Rais Magufuli: Namshukuru Waziri wa Nishati na Madini kwa kutengua upandishaji wa bei ya umeme

Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,164
5,762
Leo Januari Mosi 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amezungumzia kuhusu upandishaji wa bei za umeme na kusema anamshukuru sana Waziri wa Nishati na madini kwa kutengua upandishaji wa bei ya umeme.

Hapa chini ni video iliyotolewa na YouTube channel ya Ikulu ikionyesha kwamba hata yeye Mh. Rais hakuafiki kabisa bei kupanda.



tmp_8472-_20170101_1530581561582375.JPG


Barua ya TANESCO:

IMG_2175.JPG

Ufafanuzi wa TANESCO baada ya kuibuka kelele za kupandishwa bei ya Umeme Jan 1, 2017​
IMG_2176.JPG

 
Huu kama mchezo wa kuigiza tu, ina maana ewura waliamua wao wenyewe kupandisha bei ya umeme bila waziri husika kuidhinisha au kujua?
Haya ni maamuzi baada ya kusoma upepo nje, kwa vile wanasiasa Ndio wasemaji, mzigo wote wanabeba watendaji Lakini mpango huu walikuwa wanaujua wote na wao Ndio waliokuwa wameupanga
 
Leo Januari Mosi 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amezungumzia kuhusu upandishaji wa bei za umeme na kusema anamshukuru sana Waziri wa Nishati na madini kwa kutengua upandishaji wa bei ya umeme. Hapa chini ni video iliyotolewa na YouTube channel ya Ikulu ikionyesha kwamba hata yeye Mh. Rais hakuafiki kabisa bei kupanda.


Ni yale yale mkuu wa mkoa kuagiza polisi kamata hawa na wasipewe dhamana hadi kesi iishe.
Kwani wakati EWURA wakiitisha mapendekezo ya wadau hawa watawala walikuwa wapi?
Tusidanganyane hizi ni picha za Kihindi.
 
Hii nchi ngumu sana wezi wanataka kula tu peke yao.......
ni mpango unaendelea wa kumsafisha muongo kwa wananchi aonekane anawajali watz,baada ya malalamiko ya muda mrefu kuhusu kashfa ya ESCROW kwamba hafai kuishika hiyo nafasi tena. Masikini nchi yangu tangu awamu hii ianze watawala wake wamegeuka watu wa matamko. na kama hajatumbuliwa mtu katika hili nitaendelea kuamini yule mama Dr. wa NIMRI kafanyiwa makusudi
 
Back
Top Bottom