Rais Magufuli ni dira ya maendeleo barani Afrika

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,395
3,901
YASHUHUDIE MAAJABU YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO INAYOJENGA VIPYA PAMOJA NA KUFUFUA VILIVYOKUFA:

Uongozi wa nchi ni sawa na fumbo la imani. Hakuna awezaye kujua kesho atakuwa nani isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee ndiye mwenye ufunguo kwa kila mja wake. Unaweza ukawa na wazo, nia pamoja na malengo ya kuongoza nchi lakini endapo Mungu hajaweka mkono wake, basi wewe wafanya kazi bure.

Hivyo ndivyo Mungu alivyomwinua Daudi, kijana mdogo tena aliyekuwa mchunga kondoo, lakini alimpa nguvu na uwezo wa kumshinda Goliati, jitu la miraba minne lililokuwa likiogopwa na kila mtu. Hivyo ndivyo Mungu alivyomwinua Daudi kutoka kuwa mchunga kondoo hadi kuwa mfalme.

Pengine kwa wewe mtanzania mwenzangu, kama nilivyo mimi, inawezekana tusiamini kwamba, usafiri wa reli ya kutoka Dar hadi Tanga na Moshi uliokufa kwa zaidi ya miaka 25 iliyopita, sasa umefufuliwa kwenye serikali hii ya awamu ya tano ndani ya miaka 4 tu.

Kwa wale tunaofuatilia maendeleo ya nchi hii kwa sasa, ni kwamba, usafiri kwa njia ya reli kutoka Dar es Salaam kwenda Tanga hadi Moshi ulikufa kabisa. Kilichokuwa kimebakia ni utake usitake lazima usafiri kwa kutumia bus na kwa wale wenye mizigo, tegemeo pekee lililobakia ni malori. Kutokana na kufa kwa usafiri wa reli, bei za bidhaa nyingi zilipanda baada ya malori kubakia tegemeo pekee la uchukuzi huku kila mwaka abiria wakilazimika kulanguliwa tiketi kwa bei ya juu kwenda mikoa ya kaskazini.

Itoshe tu niwakumbushe kwamba, mapema tarehe 20th July, mwaka huu 2019 baada ya kukamilika kwa ukarabati wa reli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alishuhudia kuwasili kwa treini ya mizigo ya kwanza iliyokuwa imebeba mabehewa 20 ya saruji kutoka kiwanda cha Saruji Tanga.

Sanjari na kuwasili kwa shehena hiyo, kesho tarehe 06th Dec,2019, treini ya kwanza ya abiria ambayo ni rasmi itaanza safari zake kutoka Dar es Salaam kwenda Moshi tena unaambiwa kwa nauli kiduchu ikilinganishwa na nauli ya mabus. Kumbuka hapo juzi kulifanyika safari ya majaribio ya trein ya abiria ya mabehewa 6 ambayo ilipokelewa na wakazi wa Moshi kwa shangwe na nderemo.

Sina namna yoyote ninayoweza kuificha furaha yangu kuhusu utendaji wa serikali hii, hususani katika swala la kutoa huduma za kijamii kwa wananchi ikiwemo usafiri wa reli uliokuwa umekufa kabisa.

Nitowe wito kwa yule mwana siasa uchwara aliyeishiwa sera, macho kumchuzi aliyedai kwamba serikali ya awamu ya tano imewaumiza watu wa kaskazini, sasa ajitokeze na kuwaambia wapiga kura wake iwapo trein hii iliyofufuliwa, inakwenda kaskazini au inakwenda Chato?

Mwisho niiombe serikali kwa kushirikiana na wananchi, iimarishe ulinzi wa miundombinu ya reli iliyofufuliwa. Hii ni kwa sababu kuuawa kwa reli kulitokana na sababu za kiuchumi ambazo hadi sasa bado zipo hususani wafanya biashara binafsi waweze kutumia malori kujinufaisha

#Magufuli2035
 
Ni wajibu wake asipofanya tutamuhukumu lakini hata akifanya si kigezo pekee cha kuendelea, itategemea anayeshindana naye atakuja na sera zipi?

Mshindani wake akisema atakomesha kuua,kuteka, kutesa, kupora hela na kuweka watu mahabusu kwa uonevu tutamchagua huyo.
 
Haya hata tungebakia na mkoloni angetufanyia. Sisi tunataka demokrasia na Uhuru wa kutoa mawazo
 
Maendeleo hayaletwi na mtu mmoja wala serikali. Tunahitaji uiengwe mifumo wezeshi ambayo itamfanya kila mmoja ajenge uchumi wake binafsi na kuchangia ujenzi wa uchumi wa Taifa.

Kilichofanyika siyo kitu cha pekee wala ajabu. Kama ni kusifiwa kwaajili ya reli, tumsifu zaidi aliyejenga hiyo reli kuliko anayekarabati. Japo tunastahili kumlaani aliyeshindwa kuitunza.

Suti nzuri, asifiwe aliyeiunda au aliyeshona ilipotatuka?

Daraja la Busisi bilioni 700, ukarabati wa reli bilioni 3. Halafu wa bilioni 3 aone amethaminiwa sana na kupendelewa. Hapo ni lazima uwe mjinga wa kudumu. Ukiona mtoto amechukua noti ya sh 10,000 na ameing'ang'ania, unaweza kumpa pipi, nawe utachukua 10,000 kiurahisi maana mtoto ataona amependelewa kwa kupewa pipi tamu kumbe dhamira ni kuichukua 10,000.

Kwa leo itoshe kusema hivyo lakini mjue kuna mpango mkakati maalum wa kuiinua kanda. Na mbinu itakayotumika, kwanza ni kupeleke vitu vidogo vidogo kanda nyingine ili wapumbazike, halafu kilichokusudiwa kinapelekwa kanda inayostahili kujengwa. Endeleeni kufuatilia kuanzia sasa, hamtahitaji kuhubiriwa, kila mwenye akili atashuhudia mwenyewe. Awezaye autunze mchango huu. Ni habari ya jikoni ambayo uthibitisho wake ni kadiri siku zitakavyoenda.
 
Back
Top Bottom