Rais Magufuli: Namshukuru Waziri wa Nishati na Madini kwa kutengua upandishaji wa bei ya umeme

Huu kama mchezo wa kuigiza tu, ina maana ewura waliamua wao wenyewe kupandisha bei ya umeme bila waziri husika kuidhinisha au kujua?
Haya ni maamuzi baada ya kusoma upepo nje, kwa vile wanasiasa Ndio wasemaji, mzigo wote wanabeba watendaji Lakini mpango huu walikuwa wanaujua wote na wao Ndio waliokuwa wameupanga
Ewura ni chombo kinachojitegemea ndio maana kwenye sheria ya Nishati kuna kipengele kinachompa waziri mwenye dhamana kutengua maamuzi ya ewura. Kama ingekuwa waziri anashiriki kwenye maqmuzi hicho kipengele kisingewekwa.
 
Dah!!! Ya kufungulia mwaka hiyo...teh teh.
Lazima tujadiliwe kila wakati.
 
Yote uliyoongea sawa Mh Rais..

Lakini suala la KUKUOMBEA halipo tena.

Maana pale mwanzoni kabisa ulivyosema tukuombee.. tulikuombea sana.

Baada ya maombi yale ukazima bunge live.. ukazuia mikutano kwa vyama vya Siasa... kukamatwa kwa watu mbalimbali wanaotoa hoja tofauti na mwelekeo unaoutaka wewe..uchumi kuparanganyika nk nk.

Naona twende kimya kimya tu.

Siafiki tena kukuombea yasije yakatokea makubwa zaidi.
 
Ina maana walikuwa wapi wakati bei mpya inapendekezwa mpaka inapitishwa halafu wanakuja kutengua maamuzi, hii ni kutafuta sifa tu


RAIS amesema kwa kueleweka kabisa "haiwezekani serikali inapanga hivi , halafu MTU MMOJA anaamua kufanya VINGINE, ndio maana baba askofu ninasema BADO KUNA MAJIPU MENGI YA KUTUMBULIWA" sasa hapo usichoelewa ni nini? ina maana Bwana NGALAMGOSI KAKURUPUKA
 
Leo Januari Mosi 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amezungumzia kuhusu upandishaji wa bei za umeme na kusema anamshukuru sana Waziri wa Nishati na madini kwa kutengua upandishaji wa bei ya umeme. Hapa chini ni video iliyotolewa na YouTube channel ya Ikulu ikionyesha kwamba hata yeye Mh. Rais hakuafiki kabisa bei kupanda.


Mkurugenzi wa Ewura naona jipu lake limeshaiva
 
Safi sana,kitu linaamka tu asubuhi na kutangaza kupandisha umeme.tumbua huyo haraka.na watz wanafki sana ni nyie hao hao mngelalama bei ingepanda
 
Huyu prf mhongo nakubali sana shida yake ni uccm ndiounamualibia nimtu makini sana ila hayamajizi yaliko ccm ndio yanayohalibu mipango mizuli juu yataifahili ndiomaana nikasema mweshimiwa laisi magufuli asingekua ccm angetenda miujiza kwenyetaifa hili ila haya majizi yanamkwMisha .. Hata swala lasukali lilikwama hivyo hivyo maana majitu aliokua akipambana nayo yalikua yanatoka ndaniyachama chake nahapo kwenye sukari akafeli
 
Back
Top Bottom