Rais Magufuli na Libya

Africa kusini haijawai kuongozwa kidicteta ila ni ubaguzi wa rangi
Kama mnavyojinasibu kwamba rais hawezi kutoka kasikazini
 
Badala ya kuonyesha mstari kwa mstari udhaifu wa hoja yangu/ zangu, unaishia kunishambulia mimi badala yake.

Wewe si tu huna hoja. Wewe ni dhaifu.

Tena dhaifu wa akili.

Miaka nenda rudi humu watu tunahubiri kuwa hoja hujibiwa kwa hoja.

Wewe hujafanya hivyo. Umejibu hoja kwa viroja!

Alamsiki.
 
Kwa kauli zako basi sisi waTz na wa Africa tunapotezewa muda na chaguzi zisizo real
Sio kwamba tunapoteza mda, vyama vingi vya upinzani havina dira. Utaona viongozi wao hawana tofauti na viongozi walioshika dola, na wao pia wanang'aninia vyeo vile vile. Vyama vinatumika kama kampuni binafsi, wanachama hawana nguvu ya kuhoji ndani ya vyama vyao vya siasa. Unategemea utapewa dola? Huo Uhuru mnaoutaka nyie uko wapi ndani ya vyama vyenu? Ukiwa muwazi utaona taswira ya vyama vya siasa vya upinzani, havina malengo ya Masafa marefu wao ni kutumia ruzuku tu.

Angalia Kenya Odinga anavyofanya, asipopendekezwa kugombea anaanzisha chama chake alafu anagombea urais. Angalia Uganda besigye ni mara ya ngapi kugombea urais, INA maana hamna mwingine ndani ya chama? Twende Zimbabwe Morgan ni mara ngapi anagombea urais, INA maana hakuna wengine? Huku kwetu kuna vyama mwenyeviti wamekua ni wa milele, wanachama hawapaswi kuhoji? Angalia leo CUF rafu zinavyofanyika, alafu upime mwenyewe. Demokrasia mnayoitaka kwenye uchaguzi mkuu huko kwenu IPO? Uhuru mnaoutaka huku uraiani huko ndani ya vyama vyenu upo?
Hakuna nchi au taasisi unayoweza kuwa huru tu bila ya kufata sheria husika. Haipo!
 
Unajua Nyani Ngabu, binadamu ni kiumbe wa tofauti sasa kwa watawala wetu kudhani kuwa wanaweza kutuweka kwenye "zoo" ni sawa na kujaribu kuonja sumu kwa kulamba.
 
Unajua Nyani Ngabu, binadamu ni kiumbe wa tofauti sasa kwa watawala wetu kudhani kuwa wanaweza kutuweka kwenye "zoo" ni sawa na kujaribu kuonja sumu kwa kulamba.
Yaani katika mataifa yote hapa duniani yeye mtukufu Ngosha Libya ndo ya kuitolea mfano?

Nchi iliyoongozwa na dikteta toka mwaka 1969 ndo nchi ya kuitolea mfano wa amani?

Mwenyewe huwa anasema alikaa huko kwa wiki mbili.

Au jamaa hajawahi kwenda nchi zingine zaidi ya Libya, Rwanda, Kenya na Uganda?

Manake tunaweza tukawa tunamlaumu bure kumbe mwenzetu hana ufunuo wa kutosha....
 
Mr. Silas kwa yote haya uliohoji unataka Malaika wa mbinguni ashuke kutuwekea mfumo mzuri wa kuongozana ?! Kwanini iwe kazi ya watu wengine na siyo sisi kukaa na kujiwekea utaratibu mzuri wa kufuata kufikia kuupata huo uongozi bila mizengwe hii inayotokea Africa ?!

Pia si sahihi kung'ang'ania kutokutenda haki kwa sababu mpinzani wako ana mapungufu unayoyaona wewe ni vema wananchi wakahukumu na si system
 
Kwa hiyo kusigana Katiba ndiyo kitu sahihi kwako?
 
 
Hatuwezi kuwa na demokrasia kama taasisi za siasa hazifati demokrasia. Hii ni kwa chama vyote tawala na upinzani. Lakini vyama vya upinzani wana nafasi ya kuonesha jamii kuwa wako tofauti na chama tawala. Lakini hakuna tofauti iliyopo kati ya vyama tawala na vyama pinzani.
Hapo ndo kuna kosa, jamii ni kama ombwe.Huwezi kuwaachia waamue wenyewe, hii ni kanuni duniani kote. Ukiacha wananchi waamue hata leo diamond platinum akingombea urais atampita yule mama wa act kwa kura. Sasa shida yote ya nini, ni lazima kuwa na vigezo
 
Kwa hiyo kusigana Katiba ndiyo kitu sahihi kwako?
Katiba IPI inasiginwa?leo unaitisha maandamano ya kupinga serikali, alafu unataka huyo huyo kiongozi aliyeko madarakani awaruhusu mumpinge, inakuja kweli?
 
Mleta uzi unataka Rais magufuli atolee mfano nchi gani zaidi ya Libya hapa afrika? Libya ni mfano mzuri wa nchi ya kiafrika iliyo tumia rasilimali zake bila misaada kunyanyua maisha ya wananchi wake

Kuna mfano bora kama huo hapa afrika? Mi siuoni
Botswana
 
Tunampenda rais magufuli,nyinyi mshazoea wizi ndio maana hamumpendi
Aaaaah wapi ...hii inakula kote !! Sasa maisha mbona magumu sana kuliko kipind cha nyuma. acha zako wewe huyo magufuli nani yako mbona ubamtetea anapokosea
 
Katiba IPI inasiginwa?leo unaitisha maandamano ya kupinga serikali, alafu unataka huyo huyo kiongozi aliyeko madarakani awaruhusu mumpinge, inakuja kweli?
Ukitaka kuongoza vizuri ukubali kukusolewa pale kwenye marekibisho yafanyike zote tutafika. Kupewa uongozi si maana yake unajua sana kuliko wengine.
 
Ukitaka kuongoza vizuri ukubali kukusolewa pale kwenye marekibisho yafanyike zote tutafika. Kupewa uongozi si maana yake unajua sana kuliko wengine.
Kukosoa sio kwa kuweka watu barabarani. Alafu unaishinikiza serikali ikae kwa makubaliano?hakuna serikali ya hivyo
 

Tatizo sio vyama vingi (oppositions), tatizo kubwa ni vyama tawala.

Kwa mfano angalia Zambia ambapo Dr. Kaunda alikubali kwa moyo mkunjufu mfumo wa vyama vingi, na katika uchaguzi wa Zambia 1991 laiti kama Serikali ya Dr. Kaunda au chama chake cha UNIP vingekuwa kama CCM ilivyo na serikali yake basi Kaunda asingeshindwa na Chiluba.

Lazima pawepo na Tume Huru ya Uchaguzi + Sheria za Uchaguzi kama moja ya mambo ya msingi sana katika kuwa na chaguzi huru na zenye tija kwa nchi zetu. Lakini kwa nchi nyingi za Afrika, mfumo wa saiasa ya vyama vingi ni kama vile tulilazimishwa.

Je unakumbuka maoni ya Tume ya Jaji Nyalali kuelekea mwaka 1991-92? Ni mangapi ya msingi yaliyotekelezwa na watawala wetu? Ni kama vile tuliogopa/tunaogopa Wazungu zaidi ndio maana tuna hii mifumo lakini ki-uhalisia hakuna utayari upande wa watawala wetu. Na kwa bahati mawazo yako na ya watawala wengi yanafanana i.e. kutoheshimu au kupalilia demokrasia na uhuru wa kweli kwa kuona kuwa oppositions hawana jipya wala nafasi ya kuleta maendeleo au fikra mpya.

Hivyo badala ya kulaumu jumla jumla ni vema kuchunguza na kubaini chanzo cha tatizo.
 
Hatutaki rais wa kutufuga kama mifugo yake kule chato, Kwamba ukishawapa majani basi ni kuwafungia zizini. Ukipata wageni unachinja mmoja!! NO NO NO huyu hatukumchagua wa hivyo!!!
 
Sawa mkuu vile inategemea uungwana wa viongozi!! wengine wanafikiri wakiwa maamiri jeshi ni kutawala tu kwa mkono wa chuma. Hawa wanaosema waombewe huku wakiwa na roho za visasi ni majanga tu hata ungeweka tume huru!! damu itamwagika kuliko waachie kwa sanduku la kura!!
Nimechukizwa mno na kauli zake huko pemba na ZNZ nina uhakika kuwa huyo muungwana Dr Shein analazimishwa tu dhambi lakini hayuko hivyo!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…