Katika uchambuzi wa kisiasa, nchi imetolewa kutoka ktk udiktekta na kupelekwa ktk ufashisti.
Ufashisti unataka bunge linalotii mamlaka badala ya kuhoji serikali, matajiri wenye viwanda na biashara (National Bourgeoisie) kuunga juhudi, media kuimba na kusifu mamlaka, Miradi mikubwa ya Maendeleo ya Vitu ili watawala kudai hawataki kelele za haki uhuru na demokrasia ili watimize maendeleo ya vitu kwa haraka. Tanzania tayari imetoka ktk udiktekta uchwara na kurushwa ktk ufashisti November 2019 ilianza hatua hiyo na kuhitimishwa October 28 2020.
Hivyo nafasi ya kukutanisha utawala wa kifashisti na wananchi kama Tundu Antipas Lissu, wananchi great-thinkers waliopo Twitter na JamiiForums au katika vyuo vikuu vya wasomi wakutane na watawala walioifikisha nchi ktk utawala wa kifashisti haupo. Maana waumini wa ufashisti huwa hawasikilizi tena sauti mbadala nafasi hiyo ilikuwapo utawala ulipokuwa steji / hatua ya udiktekta-uchwara lakini CCM Mpya na wananchi wasiojua hila ya watawala hawa wamewapaisha madiktekta uchwara kwenda ktk ufashisti wakitumaini mambo yatakuwa mazuri.
Tutegemee kuona kibano zaidi ndani ya CCM Mpya kutafutana uchawi, National Bourgeoisie wenye viwanda / matajiri kukamuliwa zaidi kodi, maadui-maruhani kuibuliwa zaidi ya hawa mabeberu-ruhani, wasaliti-ruhani , wapinzani-ruhani ili utawala uliopo kijaribu kutimiza ahadi walizotoa (ambazo haziwezitimilika) katika hotuba ya Bungeni ktk bunge jipya lililoapishwa November 2020.
Kwa mfano suala la viwanda vya saruji simenti tayari vimeshaanza kusakamwa siyo na wizara ya viwanda bali mkono wa dola kupitia Polisi na wawakilishi wa wateuliwa wa mkuu wa nchi yani wakuu wa mikoa RC. Hizi ni rasharasha maana wenye viwanda hivi watabebeshwa lawama na viwanda vyao kutishiwa kutaifishwa kwa tuhuma za kuhujumu juhudi za mkuu wakati kuna sababu kubwa mfano umeme usiotosha kuendesha viwanda n.k
Pengine miradi mikubwa ya Maendeleo ya Vitu kama SGR Mpya, maDaraja, Stiegler's Gorge ilianzishwa na sementi yote kupelekwa huko kutokana na uzalishaji mdogo wa viwanda vya saruji nchini na sasa taifa limepungukiwa na fedha za kigeni kuagiza saruji hivyo uhaba sasa unaanza kuonekana si tu za fedha za kigeni za korosho bali na uchumi kwa ujumla kuyumbishwa kwa mipango ya kukurupuka.
Bunge jipya la Novemba ambapo wabunge wa CCM Mpya wameteuliwa na mtu mmoja tumeliona limeanza kwa kupiga makofi kila baada ya sentensi chache za Bwana Mkubwa, wateuliwa hawa (hawajachaguliwa na wananchi wala chama cha CCM) hawajiulizi ahadi za miradi mikubwa mipya juu ya anayo tayari ilianzishwa inaweza kumalizika ndani ya mitano mingine au 15 mingine na ndiyo maana waliteuliwa kwa gharama kubwa kwa Taifa kuua demokrasia, uhuru haki ili kisingizio 2025 apewe 15 mingine.