kha! Nimechoka kabisa.

Hii ni defensive mechanism. Sijui Samia asingekuwa anajua kiingereza ingekuwaje. Angeenda kwenye mikutano ya watu na kiswahili cha kizenji?
 
Awamu Hii sio ya ki-sport sport....

WAPINZANI MTAISOMA NAMBA
Screenshot_2018-04-30-18-13-58.jpg
 
Kwa hiyo ulitakaje labda kitokee, kwamba hawa watoto ni bora wake nyumbani mpaka hiyo unayoiita Elimu bora ipatikane au ni vipi?
Unaandikisha watoto wengi halafu walimu hakuna....[HASHTAG]#shame[/HASHTAG]
 
Ujasikia akiwambia wanafunzi eti kusoma sio kujua kiingereza? Eti private wanachuwaja, serikali inawapenda wanafunzi wote hakuna kuwachuja ili mradi walikanyaga darasani kha! Nimechoka kabisa.

Hii ni defensive mechanism. Sijui Samia asingekuwa anajua kiingereza ingekuwaje. Angeenda kwenye mikutano ya watu na kiswahili cha kizenji?
Yani huyu jamaa akili zake anazijua mwenyew kwa kweli.
 
Unaandikisha watoto wengi halafu walimu hakuna....[HASHTAG]#shame[/HASHTAG]


Haujajibu swali langu, ingekuwa wewe ungefanyaje katika hali kama hiyo, ungewaacha watoto nyumbani mpaka uweze kupata Walimu wa kutosha? Au ungefanyaje?
 
Ni tatizo sana kwa huyu bwanamkubwa,not only that but also ni muimini wa vitu badala ya hali,ndo maana haishi kutafutiza vya kuzindua
 
Nchi inasonga nyie pigeni soga Magufuli proves that visivyowezekana vinawezekana[emoji91][emoji91][emoji91]
 
Nadhani wanampa tu na yeye akishaona zinamletea sifa anazipokea na kujitapa nazo bila kupima
Ndio hapo wameshajua weakness yake ni "kusifiwa". Wanajua hata wakimlisha report za uongo ambazo zita mridhisha basi wata zid kubaki kwenye mafasi zao.
 
juzi juzi tu mlikuwa mnachukia walimu wa sekondari kuhamishiwa shule za msingi.
 
Haujajibu swali langu, ingekuwa wewe ungefanyaje katika hali kama hiyo, ungewaacha watoto nyumbani mpaka uweze kupata Walimu wa kutosha? Au ungefanyaje?

Ange Balance kwakua Hpo mwanzo Tu Mtoto kabla yake pamoja na elimu ilkua sio Bure lakin kuna wakat mwanafunzi anafika mpka lasaba hajui Kuandka vzr hata jina lake hyo ni kutokana na Uchache wa walimu mishahara duni ya kukatisha tamaa walimu na pia Vitendea kazi Duni kabisa navyo pia ni vichache mnoo..

Sasa pata Picha wanafunzi wameongezeka wengi alfu hakufanya balnsing Ya Kuongeza walimu ambao ni sawa na kuongeza nguvu kazi Ya kukabiliana na Ongezeko hilo au hata kupandisha mshahara yao ili kuwapa morali wafanye kazi yao kwa welidi na juhd kubwa..

Sasa kwa Uelewa wako hpo Huoni wanafunzi weng watakua wanapta elimu duni ambyo ni sawsawa mtu ambaye hajasoma na kama in short ndo Kaua kabisa Sector ya elimu
 
Haujajibu swali langu, ingekuwa wewe ungefanyaje katika hali kama hiyo, ungewaacha watoto nyumbani mpaka uweze kupata Walimu wa kutosha? Au ungefanyaje?
Ni lazima ningetoa ajira kwa walimu na kupunguza kununua mapangaboi na kusimamisha ujenzi wa uwanja wa ndege chato.
 
...... AMESOMA SANA OPTIMIZATION (LINEAR PROGRAMMING & THE LIKE) LAKINI AKAAMUA KUPASI MITIHANI YAKE NA KUVIACHA HUKOHUKO!
TUNAZIDI KUMUOMBEA MUNGU AMUANGAZIE NA HUKO, MAANA MAENDELEO YA VITU YAKIWAACHA BINAADAM NYUMA NI 'WORK DONE NEGATIVE'!
Hawa ni wale wazee wa kukremu tu, akishapata cheti anasahau vyote
 
Back
Top Bottom