Rais Magufuli: Namshukuru Waziri wa Nishati na Madini kwa kutengua upandishaji wa bei ya umeme

Huu kama mchezo wa kuigiza tu, ina maana ewura waliamua wao wenyewe kupandisha bei ya umeme bila waziri husika kuidhinisha au kujua?
Haya ni maamuzi baada ya kusoma upepo nje, kwa vile wanasiasa Ndio wasemaji, mzigo wote wanabeba watendaji Lakini mpango huu walikuwa wanaujua wote na wao Ndio waliokuwa wameupanga
Umeuliza Swali nzuri kwanza ungesema utaratibu wa kupandisha Umeme na maji ikoje
 
Ni yale yale mkuu wa mkoa kuagiza polisi kamata hawa na wasipewe dhamana hadi kesi iishe.
Kwani wakati EWURA wakiitisha mapendekezo ya wadau hawa watawala walikuwa wapi?
Tusidanganyane hizi ni picha za Kihindi.
Je unafahamu taratibu za ufanyaji kazi maofisini? EWURA wamepandisha bei kabla ya kuijulisha serikali, wameutangazia umma ndipo wakapeleka official notice kwa serikali. Na Waziri amefanyia kazi official notice aliyopewa. Badala ya kuwalaumu waziri na rais ungeanza kuwalaaumu EWURA kwa kufanya kazi kwa mazoea badala ya kufuata taratibu. Hii haina utofauti na ya Mkurugenzi wa NIMR
 
Hii nchi ngumu sana wezi wanataka kula tu peke yao.

Umeme unatakiwa ushuke hata hapo ulipo bado bei ni juu sana.

Hasa kama mnataka serikali ya viwanda.

Zaidi ya hapo itakuwa ni porojo tu.
nadhani kelele zetu humu jf zimesaidia kuwapa pressure. alafu eti fa.LA mmoja anataka jf ifungwe
 
Huyu prf mhongo nakubali sana shida yake ni uccm ndiounamualibia nimtu makini sana ila hayamajizi yaliko ccm ndio yanayohalibu mipango mizuli juu yataifahili ndiomaana nikasema mweshimiwa laisi magufuli asingekua ccm angetenda miujiza kwenyetaifa hili ila haya majizi yanamkwMisha .. Hata swala lasukali lilikwama hivyo hivyo maana majitu aliokua akipambana nayo yalikua yanatoka ndaniyachama chake nahapo kwenye sukari akafeli
Ni kweli ccm imeoza sana nawashangaa upande wa pili wanakomba uchafu uliotupwa na ccm halafu wanajiita wanaharakati.
 
Mh Rais amshukuru waziri wa nishati na madini kwa kuzuia kupanda kwa bei ya umeme nchini asema hakuna kupanda bei ya umeme wakati serekali inakusidia kupeleka umeme vijijini.

Chanzo: TBC 1
 
Masikini Nyamlagosi. Keshaitwa Jipu na punde tu watamtumbua. A stepping stone to raise their "acceptance rate".

Ukisoma report ya EWURA, mchakato ulikuwa wa wazi na wanadai kutangaxa kwenye gazeti la Serikali process yote. Why kina Muhongo hawakustopisha zoezi tangu mwanzo?

Maafisa huko serikalini poleni sana. Mnalo until atleast 2020. Tutakachofanya ni kuwaombea tu ili Mungu awape wepesi maana hakuna namna nyingine sasa.
 
Ngalamgosi kaingia choo cha kike, yani mukulu anapigania umeme ushuke yeye anapendekeza umeme upande, sasa huo ubishi wa kumbishia boss asubiri kupangiwa kazi nyingine.
Mkuu, wala Ngalamgosi hajaingia huko choo cha kike kwa utashi wake bali kaingizwa huko na kina Muhongo na Magufuli. Walikuwa wanamtegea na kaingia kingi kiulainiii.. Lakini ukisikiliza hiyo video unajiuliza ina maana Ngalamgosi aliwabishia Muhongo na Magufuli kuhusu bei ya umeme na akatangaza kivyake??? Ngoja nikatafute maana ya neno "Tanzania" kwenye kamusi!
 
Hii nchi ngumu sana wezi wanataka kula tu peke yao.

Umeme unatakiwa ushuke hata hapo ulipo bado bei ni juu sana.

Hasa kama mnataka serikali ya viwanda.

Zaidi ya hapo itakuwa ni porojo tu.
Nakuunga mkono hoja yako.
 
Hawa hawa Tanesko walikuwa wanamzimia umeme kipindi cha kampeni ili kuonesha kuwa CCM haifai.

Leo hii ni hawa hawa wanaotaka kupandisha umeme bila sababu zenye mashiko.

UKICHEKA NA NYANI UTAVUNA MABUA.
 
okraix.jpg
 
Back
Top Bottom